September 23, 2014
JK awapandisha saba JWTZ
NA MWANDISHI WETU
AMIRI Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo Maofisa saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kutoka cheo cha
Brigedia hadi kuwa
Meja Jenerali.
Hatua hiyo aliitekeleza kwa mujibu wa kanuni za majeshi ya ulinzi ya Tanzania ambazo zinatambulika kisheria.
Maofisa waliopandishwa vyeo ni
Brigedia Jenerali Gaudence Milanzi,
Brigedia Jenerali James Mwakibolwa,
Brigedia Jenerali Ndetaulwa Zakayo na
Brigedia Jenerali Venance Mabeyo.
Wengine ni
Brigedia Jenerali Simon Mumwi,
Brigedia Jenerali Issa Nassor na
Brigedia Jenerali Rogastian Laswai, ambao wamekuwa na vyeo vya
Meja Jenerali kuanzia Septemba 12, mwaka huu.
Katika tafrija ya kuwavisha vyeo vipya maofisa hao, iliyofanyika makao makuu ya jeshi eneo la Upanga, Dar es Salaam, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali Davis Mwamunyange, alimwakilisha Rais Kikwete.
Uteuzi huo pia umempandisha
Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC).
Meja Jenerali Milanzi amechukua nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa aliyekuwa Mkuu wa Chuo hicho,
Luteni Jenerali Charles Makakala