Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Taarifa zaidi hii hapa
Mawakala wa Forodha pamoja na Wasafirishaji wenye magari zaidi ya 500 wa Tanzania wamefanya mgomo ikiwa ni siku ya pili katika mpaka wa Namanga uliopo katika Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wakishinikiza kupunguzwa kwa utitiri wa kodi pamoja kutokea kwa sintofahamu kwenye mashine za EFD kwa Wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa kwenda nje ya Nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Forodha katika mpaka wa Namanga, Alois Makyao amesema wamesitisha usafirishaji na kuomba mfumo kuwekwa sawa ikiwemo ucheleweshaji wa ukaguzi na kusema sasa magari zaidi ya 500 yameshindwa kwenda Kenya baada ya mgomo huo na kuiomba Serikali kuingilia jambo hilo kwa kuwa Serikali pamoja na Wafanyabiashara hao wanapoteza mapato kwa wap kuendelea kukaa hapo mpakani.
@AyoTV_ imemtafuta Meneja wa Forodha wa TRA katika mpaka wa Namanga Edwin Changwe ambapo amesema kuwa yeye hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa hayupo ofisini na kuhusu mgomo huo unaondelea hana taarifa zake, bado Ayo TV inaendelea kuzitafuta Mamlaka nyingine za Serikali ili kupata kauli yao.
Pia soma
- Taarifa kwa Umma kuhusu mgomo wa wasafirishaji Namanga