Namna pekee ya kuzuia Corona virus kusambaa

Mkuu brazaj , nimefuatilia mabandiko yako, naona una hoja za msingi sana.
Kwa vile serikali yetu imeamua kupuyanga hivyo hivyo, hapa ni kila mtu kuamua hatma yake na familia inayomzunguka.

Jifungie wewe mwenyewe na familia yako ili kutii masharti ya WHO. Hakuna haja ya kusubiri mpaka serikali itangaze zuio la jumla.
Jambo lingine la kuzingatia hapa ni kwamba, serikali inahamasisha watu kutii ushauri wa wataalam wa afya. Hivyo basi, pamoja na serikali kutokutangaza total lockdown... changanya na zako!
 

Mkuu nakushukuru sana Ila ukweli ni kuwa pamoja na tahadhari binafsi haisaidii. Huu ugonjwa siyo kama ukimwi.

Mgonjwa mmoja inakadiriwa kuweza kuambukiza wengine hata 90.

Ugonjwa unakwenda kwenye hewa. Makonda anasema: "mliojifungia ndani tokeni mkafanye kazi, mtakufa njaa!". Mwisho wa kumnukuu. Hao ndiyo kina serikali. Kuna future kweli hapo?

Hatua binafsi zitakuwa na impact ndogo sana kwa hakika.
 
Ingawa una mwandiko mzuri, ni vyema ukapata ushuhuda huu utakusaidia
 

Attachments

  • IMG_2116.MP4
    21 MB
Unachokiombea HAKITAFANIKIWA..
Tanzania tunaendelea vizuri na mapambano.
najua unatamani wagonjwa waongezeke ili uone kane ulitabiri.
na kwambia hivi hapa Tanzania hata wagonjwa 50 hawatafika..
Mkuu kama wewe huna za kwako utachanganya vipi na za wengine?

Kwa vile wewe huna za kwako basi tumia za wengine.

Uko sawa kabisa mkuu tumia za wengine. Hata wakikwambia sasa hivi ni asubuhi wewe ni kuwakubalia tu mkuu, huna namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenya na uganda na South Africa . unajua wana wagonjwa wangapi?.
Na UNA JUA TANZANIA KUNA WAGONJWA WANGAPI?.
Me nmekuelewa mkuu. Watakaopinga kwamba lock down haifai watuambie ni njia zipi zingine zinaweza kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huu?

Na watuambie hizo njia zimetumika nchi gani na matokeo yakawaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
total lockdown kwa ajili ya haka ka ugongwa ka mafua, maleria kwa mwaka inaua watanzania zaidi ya laki , leo kafa mtu mmoja tujifungie ndani, huo ni uwendawazimu
 
Njia.nzuri ya kuvunja mnyonyoro wa hii virus ni kuwashawishi watu wakapime kwa hiyari..

Kumpima mgonjwa wakati tayari ana symptoms ni kupoteza resources kwani inasemekana mgonjwa anaweza kuambukiza wengine kabla hajaonyesha dalili za kuwa na huu ugonjwa..
 
Unachokiombea HAKITAFANIKIWA..
Tanzania tunaendelea vizuri na mapambano.
najua unatamani wagonjwa waongezeke ili uone kane ulitabiri.
na kwambia hivi hapa Tanzania hata wagonjwa 50 hawatafika..

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu niwewe uliyewahi kuandika duni fulani hamuugui huu ugonjwa?

Kwa nini usingejitendea haki kwa kuandika namna ya kuuvunja mnyororo wa maambukizi badala ya kubwabwaja mambo usiyo na uhakika nayo?

Niombee wagonjwa wawe wengi kwani nauza wagonjwa? Kama kuna mashindano ya wagonjwa kuna aliye nao wengi kama USA umeona tunamsifia?

Iliwahi jiulize kweli hiyo yako ni akili au matope?
 
Rwanda ana 102.
Kenya ana 126
Sauzi ana 1585..
Uganda ana 48.
Hawa wote walitumia lock down au wanaendelea kutumia.
LAKINI JIULIZENI WANA PUNGUZA WAGONJWA AU WANAONGEZA?

