Nakutakia kila la heri Wallace Karia lakini usimsahau Ally Mayai Tembele

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Posts
1,544
Reaction score
943
Ndugu zangu, kama mnavyofahamu mimi ni mfuatiliaji mwenye uchungu na mpira wetu wa Bongo na nilionyesha kutoridhishwa kwa kiwango kikubwa na hali ya utawala usio bora kutoka TFF ya Jamal Malinzi. Mimi ni muumini wa dhana ya utawala bora na kwa kiwango kikubwa eneo hili ndilo lililomwangusha Jamal Malinzi na wenzake, hata tulipopiga kelele kuponda uongozi wake wapo wengi hawakuelewa tunamaanisha nini.

Hata hivyo, ni bahati mbaya utawala wa Malinzi ulimuhusisha Wallace Karia kama Makamu wa Rais kwa hiyo doa hili la utawala usiozingatia maadili ya kiuongozi hawezi kulikwepa pia.

Lakini baada ya kuchunguza na kuwachambua wagombea nafasi ya Urais wa TFF na kulinganisha na hali halisi ya mahitaji ya mpira wetu, nimefikia uamuzi wa kumtakia kila la heri Wallace Karia ambaye sasa hivi ndiye anayekaimu Urais wa TFF. Na kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia, anapewa nafasi kubwa ya kuibuka kwa kishindo katika uchuguzi huu wa leo.

Zipo sababu kadhaa, na nitataja nne zinazompa turufu Wallace Karia kuibuka kidedea kwa sababu mpira wetu unamhitaji.

1. Wallace Karia ni TFF presidential material! Ana haiba ya uongozi kwa ngazi ya juu. Anazungumza kama kiongozi, ana act kama kiongozi, anajitambua kama kiongozi kwa ufupi ana hadhi ya kuongoza taasisi katika ngazi ya juu. Uzoefu wake kama kiongozi wa kiserikali kwa nafasi za ukurugenzi, na hata timu za mpira hasa Coastal Union, kuna mpa turufu ya dhidi ya wagombea wengine hususani Ali Mayai anayeonekana kuwa kipenzi cha wadau wengi.

2. Karia hajijiambatanisha sana na mapenzi ya timu zetu mbili kubwa na kongwe Simba na Yanga na anavyo anaonekana kuwa mtu anayeweza kuaminika na pande zote. Kusema ukweli hadi muda huu naandika haya sijui yuko mrengo gani japo hili sio muhimu sana. Kuwa shabiki na hata mnazi wa kupindukia wa timu hizi sio dhambi na wala haipaswi kuwa turufu ya mtu kuwa au kutokuwa kiongozi. Tatizo linakuja kwenye IMANI. Je unaweza kuaminika na pande zote kuwa utakuwa fair? Je rekodi zako za uongozi zimeacha alama gani huko nyuma? Nafasi ya kipekee kwa Karia ni ile hali ya kutokuwa maarufu miongoni mwa wapenzi wa Simba na Yanga - kunaweza kumpa nafasi nzuri zaidi ya kutekeleza majukumu yake bila pressure kutoka kwa timu hizi na wafuasi wao.

3. Hana kashfa ya utovu wa uadilifu. Huyu tayari amekuwa kiongozi na hata sasa ni kiongozi wa TFF inayomaliza muda wake na ambayo imelalamikiwa sana kwa vitendo vya rushwa, upendeleo, ukabila, upangaji matokeo na mambo yanayofanana na hayo lakini jamaa katoka akiwa 'Mr. Clean'! Unajua mtu anaweza kuwa mwadilifu au kujifanya mwadilifu pale anapokuwa hana madaraka au nafasi ya kupiga! Huyu ameshakuwa kiongozi lakini bado ametunza heshima yake. N ndio maana pamoja na kuwa alikuwa pamoja na akina Malinzi, ameprove kuwa hakuwa chanzo cha 'ujinga' wote uliokuwa uanfanyika. Inaonekana hakuwa 'insider' japo alikuwa na cheo cha juu. TFF inamhitaji mtu wa aina hii.

