Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu,
Kwanza naomba niseme kuwa ninaufahamu, na kuuelewa vizuri ule msemo unaosema kuwa nyani akitaka kufa "basi miti yote atayojaribu kuishika hutereza". Hivyo nafahamu fika kwamba ule muda wa mwenyekiti ambae pia ni namba 1 wa chama kufa kisiasa upo, lkn sikutegemea kama muda huo ndio umeshafikia sasa hivi mpaka nilipoanza kusikia, na kuona mwenyekiti huyo wa chama kikuu cha upinzani, aliewahi kujijengea heshima kubwa katika siasa za Tanzania akijiaibisha kwa kujibishana na wakili fulani kanjanja anaetokea katika mkoa wa Mbeya, huku akishindwa kuelewa na kutambua kwamba kwa cheo chake, hadhi yake, umri wake na hata ukubwa wa chama chake hakutakiwa kamwe kupoteza muda wake, energy yake, sauti yake na mimbari ile kumjibu huyo wakili kanjanja na mlevi wa gongo.
Ni nani mwenye akili timamu asiefahamu kuwa wakili kanjanja yule alitumwa na yule Dr aliekuwa anashindia mihogo akarushe jiwe gizani, ili aone au asikie nani atakaemjibu, na yeye Dr mihogo apate pa kutokea na pengine kurudi tena kutrend katika midomo ya watu?
Suala la bandari limekufa kibudu, maandamano wanayopanga bila baraka ya chama chochote cha upinzani kuwa nyuma yao pia yameshakufa kibudu kabla hata ya kuanza, hivyo njia ya mwisho kwa wao kurudi tena kutrend ni hiyo ya kuattack vyama na viongozi wa vyama ili kujipatia uchochoro wa kutokea katika magazeti, mitandao na vyombo mbali mbali vya habari.
Sipingi yule kanjanja kujibiwa, ila napinga mtu alietumika kumjibu. Kiongozi mkuu wa chama kikuu kupoteza muda wake kumjibu wakili kanjanja na mlevi ni kujiaibisha yeye na chama chake. Ndiomaana hata makamu wa chama hajaonesha kulipa uzito sana swala hilo, maana anaufahamu mtego uliotegwa na Dr mihogo hivyo kawapuuza. Kitendo cha kumjibu yule kanjanja ni sawa na mtu mzima kumpiga mtoto wa miaka mitatu makonzi eti kisa alikuzomea, na wakati ungetumia hata njia ya mkato kwa kumpa kazi hiyo mtoto wako wa miaka minne amshikishe adabu.
Kwa kawaida yule kanjanja na aliemtuma walitakiwa wajibiwe angalau na katibu mkuu, au mwenyekiti wa chama wa kanda au mkoa wake, au chawa wengine humu JF.
Namalizia kwa kusema kuwa kile ni kinyago mlichokichonga wenyewe na kutaka kukitumia kisiasa katika swala la bandari, na mambo mengine ya kisiasa, hivyo pamoja na kwamba kinyago hicho kinaonesha kuasi kambi, lkn bado hakina sifa wala levo ya kujibiwa na mwenyekiti na namba 1 wa chama.