Namna unavyoweza kujikinga na maambukizi ya VVU baada ya kupitia mazingira hatarishi

Namna unavyoweza kujikinga na maambukizi ya VVU baada ya kupitia mazingira hatarishi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Post-Exposure Prophylaxis au PEP ni njia inayotumika kumkinga mtu ili asipatwe na maambukizi mapya ya VVU baada ya kupitia mazingira hatarishi yanayoweza kumfanya aambukizwe.

Ni njia inayohusisha matumizi ya wiki nne ya dawa za kutibu VVU kama kinga ya dharura kwenye kuzuia kutokea kwa maambukizi mapya.

Mhusika hupaswa kufika hospitalini haraka ili apatiwe huduma hii kwa muda usiozidi masaa 72 tangu apitie changamoto hiyo.

PEP huwa na ufanisi wa hadi asilimia 81 katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU.

Baadhi ya mazingira na hali hatarishi zinazoweza kuruhusu matumizi ya dawa hizi ni kupasuka kwa kondomu wakati wa tendo la ndoa, ajali yoyote inayohusisha vifaa vyenye ncha kali kama viwembe na sindano pamoja na kubakwa.

Mwongozo wa Serikali ya Tanzania umeweka utaratibu wa matumizi ya dawa za TDF 300mg + 3TC 300mg + DTG 50mg au maarufu zaidi kama TLD kwa watu wazima na AZT+3TC+LPV/r zikitumika kwa watoto.

Dawa hizi hutolewa bure kwenye hospitali zote za Serikali.

Chanzo: Wizara ya Afya (STG NEMLIT 2021)
 
Back
Top Bottom