Namkumbuka sana SHANGAZI yangu (Alinifukuza NYUMBANI akanifunza MAISHA)....

Namkumbuka sana SHANGAZI yangu (Alinifukuza NYUMBANI akanifunza MAISHA)....

Liverpool_Jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
1,220
Reaction score
1,415
Nimeona POST ya jamaa mmoja akilalamika kuwa WAZAZI WAKE WALIMFUKUZA NYUMBANI.

Daaahh..!!! KANIKUMBUSHA sana SHANGAZI YANGU...

Ngoja nimpe TESTIMONY yangu kidogo......

Kifupi mi ni YATIMA tokea mdogo sana.
Then nimelelewa na ndugu wengii ila wa mwisho alikua ni SHANGAZI.

Niliondoka home (kwa SHANGAZI) advance level (form 5) baada ya kuona maisha ya kwa ndugu siyaelewi nikaenda kuishi gheto..

Nilikua nasoma government halafu hata HAWAFUNDISHII

Nikaanza kuuza biashara ndogondogo K.koo usiku (nikitoka darasani) ili kukidhi maisha yangu, hizi biashara nilizianza nilivyomaliza Form 4...

NILISAHAU KABISA KUSOMA.

Form 6 mock nikapata Division 0 (PCB all F)

Matokeo yangu yalivyofika home SHANGAZI aliniambia ""Nilikua najua nini unafanya na nimekua Sanaa mteja wako, ila SIJAPENDA MATOKEO YAKO, Naomba soma, tafuta hata S mbili nijue pakuanzia""

NILIKAMUA BALAA na WATOTO wa MCHIKICHINI TUTION CENTER.

Nikaingia NECTA matokeo yalivyotoka nikapata Division 4.18 (Physics = E, Chemistry = F, Biology = S)

Shangazi akaniashauri nikachukue form kwenye chuo cha afya kuanza kusomea CLINICAL OFFICER...

NIKAGOMA na kumjibu ""MI SIWEZI KUSOMEA UDAKTARI KWASABABU SIJAWAHI MUONA DAKTARI TAJIRI""

Hili jibu nilimuuma sana akanijibu "USIRUDI NYUMBANI BILA DIPLOMA na TOKA KWANGU""

Dah nilikomaa na biashara ndogondogo na kusomea DIPLOMA ya masomo ya biashara...

Nilirudi home kumuomba msamaha nikiwa na BACHELOR...

Shangazi alinijibu ""HUJAWAHI KUNIKOSEA"".
Na akanipa Fedha ya kwenda kufanya REGISTRATION kusoma MASTERS.

Hata sijui alijuaje kama nimefanya APPLICATION.

Huyu MAMA namkumbuka sanaa..
Kwa kunifukuza HOME ALINIFUNDISHA SANAAA MAISHA.

BILA KUNIFUKUZA SIJUI NINGEKUWA WAPI.

NAKUPENDA SANAA SHANGAZI YANGU.
ULINIPA UPENDO WOTEE WA WAZAZI.

Nasikiaga tu "SHANGAZI WANATESA YATIMA" ila wewe ni "Mungu WANGU DUNIA HII

Kijana wa kiume komaa UNAKAAJE HOME na huku shule ushamaliza?

#ASANTE.

#YNWA.
 
Mkuu wewe mshukuru Mungu,sio kila shangazi ana roho nzuri , wengine Ni wakatili Sana wako radhi kudhulumu yatima Mali zilizoachwa na wazazi wao

So Sad[emoji17]
 
Mkuu najaribu vuta picha purukushani za kukutoa hapo nyumbani nahisi kila chombo kilipiga kelele [emoji23][emoji23][emoji23]. Ila mkuu vipi umesoma Benjamini au??
 
Pongezi zimfikie shangazi popote alipo.

Ila Kuna mashangazi wagwadu kinoma
 
Ukisema SANAA unamaanisha nini
1. Nilifaulu vizuri O'Level ila nikaja kuichukia shule Advance.
Alinirudisha kwenye mstari wa kupenda shule mpaka sasa Nina Masters..
BILA YEYE NADHANI FORM FOUR NDIO ILIKUA MWISHO WANGU.

2. Alinifukuza home ila kumbe alikua anatuma mabraza kuja kunicheki maana nilipanga mchikichini mtaa full bangi.
ALIOGOPA NAWEZA KUWA TEJA.

3. Alikua mteja wangu wa biashara ndogondogo..
BILA MI KUJUA.

4. Alisimama kama Baba + Mama yangu.

5. N.k

Kifupi alinifundisha vingii kwenye maisha kwa vitendo na maneno zaidi ya kujitegemea.
 
Na mimi nilitaka nimuulize
1. Nilifaulu vizuri O'Level ila nikaja kuichukia shule Advance.
Alinirudisha kwenye mstari wa kupenda shule mpaka sasa Nina Masters..
BILA YEYE NADHANI FORM FOUR NDIO ILIKUA MWISHO WANGU.

2. Alinifukuza home ila kumbe alikua anatuma mabraza kuja kunicheki maana nilipanga mchikichini mtaa full bangi.
ALIOGOPA NAWEZA KUWA TEJA.

3. Alikua mteja wangu wa biashara ndogondogo..
BILA MI KUJUA.

4. Alisimama kama Baba + Mama yangu.

5. N.k

Kifupi alinifundisha vingii kwenye maisha kwa vitendo na maneno zaidi ya kujitegemea.
 
Mkuu najaribu vuta picha purukushani za kukutoa hapo nyumbani nahisi kila chombo kilipiga kelele [emoji23][emoji23][emoji23]. Ila mkuu vipi umesoma Benjamini au??
Yap BWMHS ile shule ilikua HAIFUNDISHI KABISAA..

Miezi miwili hamjamuona mwalimu wa Physics.

Vile nilitoka home nikiwa na sufuria mbili + godoro la 30,000/= + Jiko la mafuta.

Ule UJASIRI ulinifundishaga "NOTHING IS IMPOSSIBLE, JUST TAKE ACTION""
 
Vijana wa Benja nawaaminia
 
1. Nilifaulu vizuri O'Level ila nikaja kuichukia shule Advance.
Alinirudisha kwenye mstari wa kupenda shule mpaka sasa Nina Masters..
BILA YEYE NADHANI FORM FOUR NDIO ILIKUA MWISHO WANGU.

2. Alinifukuza home ila kumbe alikua anatuma mabraza kuja kunicheki maana nilipanga mchikichini mtaa full bangi.
ALIOGOPA NAWEZA KUWA TEJA.

3. Alikua mteja wangu wa biashara ndogondogo..
BILA MI KUJUA.

4. Alisimama kama Baba + Mama yangu.

5. N.k

Kifupi alinifundisha vingii kwenye maisha kwa vitendo na maneno zaidi ya kujitegemea.
Hayo maisha uliyopitia ni UTAJIRI tosha
 
Back
Top Bottom