KERO Namba nyingi za simu za Mashirika ya Umma hazipatikani

KERO Namba nyingi za simu za Mashirika ya Umma hazipatikani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari mimi ni mdau, changamoto yangu kubwa ni kuwa namba nyingi za simu za mashirika ya umma hazipatikani na zingine ukipiga zinakuwa hazipo...

Pamoja na changamoto hiyo, bado mashirika wanaziweka hizo namba kwenye anuani za mashirika hayo jambo linaloleta mkanganyiko sana hasa ukiwa unahitaji kuwapigia ili kupata huduma zao... na mara nyingi mashirika hayo yanatumia namba za zamani sana na bado hawazibadilishi ili kuendana uhitaji wa sasa.

Nashauri viongozi wa mashirika ya umma kukaa na kutafakari hili suala. Waachane kabisa kutumia namba za miaka ya zamani ambazo hazipatikani.. waweke zinazopatikana na huduma kwa wateja ziboreshwe ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na kuondoa usumbufu kwa raia.
 
Nyingi zimesajiliwa kwa line ya TTCL na Wenyewe TTCL hawana la kusema kwa huduma mbovu.
TTCL ni jipu kama nyaya walizosambaza hifadhi za mlima Kilimanjaro kwa ajili ya Wi-fi ambayo haifanyi kazi muda mwingi ni kuihujumu kampuni
 
Nyingi zimesajiliwa kwa line ya TTCL na Wenyewe TTCL hawana la kusema kwa huduma mbovu.
Hata simu za mkononi pia hazipatikani, nadhani zimekabidhiwa watu wenye majukumu mengi. Nashauri wangekabidhiwa ma-PS au waajiriwe watu maalumu wa kupokea simu!
 
Hata simu za mkononi pia hazipatikani, nadhani zimekabidhiwa watu wenye majukumu mengi. Nashauri wangekabidhiwa ma-PS au waajiriwe watu maalumu wa kupokea simu!
namba za TTCL au kampuni nyingine?
 
kimsingi suala la Costomer care Bongo ni sufuri bin sifuri hamna wanaopokea kwakua hawana cha kujibu na wengine wameweka manamba Bosheni ili waionekane wana hudumia wateja , kuna jamaa wanaitwa RITA wakipokea mniite mbwa niko pale
 
Naona hata bill za simu wanaiba
Yaani hata uki Google kuuliza chochote ni kazi bure
Vitu vya muhimu wao hawaviongelei kabisa
 
Vitu vya muhimu Tanzania havipewi kipaumbele, watafute kila campuni customer care ambae atadili na changamoto husika kwa kila campuni na tasisi.
 
Back
Top Bottom