Nakushauri Upambane katika elimu, utashinda

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
KUHUSU ELIMU !

Usiogope kuchelewa kupata kwa ajili ya muda mwingi unaoutumia katika kuitafuta elimu, jipe moyo kwa kuwa unautajiri ubongo wako kwa utajiri utakao kufa nao.

Milele, elimu yako ni utajiri utakaoufaudi mwinyewe na kwa wingine itakuwa ni zawadi.

Soma kwa ajili ya kupata maarifa kwani elimu inapanua ubongo wako na kutoa nafasi ya kuwaza mengi.

Maarifa uyapatayo leo ndio na muongozo katika maisha yako ya leo.

Elimu ni nyota isiyozimika.
Elimu ni taa penye giza.
Elimu ni mbalamwezi katika giza.
Elimu ni mvua kwenye ukame.
Elimu ni furaha penye huzuni.

Itafute kwa nguvu zote kwa kuwa unamuda sasa.

Kubali kuwa mjinga ili upate ujuzi usioufahamu, kukubali kutokujua ni mwanzo wa kufahamu zaidi ya usioyajua.

Maoni na ushauri:
0755519736 au nitafute ktk email ya iddyallyninga@Gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…