Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Habari!
Nadhani watu wengi mmeshawahi kuskia watu kadha wa kadha wakisema ya kwamba dunia inaendeshwa ki mfumo, ila pia mlio wengi huwa hampati nafasi ya kuuliza watu hao wanaosema hivyo wanamaanisha nini na badala yake huwa mnaishia tu kukubaliana nao au wachache ambao wanapata kuwauliza watu walioleta hoja za namna hiyo wanashindwa kupata majibu yaliyonyooka kwasababu yawezekana watu waliokuja na hoja hiyo nao walisikia tu pahala ila hawana uelewa wowote na jambo hilo au wanaelewa ila hawataki kukufumbua kwa lengo la kutaka uendelee kubuluzwa.
Sasa kwenye kipengele hiki nitakwenda kuelezea mambo haya ya kimfumo pamoja na nguvu za asili katika mambo mbalimbali yaliyo tuzunguka hapa duniani hasa yale yanayotugusa moja kwa moja kwa mfano fedha kwa kutumia mifano mepesi mepesi ambayo itakua rahisi kueleweka.
Nianze kwa kukuhakikishia tu ya kwamba ni kweli dunia na vyote vifanyikavyo ndani yake ili viweze kustawi na kufikia kwenye kile kiwango cha kutambulika na watu wa dunia huwa ni lazima viwe katika mtindo wa kimfumo.
Sasa mfumo ni nini? Mfumo ni mjumuiko wa nguvu nne za asili ya uumbaji wa ulimwengu ambazo ziliwekwa kwa lengo la kuujenga na kuuendesha ulimwengu katika namna tofauti tofauti.
Nguvu hizi nne za asili ndizo ambazo zinatumika katika mifumo yote ya dunia na ulimwengu kwa ujumla wake na jambo lolote ambalo litaanzishwa duniani lisipowekewa angalau nguvu moja ya asili ya uumbaji wa ulimwengu kati ya zile nne basi haliwezi kuwako kwa hii dunia.
Lakini pia kama ambavyo nimekua nikisema hapo nyuma basi niendelee kwa kusema na hapa ni kwamba jambo la umuhimu zaidi hizi nguvu huwa zinafanya kazi kwa kutegemeana na ndio maana uimara na udhaifu wa mfumo wowote ule huwa unatokana na namna hizi nguvu zinavyofanya kazi katika mfumo husika.
Kwa maana ya kwamba, mfumo ambao utaziweka hizi nguvu zote nne na kuziruhusu ziweze kufanya kazi kwa ufasaha huwa unakua imara zaidi ya ule mfumo ambao hauziruhusu hizi nguvu ziweze kufanya kazi kwa ufasaha na mfumo ambao ndani yake nguvu zote nne zinatumika na ule mfumo ambao hautumii nguvu zote nne huwa inakua tofauti katika namna ile ya ukuaji wake na kwenye namna ile ya kupokelewa kwao katika dunia au ulimwengu kwa ujumla kwa maana ya kwamba ule mfumo ambao ndani yake nguvu zote nne za asili ya uumbaji zimewekwa na kufanya kazi kwa usahihi huwa unakua na ushawishi mkubwa na kueleweka kwa haraka na watu kuliko ule mfumo ambao ndani yake zile nguvu nne hazijawekwa zote kwasababu unakosa ule muunganiko ulio timilifu na ulimwengu.
Na nguvu nnazo zizungumzia hapa ni zile zile ambazo nimekua nikizisema kwenye maeneo mengi ya kitabu hiki kwa maana ya Maono au uwezo wa kutengeneza mawazo yenye tija, Usaidizi, Maarifa pamoja na Uwezo wa kufanya kazi kwa nguvu bila kujali ugumu wa kazi yenyewe.
Wote tunajua ya kwamba hakuna jambo lolote duniani ambalo limepata kuanzishwa pasipo nguvu ya Maono, kwa maana ya kwamba kabla jambo fulani halijaanzishwa duniani kuwa na hakika ya kwamba alikuwepo mtu ambae alibeba maono ya jambo hilo kichwani au rohoni mwake.
Na ninaposema kichwani au rohoni mwake namaanisha ya kwamba, nguvu hii ya maono inapokuja ndani ya mtu huwa inatokea katika upande mmoja kati ya pande hizi kuu mbili kwa maana ya ule upande wa kiroho au ule wa damu na nyama.
