Namba hazidanganyi Ronaldo yupo kwenye anguko kama Rooney

Abu Ubaidah Commando

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
7,591
Reaction score
6,946
img_1248.jpg

Namba Hazidanganyi, Ronaldo yupo kwenye anguko kama Rooney

Zinedine Zidane alizungumza baada ya mchezo vs Las Palmas kwamba alimbadili Cristiano Ronaldo ili kumpumzisha kuelekea mchezo wa kesho vs Dortmund katika usiku wa mabingwa wa ulaya. Ilikuwa wazi ni kauli ya kisingizio, ukizingatia fomu ya CR7 kwa sasa.

Ronaldo anakikimbiza kivuli chake mwenyewe. Kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ndivyo ubora wa Ronaldo unavyopungua na huo ni ukweli usiofichika.

Namba hazidanganyi na kwa upande wa Cristiano – ambaye anapaswa kuangalia takwimu zake mtandaoni kufahamu hali aliyonayo sasa. kuna muda namba 7 zilikuwa hazina wa kulinganishwa nae. Lakini mpaka kufikia sasa ukiangalia namba zake – zinaonyesha udhaifu mno. Amekuwa na mwanzo mbaya kwenye ligi tangu alipojiunga na Real Madrid.

Hakuna aliyedhani wakati akifunga goli lake la kwanza msimu huu katika mchezo vs Osasuna, ndani ya dakika 10, kwamba hayupo kwenye fomu yake. Angalau kwenye suala la ufungaji kwenye La Liga. Hata hivyo, hilo ndio goli pekee alilofunga msimu huu mpaka sasa kufikia mchezo wa sita. Raundi ya 7 imefika na Ronaldo yupo chini kwenye msimamo wa wafungaji wanaowania Pichichi. Hata, Pedro Leon amefunga magoli mengi kumzidi.
Ronaldo yupo katika msimu wake wa 8 Santiago Bernabeu na inabidi turudi miaka 8 nyuma alipokuwa Manchester United kuona namba ndogo kama za sasa. Msimu wa 2007/09, baada ya michezo 6, alikuwa amefunga goli moja tu. Rekodi yake mbaya zaidi katika La Liga ilikuwa msimu wa 2010/11, alifunga magoli 3 katika mechi 6. Tangu wakati huo hajawahi kufunga chini ya magoli matano katik mechi 6 za kwanza.

Msimu wa 2014-15, aliweka rekodi, alifunga magoli 10 katika mechi 6 za kwanza. Neno ‘slow decline’ linaweza kutumika kama CR7 hatoweza kurudisha kiwango, na tunaweza kushuhudia kile kinachomkumba Wayne Rooney hivi sasa Manchester United.
 
Umekazania mechi 6 goli moja huku unasahau kacheza mechi ngapi na yupo kwenye hali gani kiafya
 
HAJACHEZA MECHI 6 BHANA HALAFU SUALA LA KIWANGO LINATOKANA NA MGUU WAKE KUWA PANCHA
Mbona MESSI hayuko fiti 100% ila akipata mpira anawazungusha kama kawa

BADO NAJIULIZA TUZO YA UEFA WALIMPA VIPI MMOROCO

MADRID KWA SASA INABID WAZUIE SAFAR ZA MOROCO labda huenda akarejea tena kufunga penat nyingi la sivyo tutampoteza Penado
 
Umeongea point PNC...The fact that Computer iz injured na ameprove kama kawa without any doubt, na still the best player in the world,

But UEFA OFFICIALS nikweli hadi sasa najiuliza kwa kipi alichofanya hadi apewe tuzo hiyo? Hata ukicheki mafanZ wake wametulia kimya hata kujitokeza tu wanaona aibu, ukweli ni kwamba tuzo hiyo ilikua inamhusu the greatest footballer of all time (KING) mwenyewe...(STUPID UEFA) hawatendi haki.....

Mtu mwenyewe kishajichokea,hana lolote, na imefikia hata kocha [ZIZZOU] kumchoka kabsaa na Kumtoa nje! pumbff kabisa, yani wameniudhi sana,haki haikutendeka pale.....Mungu anajua
 
Vigezo gani messi alimzidi christiano?
 
Usifananishe Ronaldo na vitu vya kijinga kama Rooney
 
Nimeona kwenye page ya Dauda, yule jamaa huwa sioni kama ni mchambuzi wa mpira, mara nyingi anatoa tafsiri ya yale yanayoandikwa na magazeti ya ulaya na wachambuzi wakongwe, ila kiuchambuzi yuko chini sana. Christiano katoka kushinda Champions league, hajapumzika kaenda kushinda Europa, kapata majeraha, hajapumzika cha kutosha karudi kwenye league. Ukitaka kuona uchwara wa Dauda subiri CR7 aanze kutupia mahatrick atakavyoanza kumsifia.
 
ujifunze kutofautisha kitu unachotamani kitokee na uhalisia,kwa hii idadi ya mechi ushatoa hitimisho.Huu si uganga wa kienyeji?!?..
 
Usifananishe Ronaldo na vitu vya kijinga kama Rooney
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kwa rooney ndiyo level yake VP KUHUSU HAZARD
 
Umeongea point PNC...The fact that Computer iz injured na ameprove kama kawa without any doubt, na still the best player in the world,

But UEFA OFFICIALS nikweli hadi sasa najiuliza kwa kipi alichofanya hadi apewe tuzo hiyo? Hata ukicheki mafanZ wake wametulia kimya hata kujitokeza tu wanaona aibu, ukweli ni kwamba tuzo hiyo ilikua inamhusu the greatest footballer of all time (KING) mwenyewe...(STUPID UEFA) hawatendi haki.....

Mtu mwenyewe kishajichokea,hana lolote, na imefikia hata kocha [ZIZZOU] kumchoka kabsaa na Kumtoa nje! pumbff kabisa, yani wameniudhi sana,haki haikutendeka pale.....Mungu anajua
Mbaya zaidi ZIZU anasema MESSI ATABAKI KUWA MESSI[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] yani hapo ndio kapigilia msumari
 
Nimeona kwenye page ya Dauda, yule jamaa huwa sioni kama ni mchambuzi wa mpira, mara nyingi anatoa tafsiri ya yale yanayoandikwa na magazeti ya ulaya na wachambuzi wakongwe, ila kiuchambuzi yuko chini sana. Christiano katoka kushinda Champions league, hajapumzika kaenda kushinda Europa, kapata majeraha, hajapumzika cha kutosha karudi kwenye league. Ukitaka kuona uchwara wa Dauda subiri CR7 aanze kutupia mahatrick atakavyoanza kumsifia.
Ronaldo yupi wa kupiga Hat Trick?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom