Namna sahihi ya kutafsri majibu ya VVU

Joined
Apr 28, 2017
Posts
30
Reaction score
73
Vipimo vinavyotumika mara nyingi sana kupima HIV/VVU ni aina ya HIV antibody tests, changamoto ya vipimo hivi ni kuwa kinahitaji mtu awe amepata maambukizi angalau miezi mitatu nyuma kabla ya kupima ili kipimo hiki kiweze kumgundua mtu kuwa ana maambukizi ya HIV/VVU.

Ndo maana ukipima katika vituo vya kutolea huduma za afya na majibu yakawa negative unashauriwa kupima tena baada ya miezi mitatu, wale wanaopima hapo hapo na mtu wake majibu yakawa negative na kuamua kwemda kavu kavu kuna risk kubwa tu.

Kipindi hiki ambacho kipimo hakijaweza kugundua kuwa mtu ana maambukizi ya HIV/VVU ndo kipindi mtu mwenye maambukizi mapya ya HIV/VVU anakuwa na uwezo wa kuambukiza HIV/VVU kwa kiasi kikubwa sana highly infectious period. Take home message ni kuwa ukimpima mtu kwa mara ya kwanza akawa negative pima tena baada ya miezi mitatu kuhakiki hali yake ya maambukizi ya HIV/VVU, pili tuendelee kutumia kinga mara zote na kuwa waaminifu kwa wenza wetu.
 
Niulize swali?
Mfano mtu anajulikana ana HIV/1 Na akaanza dawa je lakini bado anajihusisha vulnerable risk behaviour...na dawa hatumii vyema akapata HIV/2 haya nayo ni maambukizi mapya?
 
Upime mchuchu hana vijidudu kisha umsubiri miezi mitatu kujiridhisha?
Wakati huo naendelea Kula ela zako tu.
Mara Kodi ya nyumba, mara Sina vocha, sijala, Mama Anaumwa nataka nauli niende kumwona.
Ikifika miez mitatu kupima Tena mara ya pili huoni Ng'oo.πŸ˜πŸ˜€πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜
 
Take home message ni kuwa ukimpima mtu kwa mara ya kwanza akawa negative pima tena baada ya miezi mitatu kuhakiki hali yake ya maambukizi ya HIV/VVU, pili tuendelee kutumia kinga mara zote na kuwa waaminifu kwa wenza wetu.
Mkuu tatizo linakuja hivi; mtu amepima day 1 anasoma -ve, ikifika day 89 anachepuka anachota vidudu, day 90 mnakwenda kupima atasoma 0, shida iko palepale
 
Ukimwi ulikuwa zamani.
Pima,ukikutwa nao Anza dawa, utajiweka salama 95% au zaidi, ukitumia dawa ipasavyo unawalinda Kwa 95% ya wasiokuwa nao endapo utakutana nao......test and start dose ndio suluhu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…