SoC03 Namna bora ya kuwatumia walevi katika shughuli za kijamii

SoC03 Namna bora ya kuwatumia walevi katika shughuli za kijamii

Stories of Change - 2023 Competition

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Habari jukwaa,
Ni saa mbili na dakika kumi na tano asubuhi nyuma ya nyumba moja ya vyumba vitatu ya mkazi mmoja katika viunga vya jiji la Amsterdam, Uholanzi, ambapo tunakutana na kundi la watu ishirini wakiwa tayari kuanza majukumu yao ya kuzunguka mitaa ya Amsterdam kufanya usafi, huku wakiwa na chupa za pombe pamoja na pakiti za sigara. Kisha hupangwa katika makundi mawili yenye watu kumi na kundi moja hufanya kazi kwa siku tatu.
IMG_1293.jpg


Wakiwa wamebeba mifuko na mifagio wakizunguka katikati ya mitaa na kukusanya usafi na kuhakikisha kuwa mji unakuwa msafi kama kawaida yake, huku malipo yakiwa sio fedha tu bali pia hulipwa tumbaku, chupa tano za pombe, huku wakipewa na kiasi cha shilingi za kitanzania 25,400.
IMG_1294.jpg


Ambaye alikuja na wazo hilo ni Gerri Hotlerman ambaye ndo kiongozi wa mradi wa rainbow foundation project, mpango ambayo upo chini ya serikali ya Uholanzi. Yeye binafsi anadai kuwa kundi hili la watu linaongoza kwa fujo, kelele pamoja na uvunjifu wa amani hivyo, njia pekee ni kuwafanya wawe sehemu ya kutunza mazingira.
IMG_1296.jpg


Kabla ya kuanza kwa shughuli ya usafi, kundi la watu kumi ambalo linatakiwa kufanya usafi hukutana na hupewa pombe chupa mbili ambazo huzinywa kabla ya kuanza kazi. Hii imekuwa ni njia nzuri sana kwa walevi sugu, na serikali imeona ni vyema kuwapa kazi kuliko kuwaacha wakizagaa mitaroni au wakifanya fujo ovyo.

IMG_1295.jpg


Kwa ajili ya chakula cha mchana, kundi hukutana na hupewa chakula huku pia wakipewa chupa mbili za pombe kushushiwa chakula kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya kazi ya jioni, na baada y kumaliza usafi wa hukutana mwishoni na hupatiwa chupa moja ya pombe muda wa saa tisa jioni.

Hii ndo mbinu pekee ambayo serikali ya mji wa Amsterdam imeweza kuwaweka pamoja walevi sugu huku wakitumika kuleta maendeleo ndani ya mji huu. Na kupitia mpango huu wamepata watu wengi wanaokuja kujitolea kufanya usafi wa mitaa ili wapate malipo ya shilingi 25,400 na vionjo vingine.
IMG_1297.jpg


Hotlerman anadai kuwa kupitia mpango huu wamerekebisha tabia za unywaji wa pombe, kwa kuwa mtu atapewa fedha zake na chupa za pombe kama malipo endapo tu aliweza kufanya kazi siku nzima bila kutumia pombe au kilevi chochote, ila kama ulikunywa basi ni sawa na kazi bure.

IMG_1299.jpg


Kwa mujibu wa hotlerman anadai kuwa mpango huu umewasaidia sana walevi hawa kupunguza kiwango cha unywaji wa pombe huku wakiwa ni watu wenye mchango mkubwa ndani ya Amsterdam. Na hata wakazi wa Amsterdam wamekuwa wakifurahi kuona namna ambavyo mpango huu wa rainbow foundation project umewabadilisha kabsa walevi sugu hao na kuwa watu wenye umuhimu mkubwa.

Lakini sio tu Amsterdam Uholanzi ndipo kwenye utaratibu huu wa kuwazawadia walevi katika shughuli za usafi bali hata Ujerumani napo kuna utaratibu huu katika mji wa Essen ambapo walevi sugu nao hutumika kusafisha mitaa yake, wameupatia jina la PICK-UP na malipo ni chupa za pombe pamoja na fedha.
IMG_1300.jpg


Ripoti maalumu kutoka kituo cha DW inasema kuwa watu wanaosumbuliwa na Ulevi sugu hutumika kufanya usafi katika mji wa Essen na sehemu za kituo cha treni.
Kituo cha Essen’s Addiction Help Center AHC ndo kinachosimamia mpango huu ambapo kama vile wanavyofanya rainbow foundation project huko Uholanzi basi napo Ujerumani wanatumia mbinu hiyo hiyo.