Na hiki ndicho kinachotofautisha baina ya wazo la mtu mmoja na mwingine, mawazo yote mapya kwa maana ya kwamba yale mawazo ambayo hayajawahi kabisa kuwepo duniani yanapomjia mtu huwa yanakuja yakiwa yametokea katika ule upande wa kiroho na watu wanaojiliwa na mawazo ya namna hii ndio wale ambao huitwa watu wenye fikra tunduizi na mawazo yote ambayo humjia mtu kwa kuunganisha unganisha mawazo mengine ambayo tayari yapo duniani huwa mawazo haya yanatokea kwenye ule upande wa damu na nyama.
Sasa watu wengi wenye hizi nguvu za kutengeneza mawazo yenye tija au maono huwa waliowengi wanakua hawajiamini juu ya yale mawazo yaliyo wajiria na ndio maana ili waweze kuamini kwenye mawazo yao au maono yao basi wanahitaji kupata watu au mtu mwenye nguvu ya Usaidizi atasema hili ni wazo zuri na linawezekana kufanyika na endapo litafanyika litakua ni kitu kikubwa sana, lakini pia awe mtu ambae atakua na imani juu ya wazo lililopo na awe tayari kulisimamia kimawazo hadi pale litakapokamilika.
Lakini pia watu hawa wote wawili yaani mwenye maono na msaidizi wake huwa mara nyingi wanakua hawana uwezo wa kuyatafsiri mawazo hayo ili yawe katika mtindo wa kidunia au ule mtindo unaotakikana kwaajiri ya matumizi ya hapa duniani na ndio maana kuna nguvu ya Maarifa.
Ukisoma maandiko utakutana na ile hadithi ya mtu mmoja anaitwa Yusufu, huyu mtu alipata kufungwa gerezani kwa kosa ambalo hakulitenda ila kilichokuja kumtoa gerezani ni nguvu ya maarifa ambayo ilikuwako ndani mwake kwa maana baada ya mfalume kuota ndoto au kwa lugha nyingine unaweza kusema kwamba mfalume aliona maono ambayo hakuweza kuyatafsiri yawe katika ile hali ya kidunia, baada ya watu wengi wenye maarifa kushindwa lile zoezi la kuisema na kuitolea uchambuzi ile ndoto au maono ndipo nafasi ya Yusufu ilipoonekana na yeye aliisema na akaitafsiri na kuiweka katika mtindo wa kidunia na baada ya hapo zoezi la kuifanya ile tafsiri ili iweze kuwa kwenye uhalisia ikaanza kwa kuwatafuta watu wenye nguvu ya kufanya kazi kwa bidii bila kujali ugumu wa kazi na wakajenga maghala ya kuhifadhia chakula nchi nzima na kuanza kuvuna vyakula mashambani na kuvibeba kwenda kuvihifadhi kwenye maghala hayo chini ya usimamizi wake Yusufu labda pamoja na wengine ambao hawakutajwa kwenye maandiko.
Najua kuna watu pengine mnajiuliza ni nini hasa kazi ya nguvu ya Maarifa? kazi ya nguvu hii ya maarifa ni kutafsiri yale maono au mawazo yote yanayowajilia watu kichwani au rohoni mwao na kuyaweka katika ule mtindo wa kidunia kwaajiri ya matumizi.
Na watu hawa wenye nguvu hizi za Maarifa huwa wakishamaliza kuyatafsiri mawazo au maono ya mtu fulani huwa hawana uwezo wa kutenda kazi hasa zile ambazo si zakitaalam ila zile ambazo zinahitaji nguvu na ndio maana ili mambo yaweze kwenda vizuri basi nguvu ya kutenda kazi kwa nguvu pasi na kujali ugumu wa kazi inapotambulishwa na kazi itafanywa hadi pale wazo litakapokua katika uhalisia wake.
Sasa huu ni mfano rasharasha ambao mimi nimekutolea hapo juu ila kwa namna hiyo ndivyo ambavyo mfumo wowote huanza na kuendeshwa kwahiyo ili uweze kupata vizuri nenda kakae katika hali ya utulivu ufikirie vizuri na utapata kuelewa ya kwamba hata biashara zote ambazo zinafanikiwa au zimefanikiwa huwa zinaendeshwa katika mtindo wa kimfumo.
