SoC01 Namna Vigezo soko la ajira vinavyowanyima vijana kuingia soko la ajira na athari zake

SoC01 Namna Vigezo soko la ajira vinavyowanyima vijana kuingia soko la ajira na athari zake

Stories of Change - 2021 Competition

MoseeYM

Senior Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
144
Reaction score
199
UTANGULIZI

Takwimu za soko la ajira kwa mwaka 2018,Zinaonesha kuwa Vijana 800,000 huingia kwenye soko la ajira kila mwaka nchini Tanzania,lakini ni asilimia 10 tu ndio hufanikiwa kuajiriwa.
Zipo jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na serikali kupitia Sera ya taifa ya maendeleo ya vijana,lakini jitihada nyingi zilizofanyika zimeonesha kutoendana na kasi ya Mabadiliko.

VIGEZO SOKO LA AJIRA.

Miongoni mwa Vigezo muhimu kwenye ajira nyingi zinazotangazwa karibuni ni kama ifuatavyo: Uzoefu miaka (2-15),Elimu (Degree,Masters, PhD na Diploma kwa uchache),'Soft skills' kama vile( uwezo wa kujieleza,Uwezo wa kutafuta suluhu ya matatizo,uongozi,uwezo wa kuendana na mazingira ya kazi,Lugha nk),Uwezo mzuri wa kutumia programu mbalimbali za kompyuta kama vile(Excell,word nk).

VIKWAZO VIGEZO VINAVYOHITAJIKA SOKO LA AJIRA..

Uzoefu kimeonekana kuwa ni kikwazo kikubwa sana hasa kwa vijana wanaohitimu masomo na kutegemea kuingia moja kwa moja kwenye soko la ajira.Siku hizi imekuwa si ajabu kuona kazi nyingi zikihitaji Uzoefu wa miaka Hata nane ,Ukweli ni kwamba hapo kinachofanyika ni 'kuibiana' wafanyakazi baina ya taasisi na taasisi na si fursa ya ajira kwa sababu watu wengi wenye Uzoefu wa kazi wanakuwa tayari wako kwenye ajira.Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba ajira za namna hii hazisaidii kupunguza idadi ya wahitimu wanaomaliza vyuo kuzurura mitaani.

'Soft skills',baadhi ya mifumo iliyopo na hata vijana waliowengi wanaojiandaa kuingia soko la ajira hawana 'soft skills'.Kiufupi soko la ajira limeonekana kuhitaji zaidi watu wenye sifa za ziada kuliko wenye sifa ambazo kila mtu mwenye ujuzi fulani anaweza kuwa nazo.Mfano kazi inaweza kumhitaji mtu aliyesomea 'markerting' ,waliosomea ' marketing' wanaweza kuwa wengi,lakini mtu aliyesomea 'markerting' mwenye uwezo wa mzuri wa kujieleza na ubunifu akawa na nafasi kubwa ya kupata nafasi,kuliko wengine.

Baadhi ya 'Intenship' zinazotolewa zimekuwa za kinyonyaji kwa vijana,kwani kuna baadhi zimekuwa za pesa 'kiduchu' sana kiasi cha kutotosheleza kama lilivyo lengo lake la kusaidia mhusika asishindwe kumudu mahitaji binafsi madogomadogo,na sehemu nyingine imedaiwa hata hiyo 'kiduchu' haitolewi zaidi ya chakula cha bure.

ATHARI ZA VIJANA WANAOMALIZA VYUO KUSHINDWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA AJIRA.

Kujiingiza kwenye shughuli nyinginezo ambazo hazihusiani na taaluma walizosomea,hivyo kupoteza wanataaluma ambao wangekuwa msaada kwa taifa.Hii haina maana ya kwamba ni dhambi kwa kijana kufanya shughuli ambayo siyo taaluma yako.isipokuwa ninamaanisha kuna umuhimu zaidi kufanya kazi itakayokuza taaluma yako.Mfano:Fikiria kijana aliyesomea ualimu akamaliza mwaka 2015 ,ambaye akitaka kwenda kufundisha private unamdai Uzoefu miaka mitatu ,akaamua kujiingiza kwenye kilimo kama njia ya kujiajiri bahati nzuri mambo yakamnyookea akaamua kusahau suala la ualimu,Tutapoteza wataalamu wangapi kwa aina hii?.

