Kwanza Umimi Mwalimu angejiuliza tu kuwa ni kwa nini Miaka ya nyuma mikoa ya Kilimanjaro ,Kagera na Mbeya ilikua na walimu wengi vijijini ?
Mfumo wa ajira usiozingatia uhalisia na ukweli wa jamii yetu ni tatizo kubwa sana.
Ukinipa kazi ya kufuta tatizo la uhaba wa walimu vijijini wala situmii mikwala wala vitisho ni jambo dogo sana.
Kwanza ni lazima serikali ifahamu kuwa Walimu wenyeji au wazawa ndio wenye uwezo wa kufundisha shule za msingi za vijijini .
Kuna watoto wa vijijini hawajui kiswahili kabisa. Hawa hua wanawaelewa zaidi walimu wenyeji.
Mzaramo hawezi kumfundisha mtoto wa darasa la kwanza wa Kisukuma akamuelewa labda awe na akili ya ziada.
Hivyo njia rahisi ni kwenda kule Nampembe na kutangaza ajira ya ualimu na kipao mbele ni wenyeji. Hao wataishi kwao, wataoa kwao au kuolewa kwao na watakua na uchungu wa kuwafundisha watoto wao na ndugu zao.
Kwa sasa unamwajiri Mkikuyu kule Nkasi halafu anaolewa na mkikuyu Mwenzake anayeishi Mwanza ,unategemea nini kama sio kuomba uhamisho. Kwanza hana mapenzi kabisa na mazingira hayo na hata watoto na wakazi hao anawaona kama chumaulete tu.
Miaka ya nyuma mikoa iliyokua na walimu wenyeji ndiyo iluyokua inafanya vizuri.
Mmasai hawezi kumfundisha kwa mifano mmanyema.
Kuna watakaosema ni ukabila lakini ni suala la kubalansi ajira na kuinua kiwango cha elimu vijijijini na kuleta maendeleo. Hata mzunguko wa kifedha utakua mkubwa mana kijana akipata ajira kijijini kwake atajenga na kuwalea wazazi wake kwa karibu na kuanzisha miradi kijijini. Mgeni anawaza kuhama tu muda wote.