Mafano mzuri ni jamiiforum, ni kwamba kwanza ilianza kama wazo au maono ndani ya kichwa cha mtu, kisha akapata watu au mtu wa kulisapoti wazo kwa kulikubali na kwenda na mwenye wazo bega kwa bega na baada ya hapo waliweza kumtafuta mtu ambae anaouwezo wa kulitafsiri wazo kuwa katika uhalisia wake na baada ya kutafsiriwa basi watenda kazi au vitendea kazi vilitafutwa na kazi ikafanywa hadi wazo au maono kuwa katika uhalisia wake, sasa mfano huu ni katika upande wa bidhaa.
Lakini pia nikupe mfano wa huduma kama vile dini, wote tunajua uislam ulianzia mapangoni ya kwamba muasisi wa dini hii wakati yupo kwenye tabia yake ya kawaida ya kukaa katika hali ya utulivu wa akili ndipo akajiwa na maono kwa namna ile ambavyo yalikuja na baada ya kupata maono hayo alitoka moja kwa moja na kwenda kumshirikisha mkewe na hii inawezekana hakuwa na uhakika juu ya yale maono yake yaliyo mjilia kwa wakati ule lakini alipopata usaidizi kutoka kwa mkewe basi akatafutwa mtu mwenye uwezo wa kutafsiri namna inavyo paswa kufanyika ili maono yawe katika uhalisia, na alipopatikana basi nae akatafsiri kisha watu hodari katika kufanya kazi bila kujali ugumu wa kazi yenyewe wakatafutwa na kazi ikapigwa na maono yakatimia kwa maana huduma iliweza kufika duniani kote kama vile ilivyotakiwa.
Sasa kikawaida kuweza kuligeuza wazo na kuwa katika uhalisia wake ni jambo moja lakini jambo la pili ni kuweza kulifanya wazo lililokamilika liweze kupata muunganiko na ulimwengu.
Ili uweze kuunganisha ile bidhaa au huduma iliyokamilika na ulimwengu basi lazima urudie mchakato ule ule kwa maana ya kwamba utatakiwa uwe na watu wenye maono au mawazo ya kwa namna gani matangazo yafanyike na mawazo yakishawekwa mezani lazima wapatikane watu wenye uwezo wa kutafsiri mawazo hayo na wakishafanikiwa kuyatafsiri basi wawepo watu ambao watapokelezana usiku na mchana kwenye kufanya kazi juu ya mawazo yaliyotafsiriwa kwaajiri ya kuiunganisha bidhaa au huduma yako na ulimwengu.
Na mapokezi ya bidhaa au huduma katika ulimwengu unaoiunganisha nayo huwa inategemeana sana na usahihi katika namna nguvu zote nne zinavyotumika katika upande huo wa matangazo kwa maana ya kwamba nguvu yoyote inapopungua na ufanisi nao hupungua, hii ni siri ambayo waajiri wazuri wote duniani kwenye makampuni mbalimbali huwa wanaitumia na hata wale ambao huwa wanafanya utafiti wa kwanini kampuni imelega kwenye mwaka fulani ukilinganisha na miaka mingine huwa wanacheza kwenye nguvu hizi nne iwe kwa kujua au kwa kutokujua, kwahiyo na wewe usipate tabu, biashara yako ikilega angalia nguvu gani kati ya hizi nne haujaiweka kwa usahihi na ukishapata jibu na ukamtafuta mtu sahihi mwenye uwezo wa kuiongeza nguvu hiyo utaona matokeo moja kwa moja.
Sasa kabla sijamaliza hiki kipengele nataka nikuambie namna ambavyo biashara zote ambazo zinafanywa katika mtindo wa kimfumo zinavyofanya kazi…
Biashara zinazofanyika katika mtindo wa kimfumo huwa zinafanyika katika namna kuu mbili, ya kwanza huwa ni biashara inaanzishwa halafu nguvu zote nne zinawekwa na bidhaa au huduma inatokea halafu inapelekwa kwa jamii kwaajiri ya kusaidia changamoto fulani ambayo mwenye wazo aliiona.
Na biashara za mtindo huu huwa zinapokwenda kwa jamii kama ni bidhaa basi inakua haifichi nguvu yoyote kwa mnunuaji kwa maana kwamba kama mnunuaji anataka afanye biashara kupitia bidhaa hiyo basi atakua uwezo wa kufanya na akitaka awe mfanya kazi kupitia bidhaa hiyo pia atakua.
