Namna mbalimbali za kuwa Milionea hutegemea na Style Uliyotambaa nayo Utotoni

Namna mbalimbali za kuwa Milionea hutegemea na Style Uliyotambaa nayo Utotoni

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Hili somo ni refu kidogo! lakini nitalifupisha kwa ku-summarize!

Yapo Mambo mengi watu hamyajui na hamjawahi kufikilia yana nguvu gani katika maisha!
Kabla ya sayansi ya maabara haijaifunika dunia Tulikuwa na sayansi Asilia ambayo Ni pana Sana!

Leo nitawashirikisha Siri iliyofichwa kwenye chimbuko la kutambaa!

Nitaichambua mada hii pasipo kuchanganya na somo la nyota!
Binadamu anapozaliwa, Anapotoka tumboni mwa mama yake Ni lazima A-subscribe kuonyesha kujiunga na ulimwengu kwa kulia ,(Lazima mtoto alie punde akishazaliwa, Sayansi ya maabara inaamini ktk kutanua mapafu,Lakini Ukweli Sayansi Asilia inachimba zaidi ya hapo, Lipo somo nitaandaa kuhusu Sauti ya mtoto anapolia Mara ya kwanza huashilia nini maishani mwake)

Je; Ni Wakati gani mtoto anachagua kuwa Milionea! (KUTAFTA RIZIKI)

Katika hatua za ukuaji! ipo Siri iliyofichwa kwa mtoto katika kukua, na ndiyo maana Washirikina hupenda kuchezea Sana (KUTIA ZONGO) hatua hiyo kwa mtoto maana ndipo msingi wa utajiri ulipo!

Hatua hii ya ukuaji wa mtoto (Kukaa, kutambaa,kusimama na kutembea) Huwa haifanani; Jiulize kwanini?

Wapo watoto huruka baadhi ya stage mfano anaweza kukaa na asitambae then Atasimama na kuanza kutembea n.k!
Ipo Siri kubwa Sana hapo!

Chunguza mtoto anapoanza kukaa kabla ya kutambaa na kusimama huwa Kuna wakati anaonekana ukimuangalia anakuwa Kama ana mawazo flani hivi anawaza (feelings) ( then baada ya hapo hupiga miayo as if ana majukumu makubwa yanayomkabili!

Tambua Hapo ndipo huonyeshwa namna vile atakavyopata RIZIKI zake Ukubwani!
EBU TUONE AINA ZA MBALIMBALI ZA KUTAMBAA (kutafuta RIZIKI)

1. Wale wanaotambaa kwa magoti kabla ya kusimama na kutembea!

Hawa ndiyo wengi, Hii huwa inamaanisha hawa watoto RIZIKI zao Ukubwani watazipata taratibu, kwa mtiririko, Mali zao nyingi watu hawa hutokana na ujira wa kawaida, kilimo Cha miaka mingi, ufugaji ule wa kuanza na mifugo michache na kupanda taratibu; Kiufupi Utajiri wa watu hawa hutegemea kujinyima ili kufikia U-Milionea!
Mfano; Wajiliwa nyazifa za kawaida,walimu , wakulima wadogowado n.k

2. Wale watoto wanaotambaa kwa matumbo!
Hawa watoto hulamba Sana mchanga, Hii Ni ishara hawa watoto watahitaji Kufight Sana katika maisha yao kuusaka Utajiri, na Mara nyingi hufanya vizuri Sana wakijiingiza kwenye kazi zenye chimbuko la Kusota mwanzoni!

Mfano Jeshi, Mpira au mwanariadha, mwanamasumbwi,ndondi au hata kuendesha mitambo mikubwa! Mafanikio yao hubadili historia ya familia na kujenga heshima.

