Nambari 3 in Siri gani wakuu

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
8,611
Reaction score
16,118
Wakuu naomba kujuzwa Siri iliyopo nyuma ya nambari 3 maana hi nambari hutumika Sana katika Mambo mbali mbali.Kwa mfano;

1.Huwa tunakula Mila 3 kwa siku

2.Mchezaji wa soka akifunga mabao 3 hio inaitwa hat- trick na anazawadiwa mpira.

3.vijijini nyumba nyingi zina vyumba 3.

4.Wagonjwa hushauriwa kumeza dawa Mara 3 kwa siku

5.Ukimdai mtu Deni lako atakwambia usubiri kdgo atakulipa baada ya siku 3.

6.Kuku huangua vifaranga baada ya wiki 3( 21 days)

7.Babu yangu Ana wake 3[emoji23][emoji23][emoji23]

8.Mimi mwenyewe Nina ndugu 3
 
mmmmh! bado mifano yako haina mashiko! kuna mtu alishawahi kuuliza swali hilo ila yeye aliweka hoja za msingi sana na akapata majibu ya kutosha ila wewe na hizo hoja zako sina hakika kama utapata majibu
(1) babu yako ana wake 3
(2) wewe una ndugu
(3) vijijini nyumba zinajengwa vyumba 3
kwa hoja hizo sidhani kama utapata majibu ila subir wajuvi wa mambo waje
 
Sidhani kama utapata mawazo ya maana kwa jinsi ulivyowasilisha sredi yako
Hasa mwishoni
 
tunataka ushuhuda wa huo 3 sio maelezo maelezo
 
HAYO MASUALA YA MILO MITATU NI UMASIKINI TU, UNAPASWA KULA MARA TU PALE UNAPOHISI NJAA, SO UKIHISI NJAA SAA 10 JIONI UTASUBIRI HADI USIKU NDO ULE???
 
Basi namimi ningependa kujua kuhusu namba 10. Mama yangu kazaliwa tarehe 10, mimi na ndugu zangu watano tumezaliwa tarehe hiyo hiyo pia🤔
 
3.vijijini nyumba nyingi zina vyumba 3.
___________________________________

Huku kwetu nyingi ni chumba 1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…