Mkuu Ndomaana Nikasema Atoe Mazingira Na Scenario Nzima Iwe Disclosed. Labda Hatuamini Au Anaona Uvivu Kuandika. Maelezo Yake Yako Too Vague,Na Hayakupi Mtu Mwanga Wa Nini Unafanya. Btw Niliposema Sanasana Sikumaanisha Solerly Ni M-P. Afterall Hawa Ndo Wateja Na Apo Ana Hasira Anataka Kukomoa Au Alikua Hajui Kaambiwa Anaweza Kulipwa Akachangamkia Fursa Kisa Kuna Fedha Ndo Kaja Apa Aone Uwezekano Upo Wa Kupiga Iyo Ela.
Pamoja Katika Sheria!!
Walifika polisi wawili wakiwa na wazazi wa mtoto husika,pamoja na mwalimu wa shule anayosoma huyo mtoto.Mtoto mwenyewe aliyeelezwa kuwa kabakwa ana umri wa miaka 7 mpaka 8.
Walifika nyumbani kwangu na kumkuta mtoto wangu wa kike na kuulizwa na askari ambaye alivaa kiraia kama kuna mvulana mwanafunzi wa shule fulani.Alipowajibu kuwa yupo waliomba picha yake na yule mtoto wangu akaingia ndani akawapa.
Waliichukua na kumuonyesha yule mtoto ambaye alikuwa analia kwa kipigo toka kwa polisi,na kumuuliza ni yupi aliyembaka ni yupi ambapo kulikuwa na watu wawili akamwonyesha mtoto wangu ambaye alikuwa amevaa sare ya shule.
Wakaondoka mpaka shuleni na kuomba wafanye gwaride la utambuzi(Identification Parade).Walifanya na mtoto hakuweza kumtambua japo askari aliyekuwa anaendesha gwaride alipofika alipokuwa amesimama huyo kijana alisimamishwa na askari na kuonyeshwa kwa kidole kama hamtambui.Mtoto wa kike alikataa kumfahamu muhusika.Ila mwisho yule alimtaja kijana mwingine.Polisi walimchukua yule kijana wakamuhoji kwenye ofisi ya mwalimu kisha wakamuacha.
Baada ya hapo polisi walimwambia mwalimu kuwa tunaomba kuondoka na mwanafunzi ambaye tunayo picha yake,japo kwenye gwaride hakutajwa.Mwalimu aliwahoji kivipi wakasema tunakwenda kujiridhisha.Aliombwa na mwalimu kuandika alichofanya pale shuleni kwenye Logbook ya shule.Alikubali kuandika, ila kabla ya kuondoka pale shuleni yule polisi aliwaweka pamoja mtoto wangu na yule mtoto aliyesemwa amebakwa na kuwakutanisha na kumuuliza hata kama anamfahamu tu mtoto alikana kumfahamu wala kumuona.
Cha ajabu bado polisi waliondoka na mtoto wangu mpaka kituo cha polisi,ambapo alihojiwa na askari wa upelelezi na wote wakakubaliana kuwa yule kijana hahusiki na tukio lile.
Kwa pamoja waliafikiana kumuachia ila wakamwambia aje baada ya wiki moja.
Siku ya pili katika hali isiyoeleweka aliitwa tena kituo cha polisi na kufanywa gwaride kwa mara ya pili yule mtoto ndio akamtaja mtoto wangu kuwa ndiye aliyembaka.
Baada ya hapo akawekwa ndani na kunyimwa dhamana mpaka siku ya tatu akapelekwa mahakani na kushitakiwa kwa kosa la kubaka.Tukamtoa kwa dhamana mahakamani.
Kesi ikaanza kusomwa, PH tu ilichukua wiki tatu mwendesha mashtaka kila ikisomwa anasema upelelezi haujakamilika.Mpaka hakimu alipoanza kuwafokea.
Maelezo ya awali(PH) yaliposomwa mashahidi ikawa kazi kuja waliitwa mara nne bila kufika mara ya tano wakaja mashahidi baadhi.Kesi ilianza lakini huyu mtuhumiwa alisimama imara sana kuuliza maswali mashahidi mpaka wengine kuchanganyikiwa na wengine kuhamaki mahakamani.
Huyu kijana alifanyakazi nzuri sana maana mpaka askari wenyewe walikwama katika maswali aliyokuwa anauliza.
Kifupi aliwashinda mashahidi wote na hawakuwa na hoja aliyemaliza kazi ni mtoto mwenyewe aliiambia mahakama kuwa hakubakwa ila walikuwa wanamlazimisha aseme kisichokuwepo.
Shahidi wa mwisho daktari aligoma kabisa kuja mahakamani pamoja na kuitwa mara 4 hakutokea mahakamani.
Ikamlazimu hakimu kufunga ushahidi na kutoa hukumu kwa kuzingatia mashahidi waliopo na kufuta kesi.
HITIMISHO
Kinachonipa uchungu ni muda niliopoteza,mtoto kapoteza mwelekeo katika masomo ukizingatia alikuwa na uwezo mkubwa sana darasani,na huu ni mwaka wake wa mwisho.Zaidi ya yote familia imepata athari kubwa kiuchumi na kijamii.Nimepoteza kazi ambayo ilikuwa nilipwe zaidi ya laki 6 kwa mwezi kutokana na kesi hii.