Namna gani marafiki wanaweza kuathiri biashara yako

Benittotz

Member
Joined
May 24, 2018
Posts
68
Reaction score
123
NAMNA GANI MARAFIKI WANAWEZA KUATHIRI BIASHARA YAKO. /UNAO WAITA "WATU WAKO" KAMA HAWASUPPORT UNACHOFANYA SIO "WATU WAKO".

NI wazi kuwa watu nchi yetu imejengwa kwa misingi ya ujamaa na kusaidiana. Tukiwa na sifa lukuki za ukarimu na amani. Lakin pia ni wazi kuwa asilimia Kubwa ya ukarimu wetu tunauonyesha kwa wageni zaidi Huku wale watu walio karibu nasi tukiendelea kuwachukulia poa. Sina maana kuwa tuwabague wageni,la hasha lakini wazungu wanasema favor begins at home. Kama hatuwezi kuwasupport tunaowaona na kuwaita marafiki NI unafiki kusimama na kuonyesha sura ya ukarimu mbele za watu.

Leo nataka tuongee kwa ufupi kuhusu namna urafiki wetu unaweza kuwa na athari katika biashara zetu. Hususani athari hasi.

Kuna nadharia zinasema kuwa ukianza biashara usiwategemee watu wako wa karibu kuwa wateja wako, kwa kuwa hutajua wananunua bidhaa kwa sababu ni nzuri au kwa sababu wanakufahamu.
Lakini mimi nadharia yangu ni kwamba uapoanza biashara soko lako la kwanza ni Hawa unaowaita marafiki zako. Marafiki wa kweli wanaopaswa kukupa mrejesho kuhusu bidhaa yako, maoni na marekebisho. Marafiki wanaopaswa kusimama na wewe na kuwa mabalozi wazuri.

Je? Hali ndivyo ilivyo huko mitaani? Marafiki zetu ni wateja wa bidhaa zetu?Huwa wanahubiri kuhusu huduma zetu kwa watu wengine Kama ambavyo marafiki wa kweli hufanya?.

Hebu tazama mfano mdogo, unafanya biashara ya nguo, samani za ndani au vifaa vya umeme. Marafiki zako wana bidhaa hizi, na wanaendelea kununua kila siku. Je wamewahi kununua kwako? huwa wananunua kwako? Na si ajabu wamenunua sehemu ambayo wanauza Bei sawa na wew au pengine chini ya wewe. Na Kama Bei yako ni tatzo au ubora wako sio ule wanaoutaka wamewahi kukuambia? Kama majibu Katika maswal hayo yote ni hapana, Je bado Hawa watu ni marafiki zako tu?.
Vipi kwa wale wenzetu wanaotoa huduma za burudani mfano kwa washereheshaji, wachekeshaji,watumbuizaji na kadhalika. Marafiki zenu huwa wananunua tickets za show zenu au wapo katika kundi la complimentary ( tickets za bure) Wanakuahidi kuja kukusupport kwa wewe kuwapa tickets za bure na bado wanaiita hiyo ni support? is t really a support au NI njia nyingne rahisi ya kurudishana nyuma?
NI wakati Sasa wa kutazama Aina ya marafiki na mchango wao katika mafanikio yetu kijamii na kiuchumi pia. Lazima tutengeneze constructive relationships Kama kweli tuna Nia na makusudi ya kufika tulipokusudia. Marafiki wa kugeuza sehemu yako ya biashara kijiwe Cha story, saccoss ya mikopo ilihali wanapokuwa na uhitaji wa kununua cash wewe sio chaguo la kwanza sio marafiki unaowahitaji. Marafiki wanokumbuka kukitafuta katika michango ya harusi, kwenda sehemu za starehe na sehemu zinginezo bila kuwa na impact yoyote positive katika harakati zako NI muda wa kuwapiga chini Sasa. Chukua hatua, jenga himaya yako vizuri.

NB: UNAKARIBISHWA KUJIUNGA NA DARASA LANGU LA BIASHARA KUPITIA GROUP LA WATSAP KWA ADA YA TSH 2,000/= (ELFU MBILI TU) KWA WIKI.
MAWASILIANO YAPO CHINI HAPO.

IMEANDIKWA NA
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA
MSHAUR WA MASWALA YA BIASHARA.
Email bensonflexon@gmail.com
Facebook Benson Flexon Shirima
Instagram@benitto_tz
watsap 0654859954
Call/text 0653384656
 
But also don't forget the positivity of friendship in business ! Hasa kwa wafanyabiashara wadogo yaan start up ambao hawana capital ya kuanzia the only means to get fund is from family and friends and not bank , Sacco's or elsewhere
 
Nililizungumizia Hilo katika makala iliyopita, makala hii nilitaka kutazama namna gani baadhi ya marafiki wanaweza wasiwe na mchango katika biashara yako
 
urafiki na biashara ni vitu viwili tofauti rafiki hawezi kukuonesha sehemu ya mchongo zaidi zaidi ata taka yeye awe kwako ndo mchongo kitokeo chake unakula hasara.

mfano amegundua kunasehemu bidhaa ni bei ndogo sana hakwambii ye atachukua kisha anakuja kukuuzia wewe kwahiyo anajitengenezea soko kwako badala akuelekezee atoako unafuu huo.
 
Back
Top Bottom