Namna viongozi wa vyama Vya Upinzani wanavyotumia vyama na majina yao kujipia fedha kwa kuhujumu na uzandiki

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Uwanja wa siasa kokote pale duniani haujawahi kuwa uwanja wepesi. Siku zote, mtawaliwa anaitamania nafasi ya mtawala, wakati mtawala anajiimarisha kila leo nafasi yake isichukuliwe na mtawaliwa (Power Struggle).

Kwa miaka yote tangu kuumbwa kwa dunia hayo ndio yamekuwa maisha ya mwanadamu, kutamani nafasi ya juu zaidi kuliko binadamu mwingine na vita hii, haitokuja kuisha hadi dunia itamatike.

Katika uwanja wa siasa zipo njia safi za kuingia madarakani ambazo hufanywa hadharani lakini pia zipo njia chafu ambazo hufanywa kwa siri kubwa sana na mara nyingine, hushirikisha hadi watu wa nje na hapa, ndio ulipo msingi mkubwa wa andiko hili.

Kwa miaka mingi tangu nchi za Afrika zianze kupata uhuru mwanzoni mwa 1960s, mataifa yaliyolitawala Bara la Afrika yamekuwa yakifanya kila aina za hila na uzandiki kuhakikisha kwamba nchi za afrika hazitawaliki, vinakuwa na vurugu za kila aina na mikasa isokwisha ili wapate mwanya kuendelea kunyonya rasilimali zetu.

Mataifa hayo hutumia watu wa ndani ya nchi husika kama vibaraka wao kwa kuwalipa fedha nyingi kutimiza azma zao. Wanaweza kutumia njia ya mapinduzi ya kijeshi kama walivyofanya Burkina Faso kwa kumpindua Rais Thomas Sankara na kumpandikiza kibaraka wao, walifanya hivyo pia DR Congo kwa kumpindua Fabrice Lumumba na kumpandikiza kibaraka wao kuwa Rais.

Wanaweza kutumia njia za kuleta machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kama ilivyokuwa Angola kati ya UNITA na MPLA, wanaweza kusababisha maandamano makubwa yanayoweza kupindua serikali kama yale yaliyotokea Sudan na kumpindua Rais Al-Bashir au yale ya Sri Lanka mwaka 2023 ambapo yaliweza kupindua serikali.

Mara zote vurugu hizi kuandaliwa na kupikwa vizuri sana na majasusi kutoka nchi za nje kwa kutumia watu wa ndani. Kwa kiasi kikubwa ili njia za maandamano au vita vya wenyewe kwa wenyewe ziweze kufanikiwa ni lazima ushirikiano watu wa ndani upatikane.

Sasa basi, kwenye kuchagua watu wa ndani huwa wanatazama vigezo mbali kadha wa kadha vya msingi sana ambazo wakivitumia hivyo, basi ni rahisi sana kuleta machafuko. Mfano, ka,ma nchi ina historia ya migogoro ya kidini, basi watatumia kigezo hicho kuleta machafuko. Kama nchi ina mgogoro wa chini chini kama wa ukabila, basi mwanya huo utatumika kuleta machafuko, kama ni ukanda basi huo utatumika, yani lazima watazame jambo ambalo ni rahisi kuibua hisia za watu

Sasa wakikosa vyote hivyo, hutumia vyama vya siasa hasa vyama vya upinzani kuleta vurugu na machafuko. Wakishindwa kabisa vyama vya siasa, watutumia NGO's kama Ford Foundation kule nchini Kenya ilivyotumika kuleta maandamano makubwa au LHRC hapa nchini inavyotumika kupenyeza agenda za magharibi nchini lakini kutokana na misingi imara ya ulinzi kwenye Taifa letu, harakati hizo zimekuwa zikigonga mwamba.

Kwa sasa, ni wazi kabisa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatumika kutaka kuleta vurugu nchini kwa maslahi wanayojua wao. Huu ni mwendelezo wa hila za nchi za magharibi kutaka kuharibu ustawi wa mataifa ya kiafrika. Kwa miaka mingi sana CHADEMA imekuwa ikitumika kupenyeza agenda mbalimbali nchini hata zile ambazo zinakwenda kinyume na utamaduni wetu na mafundisho ya dini.

Ili kutimiza azma lengo kuu la kuleta machafuko kwenye nchi husika, hatua ya kwanza kabisa inayofanywa na nchi za magharibi ni kutumia vyombo vya habari vya nje na ndani kuandika habari za uzushi kuchafua viongozi wa nchi na mambo mengine mabaya. Jambo la pili ni kuvipa mbinu vyama vya siasa, wanaharakati na asasi za kiraia kama (NGOs) kufanya Civil Disobedience (Kuvunja sheria halali makusudi) ili kuleta taharuki.

Mfano, vyama vya upinzani vinaweza tu kuandaa maandamano au mikutano ya hadhara bila kuomba kibali kutoka mamlaka husika. Wanafanya hivyo wakijua kwamba watakamatwa, watawekwa ndani na kuanzia hapo, vyombo ya habari vinaaza kuandika sasa taarifa za uzushi juu ya uvunjifu wa demokrasia wa serikali, hata kama vinajua kwamba, uvunjifu wa sheria na amani ya nchi, ulianza kufanywa na vyama vya siasa.

Mfano, mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliopangwa ufanyike Jijini Mbeya siku ya Vijana Duniani Agosti 12, 2024, haukuwa wa kisheria kwani hauna kibali kutoka polisi kama sheria inavyotaka. Lengo lao hasa halikuwa kutaka kufanya mkutano, lengo lao ni kuionesha dunia Tanzania ni nchi ya aina gani. Kwa hilo hadi muda huu, wamefanikiwa sana ingawa, haina madhara kwa serikali kwa namna yeyote ile.