Pombe hutolewa kulingana na uhitaji wa mtu binafsi, ambapo washiriki hubadilishwa nguo na kuvaa nguo za kazi, hii ni saa nne na nusu asubuhi na huanza kazi mpaka mchana na hurejea na kupata chakula bila kupewa pombe, na hurudi kuendelea na usafi mpaka jioni ambapo hupata chakula na kufanya mazungumzo na wakati wa kuondoka kurejea majumbani ndipo hupewa chupa za pombe, huku kwa mtu mmoja huweza kupata mpaka chupa tatu za pombe.
IMG_1302.jpg


Kama wenzao waliopo huko Uholanzi pia Kituo cha Essen’s Addiction Help Center kimetengeneza mkakati bara bara ulio mzuri sana, kwani mshiriki hupewa chupa za pombe kama malipo kama tu aliweza kufanya kazi siku nzima bila kutumia pombe au kilevi chochote.

Baadhi ya washiriki hudai kuwa ni kitu ngumu sana kumaliza masaa sita bila kutumia pombe na endapo wakiweza kumaliza siku bila kutumia pombe basi kitu hiki huwajengea uwezo wa kujizuia na hata wakati mwingine wakishapewa malipo ya chupa za pombe hunywa chupa moja na zingine huweza kwenye jokofu.

IMG_1303.jpg


Hata bila kuwa na kazi ya kufanya basi unaweza kupata pombe ya bure kwa kufanya usafi, yaani kupita mitaani na kuokoa uchafu na kurudi na kupokea pesa yako na kurejea nyumbani. Huu ni mmoja wa mpango bora sana wa kuwabadilisha watu kutoka kuwa watu wasio na mchango kwenye jamii. Na unaweza kujiuliza kwanini nimeanza na visa hivi viwili vya wazi kutoka Uholanzi na Ujerumani.

Ila dhamira yangu ni kwamba, kwa kipindi kirefu Tanzania tumekuwa tukisumbuka na vijana na watu wenye uraibu uliopitiliza wa madawa ya kulevya, unywaji wa pombe mkubwa pamoja na ngono zembe. Naona ni haja sasa kwa Afrika na Tanzania tupate mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yataungana na mamlaka za miji kuondoa kabsa tabia hatarishi.

Mfano, kuondokana na watu kama omba omba tunaweza kuwatumia kufanya usafi katika miji mbalimbali za Tanzania, leo tunamzungumzia uchafu unaoisumbua dar es salaam ila je tukianzisha utaratibu wa kuwatumia kundi hili kufanya usafi huku tukiwapatia sehemu ya makazi na mtaji mdogo wa biashara kuendesha maisha yao.
IMG_1307.jpg



Katika siku moja kuna masaa 24 ila ukimpatia masaa mawili asubuhi ya kufanya usafi na masaa mawili ya usiku kufanya usafi kwa hakika ipo siku tutapishana na vipepeo na uoto mzuri wa asili pale Ubungo mataa.
Kuondoa tatizo la vijana wanaovuta bangi katika mitaa mbalimbali ya Mwanza haina haja ya kutumia nguvu ya polisi, ila tunaweza kuwatumia kufanya usafi katika bonde la mto Mirongo ili tusichafue hali ya mazingira ya ziwa Viktoria.
IMG_1305.jpg


Tusitumie nyundo kuwaua mbu waliopo kwenye vichwa vyetu, ni nguvu kidogo kwenye ufahamu mpana. Wale vijana wanaosumbua kwa kuleta fujo ndani ya jiji la Arusha haina haja ya kuwapeleka gerezani bali tuwabadilishe na kuwabadilisha kuwa watu wenye mchango mkubwa ndani ya jamii, tuwatumie katika kulinda mazingira ya pale kwenye mgodi wa Mererani.
IMG_1306.jpg


Nakupenda sana Tanzania! Nakupenda sana wewe Tanzania yangu.
 

Attachments

  • IMG_1301.jpg
    IMG_1301.jpg
    25.4 KB · Views: 3
  • IMG_1304.jpg
    IMG_1304.jpg
    25.3 KB · Views: 4
Upvote 6
Nimekagua picha za Huko ugaibuni ulizo attach nikaona ni pasafi kweli kweli, za Hapa kwetu bongo umeweka mbili tu na kila moja ina Uchafu haswa na uchafu huo ni Magari, aisee sikulijua hilo ila ukichunguza vizuri utakubaliana na mimi, kujaza Magari barabarani ni Uchafu.
 