3. Watoto wanaotambalia Makalio
Hawa ndio watu huwa tunawasikia, Mimi kazi flani na flani sifanyi Bora kufa, Hii yote Ni kwasababu walitambalia Makalio, Kijijini watu hawa nawafananisha na wale wanasubiri mifugo irudi zizini Wakamue maziwa,
Hawa ndiyo wale wafanya biashara ya kina KANGOBA Wanalangua mazao ya wakulima!
Hawa ndiyo wale wafanya kazi ambao wako idara yako wavivu Sana Ila kwenye posho wapo makini Sana, Hawa ndiyo wale wakurugenzi ambayo hupenda posho za vikao hata Kama kikao hakukaa lakini jina lake lazima liwe la kwanza juu! , kiufupi Utajiri wao uko humo humo na hufanikiwa kwa style hiyohiyo n.k
Pia wanajua Sana kutumia nafasi walipatiwa nafasi za uongozi, Hawa Ni wale wanasiasa wanaotumia mianya ya matatizo kukitajilisha wao!

4. Kuna wale watoto wanaotambalia Mgongo chali Kama wapiga mbizi kichalichali!

Hii Ni ishara ya masafa, watu wa namna hiyo Utajiri wao uko kwenye masafa, mfano RUBANI wa ndege, Nahodha, yaani kazi za kusafili (usafilishaji) huko ndiko u -Milionea wao uliko.

5. Kuna wale watoto wanaruka Kama chura!
Yes! Ni wachache lakini wapo!
Hawa Utajiri wao upo kwenye Kuvizia! Utajiri wao umefichwa kwenye kuwahadaa wengine! Mfano watoa mikopo, Unaomba mkopo unaweza dhamana Nyumba ukishindwa anachukua, Unaweka dhamana Gari ukishindwa anachukua n.k
Yaani Utajiri wao umejificha kwenye Tyming! (wapo kisheria zaidi) na endapo wakiwa kwenye ajira Basi hupenda Sana kazi zinazoambatana na mahakama!

6. Kuna Watoto ambao hawatambai yaani Hukaa na kusimama ghafla kwa kushika chochote kilichokaribu

Huku utakutana na wale wenye kujua kujikomba, yaani ukaribu wao unamtegemea aliyefanikiwa! Hapo ndipo utakutana na wale wanaohakikisha wanaolewa na tajili na kusubiri urithi wa mme/ mke tajili afe wawe Milionea!
Kiufupi utajili wao Ni wa kuchota siyo kumimina!
Hapo ndio hao wakibeti wanashinda mamilioni kwa mkeka mmoja tu!
Hawa ndiyo wenye kismart na mazali, akiingia mgodini harudi mikono mitupu!
Hawa ndiyo wale wanaomaliza chuo na kupata ajira kitengo nyeti Sana pasipo kutumia nguvu! Yaani hadi wengine mnashangaa!

HIVYO KUWA MILIONEA INATEGEMEA SANA NA ULIVYOTAMBAA UKIMUONEA GERE MWENZAKO UNAJISUMBUA
 
Hii peleka ubongo kids
Ukisikia somo la nyota lilivyo ndivyo hiyo nayo inavyofanya kazi!
Nitakupa mfano?
YESU ALIPOZALIWA ALILAZWA KWENYE ZIZI LA NG'OMBE!
Ukisoma utaona Nyota yake yule mtoto ilionekana toka mashariki ya mbali (kina mama Jusi Waliona katika ulimwengu wa roho kuwa Kuna mtoto mwenye nguvu kazaliwa)
Hapo hukusikia Yesu katambaa Kama wewe! Na hutakaa usome kuwa Yesu alitambaa, Bali utakuja kuona harakati zake!
Maanake! Mafanikio yake yalikuwemo kwenye NGUVU ASILIA soma namba 6
 
Hiyo #1&2 imeniingia kisawa sawa nampigia Maza hapa simpati nilitaka aniambie kama anakumbuka nilipokuwa kwenye stage ya kutambaa nilitambaa kwa style gani!
sawa! Kama ankumbuka vizuri utakuwa humo humo
 
Back
Top Bottom