4. Sera zake zinaonyesha ni mtu anayejua tunahitaji nini. Wengi wanakariri vitu vilevile kama kutafuta udhamini, maendeleo ya soka la vijana na timu bora ya taifa. Haya ni matamko tu hata akina Malinzi walikuwa na matamko mazuri zaidi kuliko haya ya sasa lakni wamekwama kwa sababu hawakuonyesha watafanyaje. Pia hawakupima risk ya utekelezaji. Sasa sikiliza Karia anavyosema: UWAZI, UADILIFU NA UWAJIBIKAJI. karia amesema atafanya vitu vidogovidogo vinavyotekelezeka!!!! Katika dhana ya uongozi na operesheni tunaita continuous improvement.
Amesema ataanza na kujenga nidhamu ya muundo wa kitaasisi utakaotoa nafasi ya ushirikishwaji usio wa hila kwa kamati ya utendaji. Kwa lugha rahisi amesema TFF kama taasisi imekwama kwa sababu haikujenga nidhamu ya kitaasisi, ndio maana tuliona kamati zikilumbana, maamuzi yakitenguliwa, kushikana uchawi, chauguzi kuendeshwa kimizengwe, n.k.

Ni hadi ujenge taasisi imara ndipo unaweza kuvutia kuaminika na udhamini bomba amabo utakuwa nafasi ya kutekeleza programmu nyingine za kiufundi na kimaendeleo.


MUHIMU: Kwako Karia baada ya kuapishwa tafadhali sana mkaribishe Ally Mayai Tembele, umtumie kwa kadiri ya uwezo wake maana huyu ni mmoja kati ya wagombea makini lakini anahitaji kuthibitishwa katika uzoefu
 
aliecheza aongoze mpira.... mambo ya siasa yamepitwa na wakati...mwanajeshi ndie anaekuwa mkuu wa majeshiiii....
 
Ally mayai ndiye mtu sahihi hapo hao wengine ovyo tu .

Kama tunataka maendeleo ya mpira ally ndye chaguo sahihi lakini kama tunataka siasa ndani ya Mpira tuendelee na hawa wauni.
 
Tenga pia alikuwa mchezaji wa zamani wa timu fulani.... Lakini naona kama alifanya vizuri tu pale TFF

"A voice of one calling in the wildernes"

Tatizo sio tu kuwa mchezaji, Tenga ni kiongozi kwelikweli tena alikuwa na uzoefu wa kutosha.
 
Karia hana hizo sifa ulizozitaja. Tuulize tunaomjua tukuambie. Shida mojawapo ya mpira wa Tanzania ni watu kuendekeza njaa zao na kuzipeleka kichwani, hivyo kushindwa kufikiri kwa ufasaha

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha kuhukumu watu, sio kila binadamu anaendeshwa na njaa. Huu ni mjadala tu, toa unachokifahamu kuhuyu mgombea huyu au yeyote.

Ila nakiri wazi simfahamu huyu Karia kibinafsi, ninamhukumu kama kiongozi, nitashukuru kujua ukweli wa upande wa pili kumhusu
 
Hii ndo Tanzania bhana ingekuwa mashabiki wa soka la Tanzania tungekuwa tunapiga kura mayay angekuwa rais ila huko kwa wenzake lazima wampige chini ila jamaa anakubalika sanaaaa kika la kheri mayay
 
aliecheza aongoze mpira.... mambo ya siasa yamepitwa na wakati...mwanajeshi ndie anaekuwa mkuu wa majeshiiii....
Mzee samahani Karia ameucheza mpira. Na alikuwa mchezaji mzuri kwa kiwango kizuri. Na ujue wengi tuliacha kucheza kwa ajili ya shule na kukosa kushiriki vyema kwenye soka.
Ni wachache sana waliofanikiwa kucheza mpira na huku wakisoma, mmojawapo ni Bwana Karia. Na hata ukimuangalia Ally Mayai, yeye alipata ziro form six, si kwamba hakuna kitu kichwa la hasha, kwa kuwa ilikuwa vigumu sana kwake kuweza kuihudumia Yanga na pia kupata wasaa wa kusoma. Mzee, usimhukumu mtu kwa kuwa hufahamu historia yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…