Nimekagua picha za Huko ugaibuni ulizo attach nikaona ni pasafi kweli kweli, za Hapa kwetu bongo umeweka mbili tu na kila moja ins Uchafu haswa na uchafu huo ni Magari, aisee sikulijua hilo ila ukichunguza vizuri utakubaliana na mimi, Kuchaza Magari barabarani ni Uchafu.

Umefanya nicheke [emoji2]
 
Acha kuwasumbua walipa kodi wakubwa🤣🤣


Ila hili bandiko lako ni Gud sana ,Hongera kamanda!!
 
la dhamira yangu ni kwamba, kwa kipindi kirefu Tanzania tumekuwa tukisumbuka na vijana na watu wenye uraibu uliopitiliza wa madawa ya kulevya, unywaji wa pombe mkubwa pamoja na ngono zembe.
Mkuu nitashukuru sana ikiwa hii project itaanza mapema hapa nchini ili na sisi wapenda ngono tuwe na kazi ya kufanya. The early, the better! Walevi watakunywa pombe zao na sisi wapenda ngono tutadinya. Asante kiongozi wangu, nakukubali sana.
 
Mkuu nitashukuru sana ikiwa hii project itaanza mapema hapa nchini ili na sisi wapenda ngono tuwe na kazi ya kufanya. The early, the better! Walevi watakunnywa pombe zao na sisi wapenda ngono tutadinya. Asante kiongozi wangu, nakukubali sana.

Hapo kama mdau wa maendeleo naweza kuchangia mawazo yangu kuwa;

1. Ni kweli tunaweza kuwa na mradi mahususi kwa ajili ya waraibu wa ngono; mfano, wakifanya usafi vyema siku nzima bila kufanya ngono; tunaweza kuwapatia mipira ya kujikinga pamoja na pesa mathalani na mahala pa kupoza hamu yao.

2. Lakini pia tunaweza kutumia mradi huu kuwapa elimu na utimamu na akili kupitia madarasa ya ushauri nasaha haswa linapokuja suala la uraibu wa ngono.

NB: Hii italeta mchango mkubwa sana katika jamii kupata maendeleo kupitia makundi haya.
 
wakifanya usafi vyema siku nzima bila kufanya ngono; tunaweza kuwapatia mipira ya kujikinga pamoja na pesa mathalani na mahala pa kupoza hamu yao.
Mimi nashauri wawepo wanawake maalumu watakaokuwa wakiwapoza kiu ya ngono kabla na baada ya kufanya kazi, kama ilivyo kwenye pombe. Kwa mfano, asubuhi unapiga viwili na baada ya kazi unapewa tena viwili unarudi nyumbani kwako mwili ukiwa mwepesi kama karatasi.
 
Mimi nashauri wawepo wanawake maalumu watakaokuwa wakiwapoza kiu ya ngono kabla na baada ya kufanya kazi, kama ilivyo kwenye pombe. Kwa mfano, asubuhi unapiga viwili na baada ya kazi unapewa tena viwili unarudi nyumbani kwako mwili ukiwa mwepesi kama karatasi.

Mbona dozi itakuwa nzito sana!
Tufanye hivi; mtu aangaliwe je uraibu wake ukoje? Hapo ndo tutajua kama apewe dozi ipi kwa muda gani? Na dozi iwe kwenye ushauri nasaha ili aondokane na tabia yake sio kuendeleza uzinzi [emoji847]
 
Sasa mkuu hapo kuweka mmea wa Bhangi unahusika vipi na mada yako?

Mimi navuta bhangi na nipo na kazi yangu inayoniweka mjini na kulisha familia bila shida

Tutake radhi asee
 
Sasa mkuu hapo kuweka mmea wa Bhangi unahusika vipi na mada yako?

Mimi navuta bhangi na nipo na kazi yangu inayoniweka mjini na kulisha familia bila shida

Tutake radhi asee

Kwanza naomba nikuombe samahani wewe pamoja na watumiaji wote wa mmea huu.
Nimeuweka sio kwa nia mbaya bali ni kama njia ya kuoanisha tu kile nilichokisema kuhusu kundi tofauti ambalo linatumia mmea huu kupitiliza yaani uraibu.

Pole sana Mkuu kama umepata tatizo [emoji22]
 
Back
Top Bottom