Uchaguzi 2020 Namba 4: Wakili Gaspar Mwanalyela achukua fomu ya kugombea Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Namba 4: Wakili Gaspar Mwanalyela achukua fomu ya kugombea Urais kupitia CHADEMA

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wakili Gaspar Mwanalyela amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea Urais kupitia Chadema ambapo moja ya vipaumbele vyake amesema atafumua mfumo wa elimu nchini na kusuka upya sambamba na kuahidi kutatua tatizo la ajira nchini.

gaspar.jpg


Wakili huyo amesema, ameamua kugombea ili kurudisha matumaini kwa wananchi walio na hofu na wenye kukata tamaa.

Amesema, atafuata nyayo za Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, za kuanzisha vijiji vya ujamaa na kujitegemea na kwamba, atakwenda mbali zaidi kwa kuanzisha vijiji vya watalaamu.

Baba wa Taifa alianzisha vijiji vya ujamaa na kujitegemea. Tunapaswa kutengeza vijiji vya watalaamu wa madaktari, teknolojia na kilimo. vijiji hivi ni muhimu kuongeza ugunduzi na uvumbuzi.

Suala la vijiji vya ujamaa na kujitegemea vilivyoanzishwa na Mwalimu Nyerere, nabadilisha ili tuwe na muundo mzuri wa urithishanaji taaluma tutalijengea Taifa mustalabali mwema.

Ahadi yangu ni kutoa elimu juu ya kutambua haki na wajibu wao, sababu mtu hawezi kudai haki asiyofahamu na kutekeleza wajibu asiojua.

Hili litaenda sambamba na upatikanaji Katiba ya wananchi, kwa sababu ndani ya Katiba, mkataba wa kijamii unapatikana maana yake tukiwa na Katiba ya hovyo, taifa litakua la hovyo.

Nimeisikia wananchi wengi wakiwa wamekata tamaa, hata wengine wakipata mashaka wataingiaje kwenye uchaguzi huu.


Wapo wanaodhani hautakuwa wa maana na mantiki. Fursa hii ni adhimu, tuache woga tuingie ili tuendelee kudumu katika mustakabali wetu mwema.
 
Kwani kifupi cha Chama cha Majizi si ni CCM? Kwani lazima iwe Chama cha Mapinduzi? Si inaweza kuwa pia Chama cha Masela?
🙌🙌!..leta kuku mweupe jogoo anayewika awe mkubwa*" ! Nikutengenezee zindiko wasione kuwa unawasema ccm!🤭🤭🤭😆😆😆
 
Huyu wakili ni makini zaidi ya Tundu Lissu, apewe nafasi ya kupambana na Magufuli
Mbona unasema ni makini kuliko Tundu Lissu wala sio Mbowe, Nyarandu etc??
Usituchagulie subiri makamanda waamue mgombea, wala usiwe na shaka watachagua mtu makini!!
 
Back
Top Bottom