Sent using Jamii Forums mobile app
Lockdown inazidisha wagonjwa kwa muono wangu..

Theory ya kuwa MIONZI ya jua inapunguza Kasi ya uambukizaji inawezekana kuwa ni kweli
 
Good idea! Mtu akusaidieje ikiwa ulishapuuza aliyokushauri? Rwanda wapo smarter!
 

Huyo atakayekuwa njiani kwenda kupima atakuwa anaambukiza wangapi njiani? Na hao wanaoambukizwa njiani nao wataambukiza wangapi? Na hao ... Na hao .. nk wataambukiza wangapi?

Uwezo huo wa kuwapima tunao? Maabara yenyewe iko moja tu Dar.

Mkuu hili jambo zinahitajika akili iliyotulia.
 
Lockdown inazidisha wagonjwa kwa muono wangu..

Theory ya kuwa MIONZI ya jua inapunguza Kasi ya uambukizaji inawezekana kuwa ni kweli

Hiyo mionzi ya jua iko Tanzania tu? Siyo serikali ya Tanzania imekubaliana kupunguza idadi ya maambukizi kwa maneno tu bila kujali hali halisi? Kama hii ndiyo mionzi yenyewe unayoisema nitakubaliana nawe.

Hivi yule waziri aliyesemekana kuathirika keshaonekana hadharani?

Akili za kuambiwa muhimu kuchanganya na zingine ndiyo maana sikusahau kuweka ile NB.
 
Mpaka.sasa.Tanzania ndio yenye wagonjwa kidogo ukifanananisha na nchi nyengine za East Africa

kwa mantiki hiyo Model ya Tanzania ya kuzuia mamhukizi unafanya kazi
Tanzania wameungana na Japan na Sweden kwa kutumia njia ya Sina moja kuzuia hizi virusi visisambae kwa haraka..
 
total lockdown kwa ajili ya haka ka ugongwa ka mafua, maleria kwa mwaka inaua watanzania zaidi ya laki , leo kafa mtu mmoja tujifungie ndani, huo ni uwendawazimu

Hoja yako mfu!!!!!!..China ugonjwa ulikoanzia walianza na wagonjwa watatu (3), leo ugonjwa umekua Pandemic!..nyie mlio na wagonjwa 20..mnajidai kutembelea vifua mbele!...mnatia huruma
 

Unaonaje uwashauri kabisa wote wasumbukao na mizigo ya corona hasa USA, Italy, Spain, nk pia hata Uganda, Kenya, Rwanda, South Africa nk waachane na matatizo wafuatane na model ya Tanzania?

Ninaamini una maana model ya Tanzania ni kuweka msemaji kama Ummy. Si kuwa na taarifa huru.
 
Hoja yako mfu!!!!!!..China ugonjwa ulikoanzia walianza na wagonjwa watatu (3), leo ugonjwa umekua Pandemic!..nyie mlio na wagonjwa 20..mnajidai kutembelea vifua mbele!...mnatia huruma

Waswahili wanasema wajinga ndiyo waliwao.
 
Model ya Tanzania ni kuwafanya watu waendelea na maisha,..wasifungiwe ndani,kusiwe na Total lockdown,k

Imekuwa proved kuwa nchi zote zilizoweka Quarantine wagonjwa wanaongezeka badala ya kupungu

Sweden na Japan ni mfano mzuri wa kuigwa
 
Model ya Tanzania ni kuwafanya watu waendelea na maisha,..wasifungiwe ndani,kusiwe na Total lockdown,k

Imekuwa proved kuwa nchi zote zilizoweka Quarantine wagonjwa wanaongezeka badala ya kupungu

Sweden na Japan ni mfano mzuri wa kuigwa

Sina hakika kama chapisho la WEF umelisoma. Kila lockdown maambukizi na vifo vitaongezeka kwa muda kabla ya kufika kwenye plateau. Ndipo sasa itaanza kupungua.

China ni moja ya walikofanikiwa kwa lockdown. Chapisho la WEF lina mifano yote. Tatizo tunasema sema tu. Hatusomi kuelewa pamoja na kuwepo alerts zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…