SoC04 Namna bora ya kuboresha mfumo wa elimu Tanzania

SoC04 Namna bora ya kuboresha mfumo wa elimu Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Economist Luganda

New Member
Joined
May 26, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Kwanza nipende kuwapongeza serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Elimu Zanzibar, wizara ya Elimu Tanzania na Taasisi zake zote za Elimu katika kuendelea kuboresha mifumo ya Elimu.Pia niwapongeze sana Jopo la Jamii forum kwa kubuni shindano hili la story of changes Mungu awabariki sana mzidi kubuni Mambo mazuri zaidi katika shindano hili ili kuleta mabadiliko katika nchi hii.

Baada ya kumaliza Elimu yangu ya chuo kikuu mwaka 2017 na kupata shahada yangu ya kwanza ya Uchumi nilianza kujikita katika uchunguzi na tathmini juu ya mifumo ya Elimu yetu ya Tanzania hivyo pamoja Kuna maboresho mengi yamefanyika lakini nimeona nishiriki shindano hili ili kutoa mawazo yanatakayosaidia kuboresha Mifumo Bora ya Elimu Tanzania itakayosaidia kutoka miaka 5-25 ijayo.
YAFUATAYO NI MABORESHO BORA YA ELIMU

1. KUPUNGUZA WINGI WA MASOMO: Mara nyingi katika shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne wanafunzi husoma masomo takribani tisa mpaka kumi kitu ambacho kinakuwa ni mzigo mkubwa usiokuwa na tija kwani ili mwanafunzi aweze kusajiliwa anahitaji achukue masomo kuanzia Saba hata hivyo hiyo kanuni bado haijakaa vizuri kutokana na uhalisia huu mfano mwanafunzi ameamua kujikita kwenye ndoto ya mwanasayansi inamuhitaji kusoma masomo matano TU mfano Physics, chemistry, Biology, Geography na Mathematics. Kama ataweza kusoma vizuri kabisa na kuwa na ndoto ya Kuwa mwana sayansi mzuri ataweza kufaulu vizuri bila kujali hata hayo masomo mawili yanayokamilisha Saba kupata F atakuwa kafaulu kwa daraja zuri na tahasusi zake zikiwa zimebalance mfano PCB, EGM, PGM, CBG na PCM kwa namna hiyo hapo Kuna haja gani ya huyo mtoto kusoma masomo tisa wakati akisoma matano au saba TU anakuwa kafaulu na kutimiza ndoto zake kwa kusoa masomo machache.

2. Maboresho ya Bodi ya mikopo. Maranyingi mfumo wa Bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa kutenga mikopo kwa kujali aina ya kozi yaani kozi flani Ina priority na nyingine ni non priority katika kupata mkopo hii imepelekea wanafunzi wengi kuomba kwenda kusoma kozi wasizotaka na kufanya kazi bila ufanisi hiyo ikiwa imesababishwa na mfumo wa kupata mkopo kirahisi unaotumika mpaka Sasa. Nashauri serikali iboreshe mfumo wa kutoa mkopo usiwe katika muundo wakutenga kimakundi.

3. Mfumo wa machaguo Tamisemi kidato cha Tano na vyuo vyakati.
Katika mfumo ambao wanafunzi na wazazi wao pamoja na wananchi kwa ujumla wanapata tabu katika kupigania ndoto za watoto wao ni mfumo wa machaguo Tamisemi yaani mtoto kapata sifa ya kwenda kusoma kidato cha Tano kwa sababu kafaulu vizuri pia na tahasusi zake ziko balanced wakati huo hata kwenye fomu ya machaguo ya shule alijaza kusoma kidato cha Tano lakini Tamisemi wanakuja kumchagua kwenda kusoma chuo cha kati cha serikali Tena alipe gharama kubwa kiasi ambacho kwa familia nyingi za kimasikini haziwexi kabisa kumudu hivyo kupelekea watoto wengi kushindwa kuendelea na masomo kabisa na kupoteza ndoto zao.
Niwaombe serikali kuzingatia machaguo ya watoto Kama mtoto kaomba chuo basi achaguliwe chuo na Kama kaomba kidato cha Tano basi Kama kafikia vigezo vinavyohitajika achaguliwe kidato cha Tano.

