Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 14,762
- 32,386
Wanavuka lengo ee? Mwishoe hakuna makusanyo kabisa.Anahujumiwa vipi ilihali kila siku anawasifia wanavuka lengo la ukusanyaji?, usidhani hajui yanayoendelea yeye na serikali yake wamebariki haya yanayoendelea.
Wavuke tu hakuna namnaWanavuka lengo ee??? Mwishoe hakuna makusanyo kabisa
UVCCM wao wanapiga domo tu LumumbaBavicha chapeni kazi!
... shamba boy kaingia zizini kama ilivyo kawaida kukamua. Badala ya kukuletea maziwa, katoka humo na damu ndoo mbili na wewe unamsifu! Utakuwa mtu wa ajabu kweli.Anahujumiwa vipi ilihali kila siku anawasifia wanavuka lengo la ukusanyaji?, usidhani hajui yanayoendelea yeye na serikali yake wamebariki haya yanayoendelea.
Amin Amin nakuambia... Mara ya tano wataanza kujikusanya wao wenyewe. . . maana watajikuta wenyewe tu eneo la kukusanyia... hivo ili wamfurahushe mzee baba itabidi waanze kupelekana wao kwa wao.4. Mara ya NNE sasa wanakuja KUTUKUSANYA SISI. Ole wetu sisi. Ole wetu. Ingetufaa zaidi tufungwe jiwe la kusagia na kutupwa bahari
Inatisha kiasi kwamba tunaogopa kuanzisha biashara maana ukianzisha tu tayari unafuatwa ni mgogoro nao kodi kodi.Nilishandika humu kuwa Rais aliwahi kuwapiga siasa wafanyabiashara katika kikao cha nje, baada ya muda mfupi akawa na kikao cha ndani na wakuu wa TRA, alichowaambia ndani ni kuwa “Mimi ninachotaka ni kodi” (kwa ile lafudhi yake) Bado mleta mada unadhani kuna mtu anahujumiwa na TRA? TRA wenyewe wana stress za kufikisha na kuvuka lengo 😀
It is his own making.Inaumiza sana kwa hizi hujuma za wazwaz kabisa ambazo TRA inafanya. Kuwachonganisha wafanyabiashara na Mh Rais. Ionekane serikali yake inaonea na kunyanyasa wafanya biashara. Ionekane haiwajali.
1. TRA walianza na kukusanya KODI. Hapa hatukuwa na shida ndiyo ilikuwa kazi yao. Wakasifiwa sana kwa ukusanyaji, wakamaliza.
2. Wakaja mara ya PILI wakaanza kukusanya MITAJI yetu. Hapo ndo wengi tumejikuta tumefunga biashara.
3. Mara ya TATU wanakuja kukusanya MALI TULIZOBAKI NAZO.hapa tumejikuta wengine tunaamua kuziuza tu hasara ili tubaki bila kitu. Ijulikane moja.
4. Mara ya NNE sasa wanakuja KUTUKUSANYA SISI. Ole wetu sisi. Ole wetu. Ingetufaa zaidi tufungwe jiwe la kusagia na kutupwa baharini.
Mh. Rais unahujumiwa. Wametukamua maziwa, sasa wanatukamua Damu. Wanategemea tutaishi vipi?