Kwa mfano kiwanda kinachofanya biashara ya kuzalisha mabegi mbalimbali, ndani yake kuna mfumo unaosaidia kazi iweze kufanyika ila bidhaa ikishakamilika na kuingia mtaani jukumu la kuitengenezea mfumo au kutokuitengenezea linabaki kwa mnunuaji. Na ndio maana kwenye biashara hizi hizi za mabegi utakuta kuna watu wananunua mabegi ya kutosha kutoka kiwandani na wao wanafungua duka lao na kutengeneza mfumo ndani yake kwa maana mwenye duka atakua ndio yule mwenye nguvu ya maono lakini pia atakua na wafanya kazi wanaotokea kwenye ile nguvu ya maarifa pamoja na ile ya kufanya kazi kwa nguvu au bidii pasipo kujali ugumu wa kazi kwa maana ya kwamba wapo ambao watasaidia kuuza duka ila pia wapo ambao watasaidia kuchukua mizigo kule gharani na kuleta dukani ila pia wapo ambao watachukua mizigo gharani na kupeleka mnadani lakini pia wapo watu wenye maarifa ya kuitangaza biashara na hawa watu wote wanaounda nguvu nne za asili ya uumbaji wa ulimwengu ndani ya duka hili huwa hawawezi kufanya kazi kwa kufuata ratiba bila ya kuwa na msimamizi na huyu msimamizi ndio yule mwenye nguvu ya usaidizi.
Lakini kwenye uuzaji wa mabegi haya haya wapo watu ambao wao kazi yao ni kuchukua hayo mabegi na kuyabeba kuanza kuyatembeza mtaani.
Kati ya hao watu wawili kwa maana mwenye duka na mwenye kutembeza mtaani ni kwamba wote wanauza mabegi lakini mmoja ni mfanya biashara na mwingine ni mtu aliyejitengenezea kazi yake yeye mwenyewe. Mfanya biashara ni yule mwenye duka kwa maana nguvu zote nne ameziweka ndani ya biashara yake ila mfanya kazi ni yule anaetembeza kwa maana ni nguvu moja tu ya kufanya kazi kwa bidii ndio ambayo anaitumia yeye na ndio maana bidii yake ya kutembea ikipungua basi hatoweza kuuza ila mwenye duka nguvu ya maarifa ya wale watu wa matangazo ikipungua basi itapelekea mauzo nayo yashuke au nguvu ya usimamizi ikipungua pia mauzo yatashuka na hata ile nguvu ya kufanya kazi kwa bidii ikipungua nayo mauzo yatashuka kwa maana biashara yake inawatu ambao wanafanya kazi kwa kutegemeana ingawa walio wengi huwa hawaijui mbinu hii ila wao huwa wanafanya tu kazi au wanaajiri vile ambavyo wanajiskia.
Sasa ukiwa na biashara au kampuni na ukashindwa kujua namna sahihi ya kuajiri basi kaa ukijua kampuni au biashara yako haitoweza kupiga hatua kwa maana wapo watu ambao huajiri watu wenye nguvu moja katika maeneo yote na kudhani ndivyo ipasavyo kuwa, kwa namna hii hutoweza kufikia malengo kwa hiyo kabla hujaanza kuajiri unatakiwa ukae chini kwanza uanze kuandika au kutengeneza mfumo ambao utakuwepo kwenye kampuni au biashara yako na ukishatengeneza unatakiwa uanze kuwaajiri watu bora kwenye kila nguvu katika zile nguvu nne.
Lakini ukiangalia mfano huo wa mabegi nimeutolea kwenye upande wa bidhaa ila katika upande wa huduma kwenye upande huu wa namna ya kwanza ni kwamba watu hawa au mtu huyu mwenye huduma yake baada ya kuweka mfumo wake wa ndani na kuusimamia vizuri na hatimae kutengeneza huduma ambayo ipo tayari kwenda kwa jamii huwa inavyokwenda kwa jamii lengo kubwa ni kuongeza maarifa ndani ya vichwa vya wateja au kuongeza maarifa yaliyo pungua kwenye biashara za wateja, lakini pia biashara hizi za huduma huwa zinaanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watu au jamii katika maeneo kadha wa kadha ikiwemo lile eneo la afya.
