Kwa takriban mwaka mmoja sasa nchi nyingi za Afrika zimeendelea kukabiliwa na upungufu wa fedha za kigeni, hasa dola, fedha zinazotumika katika uagizaji wa bidhaa mbalimbali.
Sababu kubwa zinazotajwa na wataalamu ni kubadilika kwa sera za kifedha nchini Marekani, pamoja na kuongezeka kwa gharama za kuagiza bidhaa. Katika mlolongo huu, nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania zimekuwa zikishuhudia shilingi yake ikishuka kwa kasi.
Tanzania kama nchi nyingine Afrika, inahitaji fedha za kigeni kuagiza baadhi ya mahitaji yake muhimu lakini pia kulipa deni lake. Sehemu kubwa ya mahitaji hayo ni kama mafuta, mitambo, chuma, mbolea, madawa na bidhaa za vyakula.
Takwimu kutoka Benki Kuu ya Tanzania inaonesha mafuta ni moja ya bidhaa inayoigharimu nchi kiasi kikubwa cha fedha katika uagizaji. Kwa mfano kati ya mwaka 2020 mpaka 2023, Tanzania ilitumia Trilioni 21.9 kuagiza mafuta nje, ikifanya kuwa biadhaa iliyotumia fedha nyingi zaidi sawa na takribani asilimia 19.5 ya Trilioni 111.9 zilizotumika kuagiza bidhaa katika kipindi hicho.
Kwa mujibu wa Wizara ya Nishati, takribani asilimia 80 ya mafuta yote yanatumika katika mikoa 10, yaani Dar es Salaam, Mwanza, Pwani, Arusha, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga, Iringa na Kagera. Hata hivyo asilimia 32 ya mafuta yote yanatumika Dar es Salaam.
Katika wazo langu hili, ninaonesha namna halmashauri za Dar es Salaam zinavyoweza kuongoza nchi katika kupunguza utegemezi wa mafuta yanayogharimu fedha nyingi za kigeni, na kuongoza njia katika kuhamia katika matumizi ya gesi asilia.
Halmashauri Zitengeneze Kampuni Mpya ya Biashara ya Gesi Asilia
Dar es Salaam ina halmashauri tano yaani halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, manispaa ya Temeke, manispaa ya Kinondoni, manispaa ya Kigamboni na manispaa ya Ubungo.
Hizi ni halmashauri zenye uwezo mkubwa zaidi kimapato, huku halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na Kinondoni zikiongoza kwa mapato ya ndani, katika halmashuri zote 184 za Tanzania. Kwa mwaka 2022/23, halmashauri zote za Dar es Salaam ziliweza kukusanya takribani Bilioni 240 za mapato ya ndani.
Katika wazo langu hili ninashauri halmashuri hizi ziungane na kuanzisha mradi wa pamoja kuwawezesha Watanzania kuhamia kwenye matumizi ya gesi asilia. Hii haitakuwa mara ya kwanza halmashauri hizi kuungana katika mradi, mfano mwaka 2001 halmashauri hizi ziliungana na kuanzisha benki ya DCB kwa mtaji wa Bilioni 26.89.
Sekta ya gesi ni biashara inayochipukia lakini yenye uhitaji mkubwa. Kupanda kwa gharama za mafuta kumefanya Watanzania wengi kushawishika kuhamia kwenye matumizi ya gesi asilia hasa kwenye vyombo vya moto.
Hata hivyo gharama bado sio rafiki, wastani wa gharama za kubadilisha gari kwenda kwenye mfumo wa gesi asilia ni takribani shilingi milioni 2, gharama ambazo ni vigumu kwa watu wengi kuweza kuzimudu kwa mara moja.
Katika pendekezo langu nashauri halmashauri za Dar es Salaam kuanzisha kampuni, itakayokuwa inaendeshwa kiusasa kwanza kuwawezesha wakazi wengi wa Dar es Salaam kuweza kubadili mifumo ya magari yao kwenda kwenye gesi asilia, lakini pili kuwekeza kwenye kuweka vituo vya gesi asilia ndani ya jiji la Dar es Salaam. Uwekezaji ambao napendekeza halmashauri hizi ufanye ni asilimia 15 ya mapato yake kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani bilioni 100.