Walijua kwamba watakamatwa na vyombo vya habari vya ndani na vile vya nje vyenye kupokea bahasha kutoka magharibi, vitarindima mtandaoni kuandika mabaya yote kuhusu serikali ya Tanzania na nadhani hadi muda huu unasoma andiko hili, tayari ushakutana na taarifa nyingi mtandaoni juu ya kuzuia mkutano wa CHADEMA na kukamatwa kwa viongozi wake.

Sasa basi, viongozi wa upinzani au wanaharakati wanavyoendelea kukaa ndani au kupitia aina yeyote ile ya dhoruba kutoka kwenye mikono ya serikali, nchi zilizowatuma kufanya hujuma hizo, hulipia mateso yao kwa fedha. Yaani kiongozi anavyozidi kukaa jela, basi ndivyo anazidi kuingiza fedha kwani, kukaa kwake ndani kunazidi kutoa justification ya hali halisi ya nchi kidemokrasia na hiyo, huvifanya vyama vya siasa na NGOs kuingiza fedha zaidi kutokana na maandiko ya proposals wanayotuma nje yenye lengo la kutaka kuimarisha hali ya kidemokrasia nchini kwani, tayari wana ushahidi mzito wa kiongozi wao kuwa gerezani ambao wanaotumia kubeba hoja za andiko lao.

Ndio maana, kiongozi wa siasa akiwa uraiani na kama kuna amani kabisa, anaweza kufanya vurugu ya makusudi isiyo na kichwa wala miguu ilimradi atiwe nguvuni apate cha kusema na vyombo vya habari vipate cha kuandika. Kwao, huu ni ugali tosha.

Ili utambue kwamba CHADEMA ni wanafiki na wanatumika vibaya, mbona ACT Wazalendo wamesherehekea siku ya vijana vizuri tu bila shida yeyote? Kwani ACT Wazalendo sio chama cha upinzani? hapo utaelewa kwamba, msingi wa sherehe za siku ya vijana kwa upande wa chadema, haukuwa sherehe hizo bali kutaka kuleta vurugu ili wakamatwe na nchi iingie matopeni.

CHADEMA haina rasilimali yeyote ile, unaweza kujiuliza inamudu vipi gharama za kuendesha shughuli za chama kama vile kufanya mikutano mikubwa kila mkoa, kiongozi wao kutumia usafiri wa gharama wa helkopta kuruka mkoa hadi mkoa. Wanatoa wapi fedha? Kama umesoma andiko hili kuanzia mwanzo, utagundua kwamba CHADEMA inatumika na watu wa nje kuchafua serikali yetu. Hili sio jambo la jana wala juzi, inajulikana siku nyingi sana kwamba CHADEMA ndio kibaraka mkubwa anayetumika kubagaza na kuuza amani ya Taifa hili zuri kwa vipande vya fedha.

Pia soma=> Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa
 
Niseme tu weweni mfano wavilaza wengi wa nchi hii wasioamini fikra huru,huwezi kuzuia siasaza vyamabingi au mawazo mbadaka labda kama ni dikteta au mbumbumbu,hauna akili
 
Halafu kwa nini hayo maandamano wasifanye Hai na Moshi? Wanaleta Mbeya tu ili kutuharibia uchumi wetu.

Wakipata ruzuku wanarudi kujenga kwao kama Mbowe alivyojenga jumba lake.
 
Heheh endelea hakuna jipya.
 
Halafu kwa nini hayo maandamano wasifanye Hai na Moshi? Wanaleta Mbeya tu ili kutuharibia uchumi wetu.

Wakipata ruzuku wanarudi kujenga kwao kama Mbowe alivyojenga jumba lake.
Fanilia ya akina mbowe ina hela tangu mkoloni,kipindi cha kudai uhuru,nyerere aliLuwa akishikwa njaa anaenda nyumbani kwa akina mboww kuomba mahitaji
 
Hakuna kitu kama hicho. Yule mzee alikwisha anza kufilisika kabla hajakufa. Mnatumika tu kumtajirisha Freeman Mbowe
 
Wale wanao uza nchi kwa waarabu hawahatarishi usalama wa nchi?
 
Halafu kwa nini hayo maandamano wasifanye Hai na Moshi? Wanaleta Mbeya tu ili kutuharibia uchumi wetu.

Wakipata ruzuku wanarudi kujenga kwao kama Mbowe alivyojenga jumba lake.

Hakuna kitu kama hicho. Yule mzee alikwisha anza kufilisika kabla hajakufa. Mnatumika tu kumtajirisha Freeman Mbowe
Una roho ya kimasikini ba utakufa masikini
 
Halafu kwa nini hayo maandamano wasifanye Hai na Moshi? Wanaleta Mbeya tu ili kutuharibia uchumi wetu.

Wakipata ruzuku wanarudi kujenga kwao kama Mbowe alivyojenga jumba lake.

Hivi maandamano yaliruhisiwa, vipi Tena mnaogopa. Halafu maandamano yalipofanyika uchumi gani ulishuka? Punguza unafiki na kuropoka .
 
Mkuu umeandika makala nzuri!
Lakini hata hivyo hayo yanatokea katika nchi ambazo hakuna utawala bora.
Mfano nchi ambazo zinatawaliwa kidikteta ndiyo mara nyingi kuna machafuko!
Na hakuna namna ya kuziondoa zaidi ya kutumia hizo njia ulizoorodhesha!
 
Back
Top Bottom