Kwenye kuongeza maarifa kwenye kichwa cha mlengwa ni kwamba hii hufanyika kwa njia ya makongamano kama vile ambavyo tunaona hawa watu wanaoanzisha makongamano na wao wakiwa wanaongea mada mbalimbali iwe za kifedha au za kiroho ila lengo kubwa ni kuhamisha maarifa kutoka kwenye vichwa vyao na kuyapeleka kwenye vichwa vya wateja wao ila pia wakati mwingine ukiachana na makongamano huwa watu hawa wanafungua mashule huku lengo likiwa ni moja.
Na utofauti wake ni kwamba mtu anaesimama mbele za watu katika makongamano mbalimbali na kuanza kuongea yeye huwa ni mfanya kazi ila anaeamua kufungua shule yeye huwa ni mfanya biashara kwa maana ya kwamba anamiliki mfumo ambao yeye anaweza kuuendesha kwa namna ile anataka na haumtegemei yeye ili fedha iweze kupatikana ila inategemea nguvu nne ambazo huwekwa na watu ambao atawaajiri.
Lakini pia nimesema hapo juu ya kwamba katika biashara hizi hizi za huduma ukiachana na zenye kuhamisha maarifa kutoka kwenye kichwa cha mtu na kwenda kwenye kichwa cha mwingine pia kuna ile ya kuongeza maarifa yaliyo pungua kwenye biashara za watu wengine na biashara za mtindo huu ndio zile agency mbalimbali ambazo huwa zinaanzishwa kama vile za matangazo ambazo lengo lake kubwa ni kuwasaidia wale wenye biashara mbalimbali ambao nguvu ya maarifa katika upande wa kutangaza biashara zao imepungua na kadhalika.
Na namna ya pili ya biashara zinazofanyika kwenye mfumo ni kwamba biashara inaanzishwa na nguvu nne huwekwa ndani yake na kutengeneza bidhaa yenye upungufu wa nguvu moja au mbili na kumtaka mlengwa kwa maana ya mteja aweze kuijaza au kuzijaza nguvu hizo ili aweze kufaidika kwa maana ya kupata fedha au heshima fulani au burudiko la moyo wake na biashara za namna hii huwa nyingi zinatokea kwenye upande wa mifumo ya kompyuta.
Na mfano mzuri wa biashara za namna hii ni jamiiforum, hii imetengenezwa kimfumo na ndani yake nafasi ya nguvu mbili ya maarifa na ile ya mawazo au maono ikaachwa wazi kwaajiri ya kuwaachia watumiaji waweze kuzijaza nafasi hizo na ndio maana utaona ndani ya huu mfumo watu huja na mambo mbalimbali ya kuongeza maarifa na mambo hayo huwa ni maono yao binafsi au ni maarifa ambayo na wao waliyatoa katika sehemu fulani iwe kwenye vitabu, kwa kuona au kusimuliwa.
Na mfano mwingine wa biashara ambayo inafanywa kwa mtindo wa kuacha nguvu moja au mbili za asili ambazo watumiaji watalazimika waijaze ni YouTube, hii yenyewe nguvu ya usaidizi na maarifa ndio zimeachwa wazi na mtumiaji akitaka aweze kuwa mmoja ya washiriki basi anatakiwa awe na maarifa ya kuongeza kwa watu na hapo hapo atatumika kama msaidizi kwa maana maarifa yake yatatumiwa na wenye mfumo kuwekea matangazo yao ili yawafikie watu wanaopata maarifa kwa huyo mwenye maarifa kwahiyo yeye atawasaidia wenye mfumo waweke matangazo yao kwenye maarifa yake aliyoyatoa.
Lakini pia kuna mifumo ya network marketing, kwenye mifumo hii nguvu ya asili ambayo imeachwa wazi ndani yake ni ile ya uwezo wa kufanya kazi kwa nguvu na bidii bila kujali ugumu wa kazi, kwahiyo ili uweze kufanikiwa humu kwenye kazi za namna hii ni lazima utumie nguvu kidogo kwa maana ya kuzunguka huku na huku kutafuta watu ambao watajiunga ili nawewe ufaidike kupitia wao.