Katika kubadili mifumo ya magari, ili kutengeneza soko kubwa badala ya wateja kulipa kiwango kitakachowekwa kwa wakati mmoja, kampuni hii inaweza kuweka malipo kufanyika kidogo kidogo katika kipindi cha walau miezi 18.
Ukusanyaji wa malipo haya ufanyike kwa kutumia njia za kielektroniki, kama ambavyo ilivyo kwa sasa ambapo faini za polisi zinavyokusanywa.
Lakini pia kampuni hii ya halmashauri ianzishe vituo vyake vya gesi asilia, hii ni kwa sababu bado wawekezaji wa kawaida wameonesha kusita sita kuingia kwenye biashara ya gesi asilia pamoja na kuwepo kwa uhitaji unaokua kila kukicha.
Vituo hivi vinaweza pia kutumika kukusanya malipo ya ubadilishaji mfumo wa wateja wa kampuni hii.
Muendelezo wa Biashara ya Gesi
Kwa mujibu wa Mamlaka ya udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) hadi Februari 2024, jumla ya futi za ujazo wa gesi asilia zilizogundulika Tanzania ni Trilioni 57.4, huku toka gesi imeanza kutumika mwaka 2004 Tanzania imeweza kutumia kiasi kisichozidi Trilioni 0.7 (asilimia 1) , sehemu kubwa ya gesi hii ikiwa imetumika kwenye kuzalisha umeme, yaani asilimia 65 ya umeme Tanzania unatokana na gesi.
Hivyo kwa kuanzia, Tanzania ina gesi ya kutosha kuhakikisha upatikanaji wa kufikia uhitaji wa sasa na wa baadae. Hii inahakikisha kwamba kuna mawanda mapana kwa biashara ya gesi, hivyo kuweza kurejesha fedha za mtaji na hata kuingiza faida kwa wawekezaji.
Kampuni mpya ya halmashauri inaweza jitengenezea fursa zaidi kwa kuweka lengo kubwa zaidi katika muda wa kati, yaani kuingia pia katika biashara ya kusambaza gesi majumbani. Baada ya kampuni kukaa katika biashara ina uwezo mkubwa wa kuanza kumiliki mabomba yake ya gesi au kushirikiana na TPDC kujenga mabomba ya gesi na kusambaza gesi kwa matumizi ya nyumbani.
Fursa nyingine ni kutokana na kuwa kwa kiasi kikubwa matumizi ya gesi asilia yanapunguza hewa ya ukaa, kampuni hii inaweza ikapewa ruhusa na halmashauri pia iangalie uwezekano wa kutanua mawanda ya biashara ya kampuni na kutengeneza mradi wa biashara ya kaboni.
Yaani kampuni itengeneze mradi mahususi kwa kutumia biashara inayoifanya pamoja na fursa nyingine ndani ya halmashauri za Dar es Salaam na kuingia kwenye biashara ya kaboni. Biashara ya kaboni ni bishara ambayo miradi mbalimbali inayopunguza hewa ya ukaa katika mazingira inaweza kulipwa na makampuni na taasisi ambazo shughuli zake zinachangia katika kuongeza hewa ya ukaa.
Kwa mustakabali huu kampuni hii mpya ya halmashauri inaweza kuwa na vyanzo vinne vya mapato moja kuuza gesi kupitia vituo vyake, pili mapato kutokana na kubadilisha mifumo ya vyombo vya moto, tatu kupitia miradi ya kaboni na nne katika mpango wa muda mrefu kusambaza gesi majumbani.
Kama misingi mizuri ya kibiashara ikiwekwa, kampuni hii inaweza pia kuja kuhusika katika biashara kubwa zaidi ya uzalishaji wa gesi kama mmoja wa washirika.
Kupitia kampuni hii halmashauri za Dar es Salaam zinaweza kujihakikishia mapato ya miongo mingi; mapato yanayoweza isaidia halmashauri hizi kukabiliana na changamoto ya msongamano wa watu na hata kuboresha jiji kuwa la kisasa zaidi. Lakini pia kwa kiasi kikubwa nchi itakuwa imepunguza utegemezi wa mafuta.

Upvote
4