Zidovudine 300mg
Member
- Jun 4, 2024
- 13
- 21
Ili kuendana na teknolojia ya dunia na kukimbia kwa kasi tunapaswa kuwa na teknolojia ambayo itaketa vitu vingi Kwa pamoja na kurahisisha huduma katika sehemu moja
Moja ya huduma hizi ni pamoja najua na namba moja ya simu ambayo itatumia mitandao yote, mtu atakuwa na namba moja ya simu itakayotumika katika mitandao Yote, ataweza kufunga akaunti ya mitandao miwili au zaidi kulingana na matumizi na mahitaji yake.
Mitandao ya simu ni akaunti kama ambavyo inakuwa na uwezo wa kutunza pesa, kutunza data na pia kutunza namba za watu vivyo hivyo ina uwezo wa kuwa na namba moja ya simu na kuwa na akaunti ya mtandao husika.
FAIDA ZAKE
Usalama, mtu kuwa na namba moja ambayo imesajiliwa Kwa jina lake itapunguza uharifu wa mitandao Kwa Hali ya juu kulinganisha na sasa mtu anaweza kuwa na namba hata 10 za mitandao tofauti na amesajili Kwa majina tofauti inampa mwanya wakufanya uharifu nakutokujulikana
Tukiweka namba moja ambayo ina uwezo wa kufanya kazi na idadi ya mitandao ya simu ambayo mtu anahitaji kutumia itasaidia kuwanasa waharifu kirahisi mfano uwepo wa namba ya NIDA huwezi kukuta zinafanana hivyo unatumia kitambulisho hicho kimoja sehemu zote na kimekusanya tarifa zako ambazo zitaonekana ni vigumu mtu kufanya uharifu kwa kutumia namba yake ya NIDA kwasababu ni rahisi kujulikana, kuwa na namba moja itasaidia kukujua ukiwa na mtandao X ni wewe na ukiwana na mtandao Y ni wewe.
Itapunguza utapeli kwa kiasi kikubwa na itungwe Sheria ya kuwa na namba moja ambayo itamlazimisha mtu kuwa na namba moja .
Picha ni Kwa hisani ya Milardayo
Picha ya utapeli hapo juu mtuhumiwa alifanikisha utapeli Kwa kutumia namba za mitandao mitatu tofauti imechukua muda kumgundua kama mtu nauwezo WA kumtapeli kiongozi mkubwa sembuse Sisi wananchi WA kawaida
Namba moja mitandao tofauti itasaidia kurahisisha mawasiliano, mfano mtu unaenda sehemu unakosa mtandao wa mtandao X utabadilisha tu akaunti itasoma mtandao Y na utaendelea kutumia huduma vivyo hivyo katika kufanya miamala ya kipesa itaondoa usumbufu.
Kupunguza mzigo wa kuwa na simu nyingi ili kuwa na mitandao tofauti ya mawasiliano kulingana na mahitaji husika ya mteja
Kusajili alama ya vidole na namba ya NIDA haijaondoa tatizo la wizi wa mitandao, Serikali tunaipongeza kwa kuweka utaratibu huu lakini wale waharifu wanaendelea kutumia watu meseji za TUMA KWENYE NAMBA HII bado wanafanikiwa mtu hata kua na uwezo wakua na namba zaidi ya moja hivyo kufanya uharifu kwa namba ya simu itakua vigumu kulinganisha na sasa
Kuondoa tatizo la kuwa na muingiliano wa mawasiliano kwa mitandao
Kuepuka changamoto za kampuni za simu kulazimisha wateja kutumia huduma ambayo hana haja nayo. Mdau kupitia mtandao WA kijamii WA JAMIIFORUMS ametoa malalamiko yake kupitia jukwa la KERO. Unaweza kutatuliwa Kwa kuwa na wigo mpana wamawasiliano ya kubadili tu akaunti nakutumia mtandao mingine.
Picha Kwa hisani ya JAMIIFORUMS
Pia itaongeza kuwa na ushindani wa makampuni ya huduma hizi za mawasiliano kwa kuboresha huduma kwa wateja ili kuendelea kuwamiliki wateja wao na kupata wengine wapya.
Itasaidia serikali kupitia shirika lake la TCRA kujua idadi ya watumiaji wa simu au hata mtandao husika kwa data kamili na kupanga miradi ya maendeleao.
Itasaidia kuimarisha na kusambaza Mkongo wa Taifa wa mawasiliano ili upatikanaji wa mawasiliano uwe Bora na umfikie kila Mtanzania haswa vijijini
CHANGAMOTO ZINAZOWEZA KUJITOKEZA
Ikitokea mtu amepoteza simu au line yake yake anaweza kukosa mawasiliano Kwa muda husika Hadi hapo atakapo irudisha namba yake
Kama simu ikidukuliwa(HACKED)anaweza poteza data nyingi Kwa wakati mmoja
UTEKELEZAJI WAKE
Kampuni za simu na wadau wa mawasiliano wanaweza kushirikiana ilikufikia Tanzania salama ya matumizi ya mtandao WA mawasiliano ya simu
Tunaweza pia kutumia namba ya NIDA ikiwa ndio namba ya simu ya mawasiliano ya mtu ambayo anawezakutumia kwenye mtandao autakao ambapo namba ya NIDA kila Mtanzania anayo yake akawa nafungua akaunti ya mtandao autakao
Kwa watumiaji wa simu Janja Yani (smart phone) mtu anaweza kutumia kirahisi kulingana na ubora wa simu hizi pia uwezo wakua na mpako mbandikao(Application)Kwa watumiaji WA simu za kawaida arimarufu kama kiswaswadu mtu anaweza kutumia Kodi ya mtandao husika na kubadili mtandao kama ambavyo ilivyo sasa katika kuingia kwenye mitandao ya kipesa
UTAFITI
Katika kutafiti kwangu na kuuliza maswali kwa watu bila kuchagua (Randomly sampling) katika jiji la Dar es salami maeneo ya Gongo la Mboto wakazi 148 Kati ya 150 walikubaliana na wazo la namba moja ya simu mitandao tofauti.
Pia maeneo ya feli, Kigamboni wananchi 230 walisema ni wazo zuri iwapo Serikali italifanyia kazi moja ya mwanachi alisema "Kwa ujumla kuwa na nambali moja ya simu mitandao tofauti hutoa unyumbufu, faraga na urahisi na kurahisisha mawasiliano huku ukiendelea kuthubiti njia zako za mawasiliano (wananchi hawa walitoa maoni Kwa mashariti ya kutokuchukuliwa picha wa sauti )
HITIMISHO
Serikali kupitia wizara ya Mawasiliano inapaswa kuendelea kua bunifu katika kuendelea kumrahishia Mtanzania haswa WA Hali ya chini upatikanaji WA uhakika WA mawasiliano Kwa muda wote.

Upvote
2