Covid-19 ugonjwa usababishwao na Corona virus hadi sasa hauna tiba wala chanjo. Waliopona ugonjwa huu wamepona si kwa kuwa walikuwa wakitibiwa Covid-19 bali zaidi kwa bahati zao na kudra za mwenyezi Mungu.
Ugonjwa huu unaua. Hata aliyeugua akapona, anaweza kuugua tena na tena, akapona tena au hata akafa. Bahati na kudra za mwenyezi Mungu huwa hazipo kila siku. Wanasema waswahili, "bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi."
Ni kwa sababu ya kutokuwa na tiba kamili ya ugonjwa huu, kwa maelfu ya watu waliokwisha ambukizwa: USA, Italy, Spain , nk, vifo vimekuwa vikiongezeka na vikipindukia hata zaidi ya 900 kwa siku kwa nchi kwa nchi na kwa siku kadhaa mfululizo sasa.
Tatizo kubwa zaidi na ugonjwa huu liko katika kasi yake ya maambukizi ambapo maelfu ya watu wanaweza kuambukizwa katika muda mfupi tu:
1. Mtu aliyeathirika ataambukiza wote anaohusishwa nao hata kwa ukaribu tu.
2. Kila aliyeambukizwa na aliyeathirika, naye ataambukiza wote atakaohusishwa nao hata kwa ukaribu wao tu.
3. Kila aliyeambukizwa, naye ataambukiza wote atakaohusishwa nao pia,hata kwa ukaribu wao tu.
4. Hii ambukizwa ambukiza huendelea hivyo kwa kasi ya mithili ya mlipuko wa bomu.
Kwa vile pia pana suala la hewa linalohusishwa kwenye kuenea au kuambukiza kwake, huu ugonjwa unamuweka kila mtu hatarini.
Ugonjwa huu unaambukizwa na kusambaa kisayansi ambapo njia pekee ya kisayansi ya kuudhibiti, imefahamika kuwa ni katika kupambana kuuvunja mlolongo na mnyororo wake wa maambukizi.
Rejea mada hii kutoka World Economic Forum (WEF) inayoangazia ufumbuzi pekee na kamili ya kuzuia maambukizi ya covid-19:
Why lockdowns can halt the spread of COVID-19
Muhimu kutumia muda kusoma na kuelewa.
Ubinafsi, itikadi, imani, kukurupuka, nk ni muhimu kukuweka pembeni, japo kwa muda.
Total lockdown pamoja na machungu yake ndiyo inayoweza kutuokoa na sisi pia ili kutokuangamia na gonjwa hili lisilo na tiba.
Mbaya zaidi ni kuwa muda wa total lockdown utakuwa mrefu zaidi kama tutachelewa mno kuanza kuitumia.
Kwa hisani (Mwana JF) "remote" katika picha ni uwezekano wa maambukizi ya yule mgonjwa wa kwanza (Tanzania Corona patient zero):
NB: "Akili za kuambiwa changanya na za kwako". Mwisho wa kumnukuu.