Namibia yakitupalia mbali Kiswahili na kuchagua Lugha ya Kichina

Namibia yakitupalia mbali Kiswahili na kuchagua Lugha ya Kichina

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Mnamo mwaka 2019, Marehemu Rais Magufuli na na Rais wa Namibia, Geingob walikubaliana kuanzisha lugha ya Kiswahili katika shule za Namibia.

Mwezi huu, Wizara ya Elimu nchini Namibia ilitangaza kuwa Kiswahili hakitatolewa nchini Namibia na kufichua kuwa shule za Namibia zinapendelea lugha ya kichina inayojulikana kama 'Mandarin' kama mbadala wake.

1730738378971.jpg

Idadi ya Wachina nchini Namibia imeongezeka sana tangu uhuru.

Hivi majuzi mnamo mwaka 1998, Redio ya Kimataifa ya China iliripoti kuwa kulikuwa na Wachina 50 pekee wanaofanya biashara nchini Namibia, lakini kufikia 2005 idadi hiyo ilikuwa imeongezeka na kufikia zaidi ya 1,000. Ukadiriaji wa idadi ya wachina nchini Namibia kupitia Ubalozi wa Marekani wa 2009 uliootolewa na ofisi za kidiplomasia za Marekani uligundua kuna wachina waishio Namibia zaidi ya 3,000 au 4,000.

Wanasiasa wa upinzaji kama vile Jurie Viljoen wa Kikundi cha Monitor Action alitoa mashtaka kwamba utoaji vibali vya kazi kiholela umesababisha kuongezeka kwa wafanyakazi 40,000 wa kichina.

Wahamiaji wengi wa Kichina huanzisha biashara ndogo ndogo za rejareja hasa katika sekta ya nguo na vito. Kuwasili kwa wafanyabiashara kutoka china kumeleta malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani kuhusu ushindani wa kibiashara na wasiwasi kuhusu ubora na usalama.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa Namibia walikubali hali ya kuongezeka kwa Wachina katika sekta ya biashara za reja reja wakitaja manufaa ya kutengeneza ongezeko la ajira na kupunguza gharama za bidhaa.

Miaka ya 2000, biashara kati ya Uchina na Namibia ilikua kwa kasi, na kupanda kutoka dola milioni 75 mwaka wa 2003 hadi dola milioni 600 mwaka wa 2009. China City, kituo cha jumla na rejareja kilicho katika eneo la viwanda la kaskazini mwa mji mkuu 'Windhoek' takriban dakika 20 kutoka katikati mwa jiji hili, lilifunguliwa mwaka wa 1998 na Li Chengyuan (李澄原), mfanyabiashara kutoka Taiwan; kufikia mwaka wa 2005,

Wafanyabiashara walikuwa wakiagiza takriban makontena 1,000 ya bidhaa kwa mwaka kutoka China.
Eneo la Oshikango, mpakani na nchi ya Angola imekuwa kivutio maarufu kwa wafanyabiashara wa China wanaotarajia kunufaika na kupanua biashara ya mipakani. Kufikia 2004, mji ulikuwa na maduka 22 yanayomilikiwa na Wachina, na kupanuka hadi maduka 75 kufikia 2006.

Kutoka kuuza viatu na nguo, maduka haya yamepanua matoleo yao ya bidhaa na kujumuisha furniture, vifaa vya kielektroniki vya nyumbani, pikipiki, maua bandia na aina nyingine mbalimbali za bidhaa. Wamiliki wa maduka haya huingiza bidhaa zao kupitia bandari za Walvis Bay au Durban nchini Afrika Kusini, na kuzileta kwa reli ili zihifadhiwe katika ghala za dhamana, ambapo zinauzwa kwa wafanyabiashara wa Angola na kuuzwa Angola kwa kiasi kidogo, hivyo basi kuepuka kutoa ushuru wa forodha kwenda Angola.

Katika baadhi ya matukio ya kushangaza, wafanyabiashara hawa kutoka China wameanzisha na kufungua viwanda feki huko Oshikango ambavyo havizalishi bidhaa za ushindani wa kweli; kazi kuu ya viwanda hii ni kupata vibali vya kazi kwa Wachina kutoka nje ambao wanaweza kuja na kufanya kazi kama wasaidizi wa duka katika biashara za kuagiza bidhaa kuja Nambia na zingine kusafirisha nje ya nchi (Import/Export Businesses).

Kwa Afrika, Nchi inayoongoza kwa idadi kubwa ya Wachina ni Afrika kusini. Nchi nyinginezo ni kama Nigeria, Angola, Kenya, Zambia.

CHANZO: Namibian Schools Favor Mandarin Over Kiswahili
Screenshot_20241104-194441_1.jpg

Soma: Kiswahili Chapingwa kufundishwa mashuleni Namibia
 
Kiswahili kitakufa kwasababu hakina hadhi ya kitaaluma wala kiuchumi
 
Wameona lugha yenye fursa za kibiashara Kwa baadae ni china maana wachina Wanazalisha bidhaa nyingi sana.Watanzania tunajinyima fursa Kwa kung'ang'ania kiswahili ambacho hakina tija yeyote duniani sababu inamilikiwa na wategemezi yaani masikini
 
Kwa hiyo tukumbatie kizungu
Mkuu Ile mada yakuhusu waafrika na waarabu kuwa waharibifu hapa inahusika,,,mwafrika ana akili ya kitumwa..Nimeona pia hao wanamibia wapumbaf wamehalalisha ndoa za jinsia moja......Kingine hawa wachina Wana ajenda ya Siri,,,na hawa Viongozi wetu dhaifu hawajali kinachoendelea,.......Hapa dar ukienda kisemvule wachina wamezalisha Sana dada zetu... unaweza kaa mahali ukaona mpaka wanawake 20 wanapita na vitoto vya kichina tu......Viwanda vyao vya kinafki walivyojenga kuanzia mwanambaya kwenda njia ya mtwara ni chambo kwa dada zetu......sidhani kama sisi watatuvumilia tungekuwa huko kwao kama wawekezaji afu tuwatie mimba watoto wao kiasi kile.
 
Hao wamekimbilia fursa zinazopatika a katika lugha ya Kichina. Tatizo la kiswahili Dola inayomiliki Ni nchi maskini .hivyo wazungumzaji wa kiswahili Ni maskini mtu akitaka kujifunza Kiswahili lazima ajiulize nitapata fursa gani? Yani MTU analazimika kujifunza lugha au ku adapt utamaduni wa kingeni kutokana nautajiri wa nchi miliki wa lugha husika. Tanzania ingekuwa nchi tajiri kiswahili kingekuwa lugha lugha ya Africa. "Hakuna lugha ya maskini inayopendwa na kuenea" hata hiki kiswahili unachoona kinazungumzwq na watu Milion 200 nikwasababu kilienezwa na Wakoloni ambao walikuwa na nguvu kiuchumi. Kiswahili kilienea zamani sio Sasa. Kwa Sasa nikwasababu za kiakademia tu. Lugha Ni uchumi
 
Kweli masiki hana rafiki unafukuzwa kila sehemu..
Acheni tupambane kwa jasho na damu hadi kieleweke..
 
Back
Top Bottom