Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Zoezi la kuchukua fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ule wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao limeanza hii leo.
Habari kutoka Zanzibar zinaeleza kuwa tayari Mbwana Juma Bakari na Ali Abeid Karume wamefungua dimba la kuchukua fomu za kuwania Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM.
Zoezi hilo litakamilika Juni 30, 2020 ambapo kwa upande wa Bara fomu zinatolewa katika ofisi za CCM Makao Makuu, Dodoma na kwa upande wa Zanzibar fomu hizo zinatolewa katika ofisi kuu za CCM Kisiwandui.
Chama cha Mapinduzi kilitangaza rasmi utaratibu wa kuchukua na kurejesha fomu kwa wagombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo juni 15 na mwisho wa kurejesha fomu hizo ni Juni 30, 2020 saa 10:00 jioni.