Under-cover
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 1,834
- 3,042
😥 Wakuu hapa nipo hospitali namuuguza ndugu fulani hivi ila nimekumbuka mbali sana, ni sehemu ambapo 2022 nililazwa, basi nilikuwaga nimepata kimanzi changu first year wakati niko third year, ndugu yangu kalazwa kile kile chumba nilicholazwa tofauti ni kitanda tu, sasa nipo kwa pembeni hapa nakiangalia kile kitanda nilipolazwa, naangalia sehemu ile babe mama yule alipokuwa ameketi pembeni yangu huku amenishika mkono tukiongea mengi moja wapo ni ile neno nilimwambia mamy usije ukaondoka maishani mwangu, basi ile ananiangia kwa mahaba na kuitikia, vile alivokuwa anakatisha masomo mchana anakuja hospitali na kuniletea matunda ile caring aisee nilihisi nimependelewa, bado nikitoka nje nikitembea mida ya night nakumbuka tulivyokuwa tunatoka namsindikiza huku kukiwa na baridi, tena usiku yaani kama wakorea fulani hivi, tumeshikana na kucheka, aisee nilimpenda sana yule manzi wa kimeru (R) na kile kiwimbo cha only you cha Christian Bela na Rosa Lee, ila ndio yakatokea ya kutokea tulishaachana, sikuwahi kutamani mwingine nilimfanya 1 & only i, eti leo hatuongei, maadui, mapenzi ni umbwa.🚮🚮