SoC01 Namna bora ya kutoa elimu kuhusu athari za madawa ya kulevya

SoC01 Namna bora ya kutoa elimu kuhusu athari za madawa ya kulevya

Stories of Change - 2021 Competition

cey03

New Member
Joined
Sep 6, 2021
Posts
4
Reaction score
4
UTANGULIZI; Kama tufahamuvyo uraibu wa madawa ya kulevya unavyozidi kushika kasi na kuongezeka kwa kiwango kikubwa nchini kwetu. Hii inatokea hususani kwa vijana wengi miongoni mwao ni watoto walio chini ya miaka 18 katika maeno mbali mbali nchini.

Makundi mengi Kati yao yamekuwa yakijihusisha na utumiaji wa madawa mbali mbali ya kulevya Kama mihadarati, mirungi, heroini na kokeini hata bangi pia. Hali hiyo husababisha watu hao kupata madhara au kuathirika zaidi kiafya.

Kulingana na vyanzo vya habari kiwango kikubwa cha vijana ndiyo waathirika zaidi wa utumiaji wa madawa ya kulevya.

Kuna sababu mbali mbali zinazofanya vijana wengi kutujitumbukiza katika wimbi la utumiaji wa madawa ya kulevya. Lakini kubwa ambayo inaonekana kuzoeleka ni shinikizo la rika ambalo linawakumba vijana wengi Sana katika sehemu mbali mbali hususani mashuleni, vyuoni na mitaani.

Hii Ina maana kwamba vijana wengi hushawishika kutumia madawa hayo kama moja wapo ya starehe huku wakihimizana na kushawishiana kutoka rafiki au kijana mmoja kwenda mwingine. Inagawa wapo ambao hutumia kutokana na kuwa wapweke, kukosa kazi za kufanya ama kutokuwa na ujasili wa kukubalika katika jamii na kutengwa pia.

Wakati jamii nyingi nchini zikihusisha na mkumtambua mtumiaji wa madawa ya kulevya Kama mtu mhalifu,muhuni asiyefaa, na aliyekosa maadili katika jamii pia asiye na msaada kabisa. Wapo pia waathirika walioweza kupata tiba na wakaondokana na hili janga.

Katika taarifa Moja, serikali ilipendekeza juu ya utoaji wa elimu kuhusu athari za madawa ya kulevya na madhara yake kuanzia ngazi ya elimu ya sekondari. Ni jambo bora litakaloweza kuleta mapinduzi chanya zaidi katika kudhibiti utumiaji wa madawa ya kulevya nchini hususani kwa vijana wengi

Kuna namna Bora itakayoweza kutumika kusaidia kutoa elimu ambayo itakuwa rahisi zaidi kufikisha ujumbe kwa watu husika juu ya athari za madawa ya kulevya na madhara yake. Hii ni pamoja na kuwatumia wahanga wa madawa ya kulevya ambao watakuwa tayari wametibiwa, kupona na kuacha mara moja utumiaji wa madawa hayo.

Hiyo ni njia ambayo itafikia watu wengi kwa rika zote wakielezwa jinsi ya athari na madhara ambayo wamepitia wenyewe kutokana madawa ya kulevya badala ya kuwatumia tuu Kama mashuhuda katika maadhomisho ya vilele mbalimbali vya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya.

Wahanga waliopona katika janga hili la dawa za kulevya ambao kwa namna moja au nyingine waliweza kuathiriwa na hayo madawa ya kulevya , wanaweza kuwa na nafasi kubwa katika ushawishi kwa jamii kuhusu kutoa elimu ya madawa ya kulevya , madhara yake na namna ya kuepukana nayo kupitia njia mbali mbali walizotumia mpaka wakasalimika katika janaga hili.

Inaweza kuwa njia nzuri kwa kiwango kikubwa kwa mtu aliyepitia maswahibu hayo Kisha kupona, kuwa na nafasi nzuri zaidi katika kuelimisha wengine mara kwa mara juu ya athari hizo kwa vijana wadogo na rika la Kati, kuliko yule aliyesikia na kusoma tuu Kisha kuenda kutoa elimu.

Kwa serikali ikiweza itoe vipaumbele vya kuwa unganisha, kuwapa elimu ya namna ya kuwasilisha ujumbe katika jamii kubwa wale wote waliofanikiwa kupona na madawa ya kulevya na pia kushirikiana nao katika hatua ya kutoa na kusambaza elimu katika ngazi zote za kijamii na kielimu zaidi katika taasisi za elimu na vikao vya ndani ya jamii mfano kwenye serikali za mitaa ili kuweza kufikia wahanga wakubwa wa madawa hayo ambao ni vijana kwa ujumla.

Hivyo basi kwa namna hiyo inaweza kusaidia kutoa elimu ya moja kwa moja kuhusu athari za madawa ya kulevya na madhara yake kiundani zaidi kutoka kwa wahusika wenyewe waliopitia changamoto hizo.


Karibuni kwa maoni na mapendekezo ....
 
Upvote 3
Hapo njia bora ni Kutia vitanzi wale wote wanaouza Madawa ya Kulevya na kuziba Mianya isiingie Nchini,

Hatuwezi kumlaumu Mtumiaji sababu yule ni Muhanga bali Muuzaji sababu yule ni Muuaji,

Naungana nawe juu ya serikali kuwapa Elimu walioishinda vita ya Madawa ili wakatoe Elimu kwa vijana ambao wapo kundi hatarishi huku wakiendelea kuwasaka wauza Madawa na kuwapiga Risasi kimya kimya.
Ndiyo nakubaliana na wewe maana hawa wanaoziingiza wanaweza wakafanikiwa kuwakamata na kufungwa lakizi njia zao za usafirishaji na upitishaji zikawa Bado zipo wazi na hapo tatizo bado likawepo. Hvyoo ni lazima serikali itafute chanzo au Chanel yao kwanza.
Shukrani.
Kura yako tafadhali..
 
Madawa ya kulevya yameharibu vijana na ya mepelekea kupoteza nguvu kazi nyingi kwa taifa. Tatizo hili nikubwa katika jamii linasababishwa na hao wauzaji. Serikali inapaswa iwekeze haswaa katika kuwatafuta na kuwazibiti wauzaji wa dawa za kulevya. Pia vijana wapewe elimu itakayo wasaidia kujiamini na kuondoa dhana potofu ya utegemezi wa kutumia dawa za kulevya kabla ya kufanya jambo lolote.
Vijana nao waache kuiga mambo ya kigeni ambayo sio tamaduni zetu na jamii au familia ziwalee watoto vyema[emoji1317]
 
Ndiyo sapoti kubwa inahitajika kutoka kwa serikali tuanze kuona matendo zaidi ya mikakati waliyopanga huku wakihusisha wale waliopona Kama chachu ya kutambua chanzo halisi Cha usambazaji wa hayo madawa kwa kasi.
 
Back
Top Bottom