Do your homework mkuu. Moja ya hatua za mwanzo katika kufungua biashara ni kuyasoma mazingira ya sehemu goli lako lilipo au linapotarajiwa kuwepo. Ni kitu gani kinakosekana huo mtaa/eneo? Usiende mahali kufungua saluni ya kiume wakati hapo mtaani tayari kuna saluni nne za kiume za nguvu; kuwa mbunifu na ufungue business ambayo kila mtu hapo mtaani atakuwa hana sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kwako. Pili,fanya utafiti kuhusu bidhaa upatikanaji wa bidhaa ambayo utakuwa unaiuza pamoja na bei ya wastani ya bidhaa hiyo kwa ujumla. Kwa mfano unataka kufungua bucha ufanye utafiti kujua ni wapi utakuwa unanunua nyama kwa ujumla, au kama ni kuletewa na meat vans na gharama yake. Pia lazima ujiulize na utafiti kuwa washindani wako watakuwa ni kina nani? na uwachunguze washindani wako na ujue mapungufu yao kisha uwe na kitu cha ziada kuwazidi wao.
Pia ni lazima ujue tabia za hao watu ambapo goli lako lipo ni kitu gani hawapendi, tabia zao katika manunuzi ya bidhaa unayotaka kuiuza, n.k.
Kwa ufupi mkuu sisi hatuwezi kukushauri ni biashara gani uanzishe kwa sababu hatujui taarifa zote hizo hapo juu na mengine mengi ambayo sijayataja(hobby yako,uvumilivu wako,n.k), lakini wewe taarifa hizo unazo na kwa ambazo huna ni kazi na wajibu wako kuzitafuta kabla ya kuanzisha hio biashara. All the best mkuu