DENIS FRANCIS ELISHA
Member
- Aug 26, 2022
- 9
- 3
UTANGULIZI
Sekta ya afya ni sekta yenye wadau na wahitaji wengi lakini bado imeonekana kutokuwa na tija katika maendeleo ya taifa na watu wake kwa ujumla Ili hali watumiaji na wahitaji ni wengi.
Hii inatokana na kutokuwa na mipango mizuri na madhubuti katika sekta hii muhimu. Kwa kuliona na kulitambua hilo mimi binafsi nimekuja na mawazo ambayo yaweza kuleta tija kama yakifanyiwa kazi.
Sekta ya afya ni sekta muhimu sana yenye kuweza kuwa na mchango mkubwa sana katika nyanja za ajira, uchumi, na maendeleo ya taifa kwa ujumla kwa kufanya yafuatayo:-
Kwanza: Kuandaa wataalamu wa kutosha wenye taalumana uwezo wa kutosha kufanya kazi katika sekta ya afya wakiwemo Matabibu, Wafamasia, Manesi na Wakunga, Watu wa mipango na Utawala katika sekta ya afya.
Hatua hii iende sambamba na ujenzi wa miundo mbinu ya kutosha kutolea huduma za afya yaani za kitabibu na nje ya kitabibu mfano kuwe na maeneo katika hospitali zetu hasa za Kanda, Rufaa na Mikoa zenye miundo mbinu kwaajiri ya viwanda vidogo na vya kati kwaajiri ya uzarishaji wa vifaa tiba na vitendanishi mfano hewa ya Oksijeni, maji ya kuwaongezea wagonjwa ( Intravenous fruid ) kama ambavyo tumekuwa tukiona baadhi ya hospital hapa ndani zimeekuwa zikifa hivyo mfano Muhimbili, Bugando Mwanza na kwingineko.
Pili: Kwakuwa tuna hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa serikali ufanye utekelezaji kwa kutumia maeneo yaliyopo katika hospitali hizo jambo ambalo haliwezi kuwa gumu kiutekelezaji na usimamizi kutokana na hali halisi ya mazingira.
Na kwa kuanza tunaweza kuanza kwa kufanya uzarishaji wa vifaa tiba, na vitendanishi muhimu na rahisi kuzalisha mfano gesi ya Oksijeni, maji ya kuongezea wagonjwa, baadhi ya dawa zikiwemo dawa za maji (syrup), dawa za kuoshea vidonda, vitanda na samani zinazotumika mahospitalini, n.k.
Tatu: Tukishakuwa na wataalamu wa kutosha, miundombinu itakayowezesha kuaanza kwa utekelezaji wa mpango wetu wa uzalishaji vifaa tiba, vitendanishi na madawa katika viwanda vyetu vidogo ndani ya hospitali zetu tayari sasa tunaingia katika utekelezaji.
Nne: Baada ya kuanza utekelezaji tunajiwekea malengo kuwa baada ya muda fulani tunataka tuwe tumeshafikia kiwango fulani cha uzalishaji na kwa uaminifu baada ya muda huo tunajitathmini kama kweli malengo tuliyojiwekea yamefikiwa.
Endapo tukijidhatiti tukawa waaminifu tukaacha ubinafsi tukaweka maslahi ya taifa mbele nina uhakika mafanikio yanaweza kuwa makubwa tena zaidi ya matarajio tuliyokuwa nayo mwanzoni mwa mradi na kutufanya kuanza sasa kufikiria kupanua wigo wa bidhaa zetu kuzipeleka katika masoko ya nje ambako kuna faida kubwa zaidi ya zile tunazozipata hapa ndani japokuwa na zenyewe ni kubwa pia.
Tano: Hii ni nyongeza ambayo ipo nje ya mfumo wa viwanda vidogo mahospitalini lakini inaweza kuleta ajira, afueni katika kupunguza gharama za matibabu na kukuza uchumi pia.
Hapa ntazungumzia kidogo kuhusu serikali kuanzisha mfumo rasmi wa utoaji vibari kwa vikundi vya watu kutoa huduma za afya kwa kutembelea zaidi maeneo yenye uhitaji wa huduma hizo mfano vijiji namaanisha huduma za afya zinazotembea ( Mobile Health Services) ambavyo kwenye muongozo wa Wizara ya afya Kuna hiki kipengere.
Ili kuleta tija serikali inaweza kuusajiri vikundi vinavyojumuisha Matabibu, Wafamasia, Manesi na Wakunga, Wataalamu wa Maabara wenye sifa za kutoa huduma hii wakapewa usajiri na vibari vya kufanya huduma.
Hii itafanya kwanza kuongeza fursa za ajira binafsi pili upatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi hasa katika maeneo yasiyofikika na kwa gharama nafuu.
FAIDA ZINAZOWEZA KUPATIKANA KATIKA MRADI HUU.
Moja: Ajira kwa vijana wetu wenye taaluma mbalimbali hasa katika kada ya afya ambao ndo watakuwa wafanyakazi na watendaji wakuu katika mradi wetu huu hivyo kuondoa wimbi kubwa la watu wasiokuwa na ajira pia kuwa chanzo cha uchumi katika familia na jamii za watu.
Kwa mfano tuna zaidi ya Mikoa 25 yenye hospital za Mikoa, na zaidi ya hospitali za Kanda 5 tusema Kila hospitali iwe na kiwanda kimoja kitakacho ajiri wataalamu 100 ni zaidi ya wataalamu 3000 wataajiriwa katika viwanda hivyo na kupunguza wimbi la wasomi ambao hawana ajira tukiachana na watakao ajiriwa moja kwa moja katika viwanda Kuna wale watapata ajira zisizo za moja kwa moja mfano wauzaji na wazalishaji wa Mali ghafi, wasafirishaji, watu wa chakula na vinywaji watafanya biashara hivyo kufanya uchumi kusambaa kwa watu wengi zaidi.
Pili: Kukua kwa uchumi na kuongezeka kwa pato la taifa hii ni kutokana na mapato yatokanayo na kodi pia mauzo ya bidhaa zitakazozalishwa katika viwanda vyetu.
Tatu: Kuokoa fedha nyingi tunazozitumia katika kuagiza vifaa tiba, vitendanishi na baadhi ya dawa tunazoweza kuzalisha wenyewe.
Nne: Kutakuwa na afueni katika gharama za matibabu kutokana na baadhi ya bidhaa zinazofanya matibabu yawe ghari zitakuwa zikizalishwa hapa hapa nyumbani Tanzania pia kunafungu litakalokuwa likitolewa kama ruzuku Ili kugharamia sehemu ya gharama za matibabu pia kuboresha miundombinu ya kutokea huduma za afya katika maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi hivyo kufanya huduma za afya kupatikana kwa unafuu.
MWISHO
Ni Imani yangu kubwa kuwa hakuna kisichowezekana endapo Kila mtu kwa nafasi yake atatimiza wajibu wake kwa maslahi mapana ya jamii zetu na taifa letu kwa ujumla kuliko kutimiza maslahi binafsi hasa tukiangalia kwa mtizamo wa kutaka kuacha alama ya kukumbukwa katika jamii zetu Kila kitu kinawezekana.
Ahsante!

Upvote
3