Namdai mtu, tumeandikishana 'Locally'

Lady Ra

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
879
Reaction score
991
Wakuu,

Kuna mtu nilimkopesha Pesa kiasi, na tuliandikishana "locally" sababu kipindi hicho alikua ni hawara/boyfriend wa Mama yangu Mdogo.

Hatukwenda kwa Mwanasheria yeyote na alinipa hati yake ya Nyumba nimshikie kama kidhibiti.

Sasa ananizungusha mwaka wa pili huu, naweza kuyatumia hayo maandikishiano kumshitaki? Na kesi za aina hua zinaanziaga wapi?

Na hii ikithibitika kua sahihi ni yake hua zinaishiaga vipi?

Naweza kuomba mahakama hiyo Nyumba iuzwe nilipwe changu?
 
Ndugu yangu hii ni kesi ya madai na huwa inaanzia mahakaman na kwisha huko huko mahakaman.
unaweza ukaitumia hiyo hati pamoja na maelezo mliyoandikishana locally kama ushahidi wako. kwa kuanzia inabidi umwandikie barua huyo jamaa (demanding letter) ikimkumbusha kuwa unamdai kiasi fulan hivyo awe amekulipa ifikapo tarehe fulan, akishindwa kukulipa kufikia tarehe hiyo mueleze kuwa utamfikisha mahakaman. asipolipa, nenda na hiyo copy ya barua mahakan kafungue kesi ya madai.
endapo utashinda kesi, mahakama itamuamuru huyo jamaa kukulipa ndan ya muda fulan na kwa namna ipi. akishindwa kulipa hapo hatua ya attachment inaweza kufuata, ambapo mali yake yanayoweza kukulipa yanaweza kuamuliwa kuuzwa na ukapewa pesa yako au hata kuchukua ww mali hiyo kama thaman zitaendana.
kama hana kitu chochote cha kukufidia ww, anaweza kufungwa lkn anakuwa civil prisoner ambapo akiwa gerezan ww utamhudumia kwa chakula, matibabu jambo ambalo litakugharim ww tena.
kias unachomdai ndicho kitachozingatiwa kes ufungulie mahakama ipi.
 

Ahsante kwa Kuniona,
Na hiyo barua kuna kumsainisha kama kapokea?

Nikimpa tu barua kisha akaja kubisha mbeleni kama sikumpa?

Na lazima nitumie wakili kwenye kufungua kesi?

Pia kama amount nayomdai ndio itachagua mahakama ya kusikiliza kesi, Mimi kwa kuanza naanzia mahakama ipi?
 

1. Tabia ya kuandikishiana locally acha.
2.alikupa hati ya nyumba "umshikie"???? Kwa maana ilikuwa mzigo kwake ama?
3.unaweza kumshtaki ila swali la wapi siwezi kujibu maana sijui mmekopeshana bei gani
4.kwani kunaubishano katika sahihi? Mbona unaifanya "sahihi" kuwa jambo sana? Amepinga kwamba hakusaini? Au unamaanisha ikithibitika alikukopa? Kama ikithibitika alikopa ni lazima alipe
5.ndiyo unaweza omba nyumba iuzwe ili kulipa deni na kama bado "umemshikia" hyo hati itakupa urahisi zaidi kwenye kuuza.

N.B kama ulimkopesha kwa riba nafasi yako kushinda ni finyu
 
Barua (demanding letter) utampatia kukiwa na mashahidi. mfano: unaweza kuiandika barua yako na kugongesha muhuri kwa kiongoz yeyote wa serikali ya mtaa. kisha unaweza kwenda na mjumbe wa nyumba kumi mpaka kwa mdaiwa akampa hiyo barua, hapo unaondosha mazingira ya kukataa kuwa hakupewa,origional unampa copy unabak nayo.
Siyo lazima kumtumia wakili. ww mwenyewe unaweza kuiendesha kesi hiyo, ila kama pesa ni nyingi na unapenda kumtumia wakili unaweza kufanya hivyo.
kuhusu kias cha pesa kita-determine ufungulie mahakama gani ni kwamba:
ili ufungulie mahakama ya mwanzo thamani ya unachodai isizid milion 10 kwa movable property au mil 12 kwa immovable property. mahakama ya wilaya/mkazi kuanzia hizo za mahakama ya mwanzo hadi mil 100 kwa movable na 150 immovable. zaidi ya thamani hizo kesi utafungulia mahakama kuu.
 
cheza na sheria mkuu. Angalia usikose vyote anaweza kukugeuka na kuwahi mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…