Namna ambazo sauti za watu wa vijijini nchini China zinaweza kusikika

Namna ambazo sauti za watu wa vijijini nchini China zinaweza kusikika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1720422458003.png


Simulizi za haki za binadamu nchini China zinaanza kujitokeza katika zama mpya ya mageuzi ya kina na mabadiliko ya kihistoria. Ni hatua kubwa katika juhudi za China za kuondokana na umasikini na mchakato mzima wa demokrasia kwa raia wake, mageuzi makubwa katika sekta za mahakama, bima ya afya na sekta nyingine muhimu zinazohusiana na uchumi wa taifa na maisha ya watu, na pia mjumuiko wa simulizi za watu mbalimbali.

Kwa muda mrefu, baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vya nchi chache wamekuwa wakiitupia lawama na kuishutumu China, hali iliyosababisha kukosa uelewa kwa watu wa nchi za nje kuhusu nadharia na mafanikio ya maendeleo ya haki za binadamu nchini China. Lakini kile kinachojitokeza katika maisha ya kila siku ya Wachina kinaelezea ukweli ulio wazi: Haki ya kuishi na maendeleo ni msingi wa haki za binadamu.

Kijiji cha Xiaogucheng kiko pembezoni mwa mji mkuu wa mkoa wa Zhejinag, Hangzhou. Kijiji hiki sio tu kwamba ni mfano wa kitaifa wa kijiji cha demokrasia na utawala wa sheria, lakini pia kimepewa heshima kubwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemi kuwa kijiji cha kitaifa cha kiikolojia na pia kijiji cha ustaarabu wa kitaifa. Katika sehemu ya kuingia kwenye kijiji hiki, kuna bango kubwa lenye maandishi ya Kichina yanayosema, “watu wanaweza kujadili masuala yao wenyewe.” Kama kijiji cha mfano cha hatua za vitendo vya demokrasia pana, halisi na ya ufanisi katika ngazi ya mashina, mwenyekiti wa Chama katika kijiji hicho, Lin Guorong anaweka wazi kuwa siri kubwa nyuma ya mafanikio hayo ni mwongozo wa kanuni ya ‘masuala ya kijiji yanajadiliwa na wote.’

Wakizungumzia mabadiliko ya kijiji cha Xiaogucheng katika miaka 20 iliyopita, wakazi wa kijiji hicho wanashukuru sana huduma na mwongozo uliotolewa na Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Xi Jinping, kwa kijiji hicho.

Januari mwaka 2005, Xi, wakati huo akiwa katibu wa kamati ya CPC mkoa wa Zhejiang, alitembelea kijiji cha Xiaogucheng. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina na kuelewa vizuri hali ya kijiji hicho, Xi alitoa pendekezo la kuimarisha ujenzi wa demokrasia na utawala wa sheria katika ngazi ya mashina, na kwamba masuala yanayohusu kijiji yajadiliwe na wote.

Mfumo wa majadiliano ya kidemokrasia unaotumika katika kijiji cha Xiaogucheng una thamani kubwa ya mfano wa ujenzi wa demokrasia na utawala wa sheria, na pia masikilizano ya muda mrefu na utulivu katika ngazi ya mashina. Ni kwa kupitia utegemezi usioyumba wa majadiliano ya kidemokrasia ya watu kujadili masuala yao wenyewe ndivyo kijiji hicho kimeweza kuendeleza ujenzi wa sehemu nzuri ya kuishi na kudumisha moyo wa ujasiri wa kijamii, na mpaka sasa, kijiji hicho hakijapokea malalamiko ya aina yoyote.

Katika kituo cha huduma za Chama kijijini hapo, kuna skrini kubwa ya kielektroniki yenye maneno yanayosema ‘ukumbi wa majadiliano wa umma.’ Lin anasema, kwa sasa watu wanaweza kushiriki katika majadiliano ya kidemokrasia kwa kufungua APP ama program ndogo katika simu zao za kisasa, na hata watalii wanaokwenda kijijini hapo wanaweza kushiriki katika majadiliano kupitia jukwaa hilo la mtandaoni.

Ukumbi wa majadiliano wa Umma ni jukwaa la kwanza la majadiliano na mashauriano katika ngazi ya wilaya mkoani Zhejiang. Jukwaa hili la mtandaoni, linatumika kama jukwaa la mashauriano ya kisiasa, taarifa za mrejesho kuhusu masuala ya jamii, na usimamizi wa kidemokrasia, linaondoa vizuizi vya mifumo ya majadiliano ya asili. Pia linawawezesha wanakijiji kushiriki katika majadiliano ya kidemokrasia muda wowote na mahali popote.

Kutoka majadiliano chini ya mti mkubwa wa kafuri mpaka kwenye ukumbi wa majadiliano wa umma katika mtandao, kijiji cha Xiaogucheng kimeshikilia kanuni ya ‘watu wanaweza kujadili masuala yao wenyewe.’ Kijiji hiki kinaendelea kuboresha maendeleo ya kila mmoja kufahamu mfumo wa uongozi, kila mmoja kushiriki katika mchakato wa usimamizi, na kila mmoja kufaidika na matunda ya maendeleo, na hivyo kuimarisha zaidi msingi wa masikilizano na uongozi mzuri kwa ajili ya ustawi wa pamoja katika maeneo yote ya vijijini.
 
Back
Top Bottom