Na mfumo mwingine ni mfumo wa trading kwa maana ya metatrade 4 au 5 au wowote ule ambao watu wa forex huwa wanautumia kwaajiri ya kusoma charts kwa lengo la uchambuzi wa soko, sasa mfumo huu nao nguvu ambayo imeachwa wazi ni nguvu ya maarifa kwa maana ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe na maarifa sahihi ambayo yatakusaidia kwenye uchambuzi wa soko ili uweze kujua wapi ununue wapi uuze na wapi uwe nje ya soko.
Mfumo mwingine ambao nitautolea mfano hapa ni mfumo wa michezo ya bahati na sibu kwa maana ya betting, sasa katika mfumo huu nguvu ambayo imeachwa wazi ili iweze kujazwa na wateja Au wafanya biashara ni nguvu ya maono kwa maana ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe na uwezo mzuri wa kuona namna mambo ya mbele yatakavyo kuwa kwa maana ya kubashiri.
Ukisoma vizuri hapo juu kwenye hiyo mifumo mbalimbali niliyoweza kuielezea ni kwamba nimeelezea ile mifumo ambayo haimpi nafasi mtu anaetaka kuwa sehemu ya mfumo kuongeza nguvu zote nne na usidhani mifumo inayomtaka mteja aongeze nguvu zote nne haipo, hapana mifumo ya namna hiyo ipo na mfano mzuri ni Amazon.
Amazon ni mfumo ambao watu huutumia kuuza bidhaa zao mbalimbali kwa njia ya mtandao, na mfumo huu namna unavyofanya kazi ni kwamba mtu anaetaka awe sehemu ya mfumo anajisajiri na kufungua duka lake ndani ya mfumo na baada ya kufungua duka basi ataruhusiwa kuweka bidhaa zake huko na zinapokutana na mtu au watu wenye kuzihitaji basi watazinunua na muuzaji kuweza kupata pesa yake kupitia utaratibu maalumu uliowekwa.
Kwenye mfumo huu wanaofanikiwa ni wale watu ambao hutengeneza mfumo ndani ya mfumo kwa maana ya kwamba pindi wanapofungua maduka yao na wao uhakikisha wanaweka nguvu zote nne ndani ya hiyo biashara ili waweze kuiunganisha na mfumo ili mfumo uweze kuziunganisha biashara zao na ulimwengu.
Katika mfumo huu wale wote ambao wanaingia kwa lengo la kufanya kazi huwa hawafanikiwi na watashangaa ni kwa namna gani watu wengine wanapata pesa au wanauza bidhaa zao kupitia mfumo huu kwa maana mfumo unawalazimisha watu watengeneze mifumo yao ili wafanikiwe.
Ndio maana huwa ni kazi sana kufanikiwa na kuwa mfanya biashara mkubwa ndani ya mfumo huu wa amazon kwa maana ni mfumo ambao unamtaka muuzaji afuate taratibu zote za biashara kwa maana ya kuweka nguvu zote nne za asili ya uumbaji wa ulimwengu ili biashara yako iweze kupata muunganiko na mfumo wao kabla mfumo wao haujaiunganisha hiyo biashara yako na ulimwengu.
Kwahiyo ipo mifumo ambayo imetengenezwa kwa lengo la kumlazimisha mtu awe mfanya kazi lakini pia ipo mifumo ambayo imetengenezwa kwa lengo la kumlazimisha mtu awe mfanya biashara.
Na ukitaka uijue tofauti ya haraka kati ya mfumo na mfumo angalia namna ambavyo tangu unajisajiri katika mfumo huo hadi kuingia sokoni yaani kuanza kufanya hiko unachotakiwa ukifanye ili upate pesa inachukua muda gani.
Kwa maana kuna mifumo ambayo haichukui hata dakika tano mtu kuingia sokoni tangu alipojisajiri na kupata hiyo nafasi ndani ya mfumo ila kuna mifumo ambayo inachukua muda mrefu sana kumfanya mtu aingie sokoni kwa maana ya kuanza kupata faida kutoka pale alipojisajiri.
Kwa mfano angalia ile mifumo ya tax mtandao ni kwamba ukishajisajiri na wakakupatia nafasi ndani ya mfumo wao basi hapo hapo unaouwezo wa kuanza kufanya kazi kwa maana mfumo huu huwa unamtaka mtu ajaze ile nafasi ya nguvu ya kufanya kazi kwa bidii kwa maana mtindo wake ni wakutumwa yaani mwenye gari anatumwa na wenye mfumo kwamba nenda sehemu fulani kachukue abiria, sehemu fulani kuna abiria, sasa uwezo wako wa kupata pesa unategemeana na bidii yako au uchapa kazi wako bila kujali ugumu unaoupata.
