Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
Tulio wengi Tumetokea kijijini kama sio sisi basi wazazi wetu na kama sio wazazi wetu basi hata babu na bibi zetu.
Sisi ni wale watoto wa tabaka la walio wengi. Yaani tabaka la watu masikini.
Leo tupo mjini tunapambana. Maisha yetu bado sio mazuri na hatujafikia zile ndoto kubwa zilizotusukuma kuja huku mjini kutafuta.
Hatujui tutafanikiwa lini lakini tuna imani kubwa sana juu ya Mwenyezi Mungu mgawaji wa riziki kwamba ipo siku na sisi tutapata walau cha kuwafuta machozi wazazi na ndugu zetu ambao hawajachoka kutuombea.
Picha ama taswira za maisha ya kijijini kwetu zinatukumbusha mazingira ya huko nyumbani ambayo bado sio mazuri na yanatuumiza vichwa sana.
Tunaumia sana kuona yale mazingira mabovu bado hatukuweza kufanya chochote cha maana kuyaweka kwenye hali nzuri na kufuta ile dhana ya umasikini kwenye familia zetu.
Japo kuna wenzetu wachache huku mjini ambao hali zao ni alhamdulilah lakini hawapo tayari kutushika mkono na kutuvuta walipo wao wakihofia tutawavuta tulipo sisi.
Nadhani labda wenzetu hao wamesahau zile nasaha za wazee wetu waliposema "kidogo chetu na kizuri kula na ndugu zako."
Taswira za maisha huko kijijini kwetu zinatukumbusha umoja na mshikamano kama siraha pekee ya kupambana katika vita dhidi ya umasikini.
Sherehe zetu huko kijijini kwetu hasa hapo zamani nakumbuka tulizifanya pamoja kama watoto wa nyumba moja. Huko kijijini kwetu vyakula vilipikwa na tulikula pamoja kwenye nyungo na tulishare furaha.
Huko ngoma zilipigwa na tulicheza pamoja, wakubwa kwa watoto, wanawake kwa wanaume sote tulicheza na kusahau shida zetu.
Kuna zile tanga ndugu baada ya msiba, nazo tulishiriki pamoja hadi na majirani zetu lakini siku hizi hata hao ndugu wa familia siku hizi wanasema "sisi ni ndugu zao wa mbaaaali sana. Dah! Inaumiza sana.
Ndugu zangu tuliotokea kijijini, hawa watoto wa kishua huku mjini wasitusahaulishe tulipotokea. Tuishi nao vizuri na tujifunze mazuri kutoka kwao yatakayosaidia sisi kuinuka kimaisha na kiwainua wenzetu wanaotutegemea.
Ndugu zangu tugangamale sana, maisha ya mjini hayataki uwe lelemama. Tusikae kinyonge wanangu. Tupeane michongo ya pesa na dili za maana ili siku tukirejea nyumbani ndugu zetu watupokee kwa tabasamu.
Kufanikiwa kama wao ilo linawezekana mbona!! Kikubwa jitihada zetu na neema za Mwenyezi Mungu.
Kama unapapenda kijijini kwenu like, comment na share ujumbe huu kwa watu wengine wengi.
It's me
Mr George Francis