Namna bora kudumisha afya ya ubongo wako

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


KWA UFUPI

  • Kuepuka hasira
  • Kupata usingizi wa kutosha
  • Kupata muda wa kutafakari mambo yako katika mazingira ya utulivu
  • Kufanya mambo kwa mpangilio

Wiki iliyopita niliahidi nitaendelea kujibu maswali ya wasomaji waliotaka kujua namna ya kuwezesha ubongo kuweka kumbukumbu na mazingira mazuri ya kuufanya utende kazi vizuri.

Tuliona namna tafiti mbalimbali tulizozipata kupitia msaada wa vitabu na mitandao zilivyobaini njia mbalimbali za kumsaidia mtu kujifunza na kuwezesha asisahau.
Kutokana na hali hiyo, tafiti mbalimbali zinapendekeza mambo kadhaa ya kufanya ili mtu asisahau.

Leo nitajikita zaidi katika kuelezea kuhusu afya ya ubongo. Watafiti mbalimbali waliozungumzia afya ya ubongo wamegusia mambo mbalimbali ambayo ni muhimu mtu kuyafanya ili ufanye kazi vizuri.

Miongoni mwa mambo hayo ni mazoezi, kujifunza mambo mapya, kubadilishana mawazo na wenzako hasa nyakati za jioni na kuepuka mambo yanayosababisha msongo wa mawazo.
Wanashauri uzoeshe ubongo wako kufikiri mambo chanya kuliko hasi. Mfano kuwa na hisia ya mambo mabaya wakati huna uthibitisho wa moja kwa moja katika yale unayofikiri.

Yanayozungumziwa hapa zaidi ni masuala ya uhusiano mfano mtu anaweza kufikiri hasi dhidi ya mwenzake kwamba ana malengo mabaya juu yake au anamtendea kinyume, wakati hana uhakika na yale anayowaza.

Hapa watafiti wanashauri mtu kuepuka hasira au mambo yatakayomfanya awe na hasira mara kwa mara.

Mapendekezo mengine ni kupata usingizi wa kutosha, kupata muda wa kutafakari mambo yako katika mazingira ya utulivu na kufanya mambo kwa mpangilio.

Mfano asubuhi pangilia mambo utakayoyafanya siku nzima na chunguza kama kuna mpangilio wa miadi au mambo uliyokwishayapanga siku za nyuma kuifanya katika tarehe hiyo.

Kuwa na tabia ya kujitathmini iwapo umefanikisha yote uliyojipangia siku hiyo na kama kuna makosa, jisahihishe ili usirudie katika mipango yako ya baadaye.

Kuhusu chakula inashauriwa kuwa na mazoea ya kula vyakula vyenye mafuta yatokanayo na samaki, nazi na mbegu. Vilevile matunda ni muhimu.

Wataalamu wa ubongo wanasema kumbukumbu zinaweza kuhifadhiwa sehemu mbalimbali za ubongo, lakini sehemu muhimu zaidi ni ile inayojulikana kama hippocampus.

Hii ni baada ya uchunguzi uliofanyika kuonekana kuwa hippocampus ikiathirika kwa namna yoyote ile kwa mfano kwa kiharusi mtu huyo hupoteza kumbukumbu na inakuwa vigumu kujifunza kitu kipya.
Kwa hivyo, wanasayansi wanasema hippocampus huweka kumbukumbu ya kudumu wakati sehemu nyingine huwa ni kwa muda mfupi tu, jambo hilo laweza kusahaulika. Ugonjwa wa kusahau
Utafiti wa karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha California nchini Marekani ulionyesha kuwa ugonjwa wa kusahau maarufu kwa jina la kitaalamau la Alzheimer ni tatizo kubwa miongoni mwa jamii.

Lakini wakaonya kuwa ili kuepukana na mazingira ya kuchochea ugonjwa huo, mtu hana budi kuepuka uzito kupita kiasi, uvutaji wa sigara na ugonjwa wa sukari.

Baadhi ya vyakula ambavyo vina viinilishe muhimu kwa ubongo ni mayai, maziwa, mboga za majani ambazo kupikwa kwake hazikuiva sana na matunda ni apple, parachichi na ndizi.

Moja ya tabia zinazopendekezwa mtu awe nazo ni kula mlo wenye vyakula vya aina mbalimbali, epuka kushiba sana, usizoee kula au kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi.

Fanya usafi wa kinywa mara kwa mara kuzuia magonjwa ya meno na fizi mbayo ni rahisi kuathiri ubongo na hakikisha uzito unawiana na urefu. Wataalamu wa afya wanaweza kukushauri vizuri juu ya uzito Namna bora kudumisha afya ya ubongo wako - Makala - mwananchi.co.tz





 
sasa wale wavutaji wa ile kitu ambayo inataka iruhusiwe nao inakuwaje?
 
na hii misongo ya mawazo (stress) na mi fustration alzheimer ni ngumu kuikosa japo sio kiwango hicho
 

MziziMkavu,
Nasema asante kwa hii topic. Sasa naomba nisaidie kwa Mgonjwa mwenye Brain infection anapaswa kufanya haya haya au yeye afanye vipi? Maana yeye tayari keshadhuru ubongo wake kiasi fulani. Nisaidie kaka
 
Ahsante mkuu MziziMkavu, niliwahi sikia Almond ni nzuri kwa ubongo pana ukweli au ni mambo ya biashara?

Ubarikiwe
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…