Ila mfano huo huo ukiupeleka kwenye mfumo kama amazon utagundua ya kwamba licha ya kupewa nafasi ya duka kwenye mfumo na wewe kuweka bidhaa zako lakini hakutakua na namna utapata pesa bila ya kutengeneza mfumo ambao utaiunganisha biashara yako na mfumo huo wa amazon ili wateja wako wanapoingia kwenye huo mfumo wa amazon waweze kukutana na hizo bidhaa zako, kwahiyo kama utashindwa kufanya hivyo basi bidhaa zako zinaweza kukaa hata mwaka mzima pale kwenye duka lako bila kupata mteja wakuzinunua.
Kwahiyo mfumo wenye mlengo wa kukufanya wewe kuwa mfanya kazi huwa hauhitaji muda wa wewe kuanza kazi tangu pale ulipojiunga na mfumo huo ila mfumo wenye mlengo wa kukufanya wewe kuwa mfanya biashara huwa unahitaji muda wa kutosha tangu ulipojiunga na mfumo hadi kuanza kupata pesa.
Na kawaida ya mifumo yenye mlengo wa kumfanya mtu awe mfanya kazi huwa inamuhitaji mtu awekeze muda wa kutosha ndani yake ili aweze kupata fedha ila mifumo yenye mlengo wa kukufanya uwe mfanya biashara huwa inahitaji uwekeze muda wa kutosha wakati unapoanza kutengeneza mfumo wako binafsi ndani ya mfumo na ukishafanikiwa kutengeneza mfumo huo basi utakuacha huru na utakua na muda mwingi wa kufanya mambo yako mengine huku pesa zikiwa zinaingia kama kawaida.
Kwahiyo biashara yoyote ambayo inaweza ikampatia mtu faida inayoeleweka na kumpa mtu uhuru wa muda ni lazima angalau iwe na nafasi ya nguvu mbili ambazo mfanya biashara anatakiwa azijaze ili apate pesa ila ikitokea biashara ikawa inamuhitaji mtu aweze kuweka nguvu moja kati ya zile nne basi hiyo ni kazi sio biashara na kazi ili uweze kupata pesa inakuhitaji uwekeze muda mwingi sana ndani yake ili pesa iweze kupatikana.
Mfano mzuri ni youtuber na mtu wa trading, ni kwamba youtuber haitaji muda mwingi wa kila siku ili aweze kupata fedha pindi anapokua tayari ameshajitengenezea mfumo wake ndani ya mfumo wa YouTube ila mtu wa trading anatakiwa awe na muda kila siku ili aweze kupata fedha, kwasababu youtuber ameachiwa nguvu zaidi ya mbili za usaidizi pamoja na ya maarifa na kuna wakati inaweza kwenda hadi kwenye nguvu tatu hadi nne kwa maana na ile ya maono pamoja na ya kujituma au kufanya kazi kwa bidii wakati unapoanza kutengeneza mfumo wako ndani ya mfumo wa YouTube huwa zinahitajika ndani yake kuweza kuingia ila mtu wa trading ameachiwa nguvu moja ya maarifa na zingine zote zimezibwa na mwenye mfumo kwahiyo hawezi kutengeneza mfumo ndani ya mfumo na ndio maana ni ngumu sana kwa yeye kuwa huru isipokua anahitajika kila wakati aweze kuwekeza muda wake ili aweke hiyo nguvu ya maarifa kwaajiri ya kupata fedha.
Na ndio maana ukiona mfumo wowote ambao umeziba nguvu tatu na kukuachia wazi nguvu moja ili wewe uijaze upate pesa kuwa nao makini kwa maana haukuchukulii wewe kama mfanya biashara ila unakuchukulia wewe kama mfanya kazi, sasa mfanya kazi mzuri ni yule ambae ataajiriwa na kulipwa mshahara kila mwezi kinyume chake atahangaika sana ili aweze kufikia angalau robo ya malengo yake.
Kwahiyo mtu ili uweze kufanikiwa kibiashara ni lazima uifanye biashara yako iwe katika mtindo wa kimfumo kinyume chake hauwezi kufika pale ambapo unapataka kwa maana watu wote ambao wamefanikiwa kibiashara huwa wamefanikiwa kuzifanya biashara zao zifanye kazi katika mtindo wa kimfumo iwe kwa kujua au kwakutokujua.
Na ukijiona wewe ni mfanya biashara ila biashara yako haikupi muda wa kufanya mambo mengine kwa maana ya kwamba biashara inakutegemea wewe uwepo ili pesa iweze kupatikana na usipokuwepo pesa haipatikani basi yakupasa ujue ya kwamba ni labda bado hujaitengenezea mfumo au hiyo sio biashara ila ni kazi.
Na ndio maana utaona hiyo mifumo yote ambayo nimeitaja hapo juu watu wanaofaidika sana ni hao wamiliki wa hiyo mifumo yenyewe kwa maana wao ndio wenye mifumo kwahiyo wameweka nguvu zote nne ndani yake huku wakiwalazimisha watu wengine wazitumie kwa kuweka nguvu moja au mbili ili wapate fedha.
Wamiliki wa mifumo kwa maana ya wafanya biashara huwa ndio watu ambao wanastafu mapema kwa maana wakishamaliza kutengeneza mfumo na kuweka taratibu zinazofanya mfumo uweze kujiongoza basi mfumo huo huwa unajiongoza wenyewe kwa kufuata zile taratibu zilizowekwa wakati ule ambao mfumo huo ulikua ukitengenezwa.
Lakini wafanya kazi huwa hawawezi kustafu hadi pale ambapo wataona sasa pesa walizonazo zinatosha na kuamua kuacha hiyo kazi ambayo waliianzisha ili nao wapate muda wa kupumzika lakini sasa katika nyakati hizi huwa pesa haiingii tena kwao ukilinganisha na wale watu wenye biashara.
Ndio maana huwa mara nyingi nasema ya kwamba biashara ni mchakato ambao unahitaji muda hadi kuanza kuleta matunda ila mchakato huo ukishakamilika basi matunda yake huwa yanakua ya daima ila kazi ni rahisi kwa maana inahitaji nguvu au maarifa ili iweze kuanzwa ila matunda yake huwa si ya maisha yote kwa maana mfanya kazi huwa anabadilisha muda wake kwa fedha ila mfanya biashara huwa anabadilisha thamani ya biashara yake kwa fedha.
Kwahiyo ili uweze kulisimika jambo lolote katika hii dunia ni lazima uwe tayari kulifanya katika mtindo wa kimfumo ila ikitokea ukalifanya kinyume chake basi hii itahesabika ya kwamba wewe ni mbinafsi na mtu ukishakua mbinafsi huwa ni ngumu sana kupata uwezo mkubwa wa kumiliki fedha au kama utapata uwezo wa kumiliki fedha basi muda hautakua nao wa kutosha wa kuzifurahia hizo fedha unazozimiliki pamoja na familia yako au watu unaowapenda.
Na hapa naomba niliweke hili sawa, ya kwamba lengo la kuandika haya simaanishi kwamba usifanye kazi ila lengo langu nataka ujue kitu kinachokukwamisha kuelekea kwenye maendeleo makubwa ya kifedha au kupata muda wa kutosha wa kufanya mambo mengine.
Pia nataka ujue utofauti uliopo baina yako na yule unaemuita bosi au kwanini biashara moja inayofanywa na watu tofauti utakuta wengine wako na muda wa kutosha lakini wengine hawana muda kabisa au kwanini wengine wanakua sana kibiashara yaani kama ni maduka utakuta wanayafungua kila mkoa ila wengine hawakui kabisa kibiashara.
Sasa tofauti hizi zote huletwa na mambo ya kimfumo. Mfumo unauwezo wa kumfanya muuza matunda akawa na uchumi imara kuliko mwenye kiwanda cha mamilioni ya fedha.
Mfumo hauna kawaida ya kuchagua ukae kwenye biashara iliyoanzishwa kwa mtaji mkubwa kiasi gani ila mfumo unaouwezo wa kukaa hata kwenye biashara ambayo haijaanzishwa kwa mtaji, kitu muhimu na cha kuzingatia wakati unaitengenezea biashara yako mfumo hakikisha hiyo biashara uwezo wake wa kusambaa na kukua ni mkubwa kwa maana iwe biashara ambayo uhitajikaji wake kwa jamii ni mkubwa yaani iwe biashara ambayo inaigusa jamii moja kwa moja.
NITARUDI...