Kiteitei
JF-Expert Member
- Jan 14, 2009
- 1,595
- 1,540
Naomba msaada wa kisheria juu ya kuwashtaki hawa dawasco, ninaishi boko na maji yamekatwa takriban siku ya nane leo, ninefuatilia dawasco boko jana nikapewa majibu rahisi kuwa kwa siku za jumatano, alhamisi na ijumaa maji huwa yanahamishwa boko, nilijaribu kumueleza huyo mtu wa dawasco kuwa majirani zangu maji yanatoka akadai hayo ni yale yaliyobakia kwenye bomba, hivyo nisubiri hadi jumamosi ndio nirudi kwao,haikuwa kweli kwani kwa majirani maji hayajakatika hadi leo hii! Huyu mtoa huduma hakuwa tayari kunisikiliza na alitoa majibu mengi tu ya kejeli!
Nimefuatilia jana jioni na kugundua kuwa bomba letu lilikatwa na hawa jamaa wanaoweka fibre optic cable na watu wa dawasco walikunja bomba na kulifunga badala ya kuliunga!
Naomba kujua nianzie wapi kuwashtaki hawa watu na je ni wajibu wa nani kuliunga hilo bomba.. ie mteja, dawasco au waliolikata...ahsanteni