SoC03 Nalilia kizazi changu

SoC03 Nalilia kizazi changu

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jul 22, 2022
Posts
20
Reaction score
38
Nalia juu ya kizazi changu,nalilia kizazi changu,Nalilia kizazi cha taifa langu,hakuna mzazi afurahiaye kuharibika kwa binti au kijana wake wa kiume.Ulimwengu unapoenda hakuna ajuaye,Watoto wengi na vijana wengi wamekuwa wakiendeshwa na ulimwengu wa sasa.

Nani apendaye kumuona kijana wake wa kiume akipotea na kuwa shoga,Wazazi wengi huwa na mategemeo makubwa kutoka kwa watoto wao na vijana wao wazazi wengi hutegemea watoto hao kuwa vichwa vya familia hapo baadae na hata MwenyenzI Mungu akijalia kuwaletea wajukuu lakini kwa wakati wa sasa mambo ni tofauti watoto wa kiume au vijana wa kiume wanabadilika na kuwa na tabia na mwenendo wa kike,Wapi ulimwengu unapoenda yule aliyetegemewa kuwa baba na kaka anajifanya kuwa dada.

Hivi ni kweli taifa linaweza kusonga mbele kwa hali hii ya vijana kuangamia na kupotea,Tatizo hili la vijana kupotea kwenye ushoga linachangiwa kwa kiasi kikubwa na malezi ya wazazi kwa watoto wao,Wazazi wengi husahau majukumu yao ya malezi na kuwaachia dada wa kazi kulea watoto wao kupitia hao hao wadada wa kazi wasiojitambua huwaribu watoto mapema mpaka mzazi atakapokuja kushtuka anakuwa ashachelewa pia tabia ya wazazi kuwaruhusu ndugu pamoja na wageni kulala pamoja na watoto nayo inachangia watoto kuharibika mapema maana kuna kesi nyingi sana zinazotokea majumbani ambapo utakuta ndugu wa karibu anaweza kuwa mjomba,baba mdogo na rafiki wanawaingilia watoto wa kiume na kuwatishia kuwapiga endapo watasema mfano kesi ya Halfan Rajabu Mohamed v jamhuri

Kwenye kesi hii mtoto wa kiume alikuwa akiingiliwa na mlinzi ambaye pia alikuwa mtunza bustani kila siku bila wazazi kujua mpaka pale mama alipokuta nguo ya ndani ya mtoto wake ikiwa imetupwa kwenye za kusafishia sakafu ikiwa imechafuliwa na kinyesi.Utafiti uliofanywa na serikali kwa kushirikiana na shirika la watoto ulimwenguni(UNICEF)unaonesha asilimia 60 ya matukio yanatokea nyumbani na asilimia 40 yanatokea shuleni.

Hivyo utafiti huo unaonesha chanzo kikubwa kinatokea nyumbani hivyo kipindi cha sasa mzazi unapaswa kuwa makini na mtoto na usimuamini mtu yoyote maana vitendo hivi vya ulawiti na kuingiliwa kwa watoto hufanywa na watu wetu wa karibu sana,sasa hivi hata madereva watoto wetu (school bus driver)wamekuwa wakishiriki kwenye vitendo hivi vya ukatili dhidi ya watoto.

Hivyo ewe mzazi unapaswa kutengeneza urafiki na ukaribu na watoto wetu ili waweze kufunguka na kueleza kila jambo ambalo analopitia akiwa shuleni,nyumbani,bwenini na kwenye (school bus),Lolote lile liwe nzuri au baya atakalokuwa anafanyiwa anaweza kukuambia bila kuficha kwa kuwa utakuwa rafiki yake.

Pia ni vizuri kwa wazazi kuwapeleka watoto bweni wakiwa katika umri sahihi wa kutambua nzuri na baya maana huko ndiko chanzo kikubwa cha ushoga na usagaji lakini pia sheria ipo wazi dhidi ya masuala haya "Sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria ya Tanzania imetamka bayana kwamba vitendo vya mapenzi ya jinsia moja au kinyume na maumbile iwe kwa faragha au makubaliano ni kosa la jinai, hivyo hii sheria inahitaji utekelezaji wa hali ya juu ilimradi kuinusuru jamii yetu,Serikali pekee yake haiwezi kama jamii ikiamua kuwa kipofu na kiziwi juu ya masuala haya.

Wanajamii wanapswa kushirikiana na serikali katika kuwaibua watendaji wa makosa haya bila kuogopa,Mimi nikifunga kinywa changu na kuyaziba masikio yangu na wewe ukafanya hivyo kwa kuogopa kizazi chetu kitazidi kupotea na kuangamia,Fungua kinywa chako kusema na kukemea masuala haya bila kuogopa ili kuondoa kilio hichi juu ya kizazi chetu.

Wazazi tutafute pesa kwa bidii kwaajili ya kulea watoto wetu ila tusisahau majukumu yetu ya malezi kwa watoto wetu.
 
Upvote 10
Back
Top Bottom