Namna kushinda mijadala ya mtandaoni

Namna kushinda mijadala ya mtandaoni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
NAMNA YA KUSHINDA MIJADALA YA MTANDAONI!!

By
Æfrica Macka Bara
----------------------------------

Ghadhabu imepanda, joto limekuwa kali sana baada ya kuona Mtu fulani akipingana na mawazo yako ama kupost jambo usilopenda mtandaoni linalopinga mtazamo wako wa kidini, kisiasa, kiafya, kiuchumi na kijamii? Basi, suluhisho si kughadhabika. Hapa nimekuandalia njia kuu SITA za kushinda mijadala kama hii na kuyateka mawazo ya wale wanaopingana na Mawazo yako.

1. USIPIGANE VITA BILA KUMTAMBUA ADUI YAKO.

Je wahisi aliyepinga hoja zako ni adui yako? Hapana, Adui yako mkubwa si mpinzani wako bali ni mawazo ya mpinzani wako. Kumuona mpinzani wako kama adui yako ni kushindwa kutambua hasa adui yako ni nani katika Mjadala. Badala ya kumchukulia kama adui yako, mchukulie kama rafiki aliyekabwa na mfupa wa samaki shingoni ambaye anahitaji msaada. Hutochukua uamuzi wa kukata shingo lake ( kumtukana, kumblock na hata kumtoa katika group) ili kuuondoa mfupa, badala yake utatafuta njia rafiki za kuuondoa mfupa Huo na Rafiki huyu kubaki salama.

2. KUTAMBUA DHUMUNI LA VITA NI HATUA YA PILI YA KUSHINDA VITA

Huwezi kupigana vita ukashinda bila kujuwa dhumuni La vita ni nini. Kusoma makala kwa juu juu ama Kusoma kasehemu kafupi na kuanza kuishambulia makala nzima bila kuisoma kwa kina hadi mwisho ni sehemu muhimu sana ya kushindwa hii vita. Kabla ya kujibu LOLOTE, hakikisha Umetambua LOTE.

3. HASIRA HUONDOA MAARIFA

Huwezi kushinda vita ukiwa umeghadhibika. Kujaribu kujibu hoja ukiwa umejawa na Hasira moyoni kwaweza saidia ila kwa muda mfupi sana. Kadiri muda unavyozidi kwenda, ndivyo unavyozidi kudondosha hoja za msingi chini na kuanza kuandika hasira kama hoja.
pindi unapokutana na Makala usiyokubaliana nayo, usijali— waweza kujaribu kuiacha kama ilivyo. Kama wahisi una point za msingi za kujibu na una hamasa ya kujibu ila umeghadhibika kwa wakati huo, nakili Mahala ulipoiona hiyo post, na baada ya akili kurudi katika utulivu waweza kujibu kwa hoja.

4. KUTAMBUA MBINU NA SILAHA ZA MPINZANI WAKO KATIKA UWANJA WA VITA, NI KUMSHINDA KWA ASILIMIA 50.

Badala ya kuanza kumkejeli mpinzani wako na kutoa hoja zako, ni vema kama Utatambua mwandishi wako anatoa wapi hoja zake, na kuwa na ppingamizi zenye kina juu ya hoja zake. Kwa kuzipinga hoja zake kwa kutumia madhaifu ya hoja zake, utakuwa umemvuta kutaka kufahamu hoja zako.

5. TUMIA KIFAA MAHUSUSI KUJIKINGA NA SILAHA ZA MPINZANI.

Askari awapo katika uwanja wa vita, basi lazima awe na kofia ya chuma iwezayo kuzuia mashambulizi katika sehemu ya kichwa, na Kizuizi risasi kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya kifua. Vile vile, mpinzani wako akuulizapo swali, pendelea sana kutumia Jibu sahihi kujibu swali lake, na Baada ya kulijibu kwa usahihi litolee maelezo ya kina yenye ushahidi.

6. USIMSHAMBULIE MPINZANI ALIYEWEKA SILAHA CHINI NA KUINUA MIKONO.

Waweza tumia njia ya kumkejeli na kumdharau yule uliyemshinda kwa hoja, lakini hiyo haitosaidia. Badala yake, mgeuze kuwa mateka wako kwa kumfanya azidi kuamini hoja zako zenye ushawishi. Na baada ya muda ataanza kuwa na mtazamo ulio nao. Kumshambulia aliyekwisha kujisalimisha kihoja ni kuamsha uadui badala ya elimu huru yenye kuleta mabadiliko.

Mijadala ya mtandaoni si vita ya kuvuja damu ya mtu mwingine, ni njia ngumu ya kufikisha mawazo yako kwa wasomaji na kuyashinda mawazo yake bila kutumia upanga. Ni vema kama kila mwandishi angetambua lengo la kuandika, na njia rafiki za kushinda mioyo ya wale watakaopinga mawazo yake, kuliko kuleta mawazo mbele ya hadhira bila kuandaa njia rafiki za kukabiliana na Mawazo pinzani.
 
Mijadala ya mtandaoni si vita ya kuvuja damu ya mtu mwingine, ni njia ngumu ya kufikisha mawazo yako kwa wasomaji na kuyashinda mawazo yake bila kutumia upanga. Ni vema kama kila mwandishi angetambua lengo la kuandika, na njia rafiki za kushinda mioyo ya wale watakaopinga mawazo yake, kuliko kuleta mawazo mbele ya hadhira bila kuandaa njia rafiki za kukabiliana na Mawazo pinzani.📌🔨
 
Back
Top Bottom