Kuwakatisha tamaa wale wanaoingia kwenye mfumo wa elimu,kusomea taaluma ambazo wanawaona ndugu zao wapo mtaani hawana ajira.Ilihali taaluma hizo bado zina umuhimu kwa maendeleo ya nchi.

Kutokana na ugumu wa kuingia soko la ajira, na vijana wengi kuhitaji kuingia.Hii inaweza pelekea kukithiri kwa rushwa (Kama vile pesa,ngono nk) kwenye soko la ajira ,kwa lengo la kupata upendeleo wa nafasi ya ajira.

Kasi ndogo ya urejeshwaji au kushindwa kurejesha madeni ya bodi ya mikopo (HESLB) hasa kwa wale waliopewa mikopo ya serikali wakiwa vyuoni.Ieleweke kuwa hata kama mfumo wa bodi utawafikia wahusika wote,bado kasi ya urejeshwaji itategemea na kiwango cha kipato cha wahusika.Lakini pia ikumbukwe kuwa wale walio kwenye mfumo wa ajira rasmi ndio wanaotambuliwa kirahisi na mfumo wa bodi kuliko ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira.



NINI SULUHISHO?

Kuanzisha mikakati itakayowahusisha kikamilifu vijana katika maamuzi au maandalizi yanayohusu Sera ya ajira kwa vijana.

Waajiri kutoa kipaumbele zaidi kwa vijana ambao wana ujuzi lakini wako mtaani,kuliko wale waliopo makazini.Hii itasaidia kupunguza idadi ya vijana wenye ujuzi walioko 'mtaani'.

Posho zinazotolewa kwa vijana wanaofanya 'intenship' ziendane na hali halisi ya maisha.Hii itasaidia hata vijana wasiingie katika mtego wa wizi,kwani kutojitosheleza kwa maslahi kunaweza kuwapelekea katika tamaa ya kuiba ili wapate pesa za kujikimu.

Sera za kusaidia vijana kuingia kwenye mfumo wa ajira,ziendane na mazingira ya nchi (Ambapo lengo hili linaweza kufikiwa endapo tafiti nyingi zinazohusu namna ya kutatua changamoto ya ajira zitaendana na mazingira tuliyopo).Na sio tu "kukopi" kila kitu kutoka mifumo ya nchi nyingine ,ambazo zimetatua kulingana na mazingira yake.Mathalani,Ujerumani wamefanikiwa sana. Kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambapo ,inadaiwa kupitia shirika La kazi duniani ,ILO ,miongoni mwa sababu zilizochangia suala hili kufanikiwa ni kuwa idadi ya vijana imeonekana kupungua kwa miongo kadhaa.hasa kundi la vijana kati ya miaka (15-24).Hii ni tofauti na huku kwetu ambako idadi ya vijana wa rika hill wamekuwa wakiongezeka.


HITIMISHO

Suala la kujiajiri ni la muhimu endapo mifumo iliyowekwa na serikali inakuwa na unafuu na ya 'kutia moyo' vijana kujiajiri,kuliko kupiga 'propaganda' vijana wajiajiri ,na hali mazingira hayatoi fursa kujiajiri.IELEWEKE kuwa suala la kujiajiri tu,sio suluhisho pekee la kila kinachoitwa 'Tatizo la ajira'.Ni muhimu pia kuangalia mfumo wa ajira wenyewe.

Hakuna umuhimu wowote wa serikali kuendelea kutoa PESA kwaajili ya kuwasomesha watu ambao mwisho wa siku hawazitumii taaluma zao.kutokana na kusisitizwa kujiajiri kwa kufanya shughuli nyinginezo mbali na taaluma walizosomea.

kiwango cha elimu kinaweza kumpa mtu fursa ya kuleta mabadiliko na yasije,isipokuwa matumizi ya elimu aliyonayo.



Nawatakia utekelezaji mwema katika kunipigia kura
 
Upvote 3
Back
Top Bottom