Namibia yafunga huduma za Shirika lake la ndege, wafanyakazi 600 kukosa ajira

Namibia yafunga huduma za Shirika lake la ndege, wafanyakazi 600 kukosa ajira

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Shirika la Ndege la Namibia, Air Namibia limetangaza kusitisha shughuli zote za usafirishaji na kurudisha ndege zote zilizokuwa zikifanya safari, ikiwataka abiria wote waliokuwa wamekata tiketi kuomba kurudishiwa fedha zao.

Bunge la Namibia limetoa kibali cha kufunga shirika hilo, huku zaidi ya wafanyakazi 600 wakitarajiwa kupoteza ajira zao. Hata hivyo, wafanyakazi hao watapata stahiki zao za mishahara kwa miezi 12 ijayo.

Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa serikali ya Namibia imesema kwamba imeangalia njia zote za kulihudumia shirika hilo ikiwamo kutafuta uwekezaji kutoka kwa mashirika mengine ya ndege kabla ya kufikia maamuzi ya kulifunga shirika hilo. Inakadiriwa kuwa serikali ya Namibia imetumia zaidi ya dola bilioni 8 za Namibia (sawa na zaidi ya Tsh. bilioni 340) kugharamia shirika hilo, na sasa imekiri kuwa hali ya uchumi wa nchi hairuhusu kuendelea kutoa fedha zaidi kwa shirika hilo.

Shirika hilo lina jumla ya ndege 9, lakini ndege nyingi zilikwisha acha kufanya safari zake ndani ya kipindi cha mwaka 2020. Ingawa ndege zake nyingi zilifanya safari katika ukanda wa Kusini mwa Afrika, ndege za Airbus A330 zilifanya safari zake kati ya Windhoek na Frankfurt nchini Ujerumani.

Shirika hilo lililoanzishwa miaka 74 iliyopita lilianza kutumia ndege kubwa za abiria mwaka 1989, likitumia ndege ya kuazima kutoka Shirika la Ndege la Afrika Kusini, aina ya Boeing 737-200. Hadi wakati wa kufungwa kwake, Shirika hilo lilikuwa na ndege za kuazima aina ya Boeing 747 kutoka Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
 
ATCL inaficha ripoti yake ya ukaguzi wa mahesabu kudadeki.....shirika linaendeshwa kwa makusanyo ya kodi na sio mtaji wa biashara
Na saivi limeamishiwa kwenye mfuko wa raisi hakuna mwenye mamlaka yakulichunguza kukagua wala kutoa ripot yoyote ya mahesabu
 
Wenye akili hao! B8 za Namibia ni sawa na B340 za Bongo? Hatareeeeee
Windhoek ni kati ya products za Namibia zilizotapakaa katika soko la Tanzania na inapendwa kuliko equivalent local products. Wako makini kwenye suala zima la demokrasia, haki za binadamu, utawala bora, Katiba na sheria. Serikali yao ni inclusive; hakuna wao na sisi. Lazima dola yao iwe juu.

Juzi kati tuliletewa uzi humu; miundombinu ya barabara Namibia ni kati ya miundombinu bora kabisa Afrika na duniani. Inaonesha ni taifa linalotumia akili. Namibia pengine ni nchi inayoongoza Afrika ambako wasomi wa Tanzania wanakimbilia kutafuta kazi zenye maslahi bora.
 
Screenshot_2021-02-13 Drone Photos Capture the Stark Divide Between Rich and Poor in South Afr...png

Hii ndiyo demokrasia unayoisifia? Wanawatenga na kuwanyanyasa masikini?
 
Back
Top Bottom