4. Mfumo wa mikopo ya Elimu vyuo vya kati ( NACTE)
Bado serikali haijaweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wengi kunufaika na mikopo vyuo vya kati kwani imejikita kwa kada chache sana kitu ambacho tuna idadi kubwa ya watoto wanasifa ya kusoma vyuo vya kati na hawana uwezo wanatoka familia masikini sana. Ifikie kipindi kusoma kwenye nchi ya Tanzania isiwe na yenye kuwatenga watu kwa kada zao nashauri mamlaka husika kufanya MABORESHO BORA ya mikopo hiyo ili Kila mtoto wa mtanzania masikini mwenye sifa ya kusoma aweze kupata mikopo hiyo.

5. Mafunzo kazini yawe lazima na malipo yawe 0.25% ya basic salary kwa kada anayofanyia mafunzo.
Maranyingi serikali imejitahidi kuboresha namna ya wanafunzi kusoma Elimu zao za vyuo vikuu lakini wahitimu mtaani wanazidi kuongezeka na kuwa rasilimali watu wasiokuwa na tija hivyo Kuwa serikali imepoteza pesa zake kuwasomesha lakini pia tunaweza kupata watu watakao jiingiza kwenye kundi la waharifu au watu tegemezi. Pia ni tabaka lililopata mikopo ya serikali lakini lisiloweza kurejeshwa mikopo hiyo kwa muda wa miaka mingi kutokana na kuwepo kwa ukosefu wa ajira nchini. Lakini Kama serikali itaweza kuboresha mfumo wa mafunzo kazini( Internship) kwa hayo malipo tutafanikiwa kuwatumia hao wanafunzi na wao kupata malipo ya kujikimu lakini kupata uzoefu mkubwa wa kazi .

6. Mitihani ya mwisho ya Chuo kikuu iwe chini ya TCU na vyuo vya kati iwe chini ya NACTE.
Baada ya kuhitimu Elimu yangu ya chuo kikuu nilipata kujifunza mambo mengi kipindi nasoma nilichotathmini ni Kuwa mitihani ya U.E ya chuo kikuu iwe chini ya TCU na vyuo vya kati iwe chini ya NACTE kutokana na uhalisia Kuwa vyuo vingi inapofika mitihani ya mwisho katika Kila mwaka Kuna ubadhilifu mkubwa sana wa mitihani kuvuja au kusahihishwa kwa njia ya rushwa ya fedha na ngono hasa kwa wadada nakupelekea kupata wasomi wasiokuwa na sifa stahiki na kupoteza maadili ya Elimu yetu pia ufanisi katika majukumu ya kazi wakati akiajiliwa.
Nashauri serikali iboreshe mifumo ya Usimamizi ya Elimu ya vyuo vikuu na vyuo vya katiili tupate wasomi wenye sifa sahihi.

7.Tuwe na mfumo wa kuanzisha vituo vya usahihishaji wa mitihani ya kawaida shule za sekondari ( Local Examination marking center)
Maranyingi serikali imejitahidi kuboresha Elimu katika shule za sekondari nchini Tanzania lakini ukweli ni kwamba idadi ya walimu ni ndogo sana ukilinganisha na uhitaji wa wao. Hivyo kupelekea walimu kutumia nguvu kubwa katika kufundisha idadi kubwa ya wanafunzi. Pale inapofika kusahihisha mitihani ya mihula kazi ya kusahihisha inakuwa ngumu sana kutokana na idadi ya wanafunzi Kuwa kubwa hivyo hupelekea walimu kukodi wanafunzi wa madarasa ya juu au ya chini kusaidia kusahihisha mitihani hiyo Tena kwa ufanisi sifuri kwani swala la kusahihisha mitihani ni swala la utaalamu.

Hitimisho.
Kwenye Elimu yapo mambo mengi sana yanayohitajika kuboreshwa ili kupata vijana wenye Elimu yenye tija lakini kupata wafanyakazi watakaoleta ufanisi katika kazi zao na kuletea maendeleo makubwa taifa hili.
Naomba kuwasilisha mawazo hayo yatakayoleta mabadiliko makubwa katika Taifa hili.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom