Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Kama mkopo wowote, kama hakuna udhibiti madhubuti, pesa zitakwisha bila kujua zilikokwenda! Na kama mkopo wowote, hiyo miaka arobaini ya grace itapita kama maji.
Kama hujasikia, Tanzania imekopa na kupatiwa mkopo mkubwa zaidi kuwahi kutokea, na Jamhuri ya Korea Kusini. Pamoja na kupewa mkopo huo kamambe, hakuna maelezo mazuri yaliyotolewa na serikali ya kuhesabu shilingi kwa shilingi kujua mkopo huo utatumika vipi. Wengi wetu tumesikia kwa ujumla tu, oooh tutajenga hospitali ya vitanda 600 kule Zanzibar, nyingine zitakwenda kwenye umeme, reli nk. bila ya kuelezea ngapi zitakwenda wapi. Ni kana kwamba mkopo huu ulichukuliwa kwa mhemko tu, baada ya kuona Korea iko tayari. Kutokana na uzoefu, ni dhahiri pesa nyingi 'zitapigwa' halafu Watanzania, sio sisi, bali wana wetu na wajukuu zetu, waachiwe mzigo bila hatia!
Kifupi. Napendekeza matumizi yafuatayo (the nitty-gritty of numbers should be left to Mwigulu or his sister!)
1. Kwa vile mkopo huu ni wa bei nafuu sana, tumieni nusu bilioni $ kulipa mikopo yote mlioichukua kwa bei ghali kwa upumbavu wenu, na ambayo inawaumiza kwa riba zake.
2. Tumieni bilioni 1$ kwa kujenga oil refinary ya aina kama tano za mafuta yakiwemo ya ndege na hata lami
Hii itakuwa na uwezo wa kurudisha kiasi kikubwa cha mkopo kwani mtauza mafuta kwa Congo, Comorro, Madagascar, Zambia, Burundi, Malawi nk.
3. Fungueni shamba la eka milioni 2 la kulima ngano. Huwezi kukosa soko la ngano. Dunia nzima inakula ngano. Shamaba hili liwe la serikali na usimamizi mzuri. Ikibidi walipeni wageni waliendeshe. Msione vibaya kuwatumia wageni kwa sababu za uzalendo wa kipumbavu. Ghuba ya Waarabu, hizo Emirate, Saudia, Kuweit, Qatar zilianza kwa kuwalipa wageni na sasa wanaendesha wenyewe. Kama hujui hujui tu, uwe mwananchi au nguru!Mbona Wagiriki waliweza kuendesha mashamba makubwa ya katani hapa Tanzania hadi wakati fulani Tanzania ilikuwa nambari 1 kwa katani duniani? Shamba hilo litatoa ajira, pia ujuzi wa kilimo, kwa maelfu ya Watanzania. na ifikapo miaka arobaini litakuwa na uwezo mkubwa wa kuchangia kulipa deni.
4. Tumieni kiasi kikubwa kuchimba mabwawa ya maji kiasi kila maili tano pawe na bwawa. Wazungu walipokuja Tanzania walifanya hivi lakini tukashindwa kuya maintain mabwawa hayo. Wazungu si wajinga kufanya hivyo, maji mengi inamaanisha mazingira mazuri na kuzuia ukame.
5. Zilizobaki rukhsa kuzipiga, maana lazima mtafanya hivyo. Ila acheni upuuzi wa kujenga hospitali, shule, masoko kwa hela za mkopo. Vitu ambavyo havirudishi fedha,. Tumieni akili zenu kujenga shule na hospitali zenu kwa vianzo vyenu, acheni uvivu wa akili.
Ahh, nimchoshwa na viongozi wa Tanzania. Hakuna kitu kigeni katika kuleta maendeleo, wala huna haja ya kuunda kipya. Ni kuiga tu walioendelea. Hilo pia ni gumu? Kila siku mwatupiga porojo ugumu ugumu hata wengine twaelekea kaburini bila ya kuonja maisha mazuri? Pumbaaaaaaf