Zanzibar 2020 Namba 3: Kada wa CCM, Mbwana Yahya Mwinyi achukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar

Zanzibar 2020 Namba 3: Kada wa CCM, Mbwana Yahya Mwinyi achukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Eas75rIXYAE2DDS.jpg

Zoezi za kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) limeendelea ambapo Mzanzibar mwingine Mbwana Yahya Mwinyi amefika katika ofisi za chama hicho Kisiwandui mjini Unguja na kuchukua fomu hizo kwa lengo la kuwania nafasi hiyo.

Mbwana Yahya Mwinyi anakuwa mwanachama wa tatu kupitia chama hicho kujitokeza kuchukua fomu hizo tangu kuanza kwa zoezi hilo siku mbili zilizopita.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mgombea huyo amesema baada ya kujipima na kuhakikisha kuwa ana vigezo vyote vya
kugombea Urais pamoja na kujiridhisha ndio njia moja wapo iliyompa hamasa ya kugombea nyadhifa hiyo.

Amesema hadi sasa Chama cha Mapinduzi hakina mgombea rasmi ambaye ameteuliwa kuwa ni Rais wa Nchi jambo ambalo lililompa hamasa ya kuchukua fursa hiyo.

Hata hivyo amehakikisha kuwa atakapopata nafasi ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar ataulinda na kuutetea Muungano wa Tanzania na kuitumia vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa ajili ya maendeleoya Nchi.

CCM ilifungua milango kwa wanaoomba nafasi ya uteuzi kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri na Zanzbar kuanza kuchukua fomu na kutafuta wadhamini ambapo mwisho ni June 30.
 
Back
Top Bottom