Namna viongozi wa vyama Vya Upinzani wanavyotumia vyama na majina yao kujipia fedha kwa kuhujumu na uzandiki

Hivi maandamano yaliruhisiwa, vipi Tena mnaogopa. Halafu maandamano yalipofanyika uchumi gani ulishuka? Punguza unafiki na kuropoka .
Nataka yakafanyikie Moshi siyo Mbeya. Mnatuharibia jiji letu. Kaharibuni kwenu huko uchagani
 
Ujinga mkubwa sana kwa kuisapoti CCM na bado umaskini unakutafuna.
 
Binti Mjinga huyuuu
 
Wewe hauko sawa sawa kabisa kwa hichi ulichokiandika
 
Halafu kwa nini hayo maandamano wasifanye Hai na Moshi? Wanaleta Mbeya tu ili kutuharibia uchumi wetu.

Wakipata ruzuku wanarudi kujenga kwao kama Mbowe alivyojenga jumba lake.
Kwani Mbeya iko Afghanistan?
 
ujinga wako unaanzia hapa, na katika maandiko yako mbalimbali umeonesha kujitanabaisha na watawala kwa namna ya kutoka kuhojiwa au kukosolewa kwa namna yoyote kwa kutumia mwamvuli wa uvunjaji wa amani. Serikali iliyoko madarakani hivi sasa inatokana na chama cha mapinduzi na ndiyo baada ya mabadiliko ya kidunia katika siasa na uchumi iliridhia kwa lazima kukubali mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania. Kupitia bunge la chama kimoja ilihuisha katiba ya chama kimoja iliyotokana na kikao cha ccm (bunge) na kuifanya kuwa katiba inayotambua uwepo wa vyama vingi jambo ambalo kiuhalisia au kivitendo (practical) sio kweli.
Chama cha mapinduzi hakikuwa tayari kukubali mfumo wa vyama vingi hata kidogo na kilikataa mapendekezo ya Tume ya Jaji Francis Nyalali. Ilikua ni Busara ya mwalimu Nyerere kulazimisha hilo kufanyika.
Chama hicho kilikaa kama kamati ya ccm kikaandaa muswada wa sheria ya vyama vingi vya siasa na kuwasilisha katika Bunge kwa ajili ya kupitishwa na kuwa sheria.
Pamoja na mambo mengine kwa kuwa hawakujua kitakachokuja kuwa nguvu ya umma kutaka mabadiliko kwa kupitia njia mbali mbali au kueleza kero zao, wakaweka moja wapo ya haki za vyama vya siasa kuwa ni kufanya mikutano ya siasa, kuandamana miiongoni mwa mambo mengine. Hali kadhalia sheria hiyo ikaweka bayana kwamba vyama vya siasa vitatoa taarifa kwa afisa wa polisi wa eneo husika kuhusu kufanyika mikutano au maandamano ili kupatiwa ulinzi. Hakuna mahali popote sheria hiyo imetaka kwamba waombe unachoita kibali. Kwa sababu katiba ambayo miaka hiyo ya 90 iliweka bill of rights kama sehemu yake inatoa uhuru na haki ya watu kukusanyika, kutoa maoni au mawazo yao juu ya mambo yanayowahusu ilimradi wasivunje sheria za nchi.

Kwa muktadha huo basi ujinga wako unajidhihirisha pale unapondika kwamba : Mfano, vyama vya upinzani vinaweza tu kuandaa maandamano au mikutano ya hadhara bila kuomba kibali kutoka mamlaka husika.
Kumbe sasa kwa uthibitisho uliyo bayana ni kwamba CHADEMA walifanya mikutano yao ya kisiasa mikoa kadhaa hapa nyuma na wakapewa ulinzi wa polis na hakuna tafrani yoyote iliyotokea.
CHADEMA walifanya maandamano katika baadhi ya mikoa kuwasilisha maoni yao juu ya kupanda kwa gharama za maisha pamoja na mambo mengine na hali ilikua shwari kabisa na hatukusikia chochote kilichotokea na nchi ilikua na utulivu.

Ajabu ni kwamba wakati vijana wa CCM wanafanya maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani kule visiwani Zanzibar walipewa state protection na state facilities na wakadhimisha maadhimisho yao bila shida yoyote na nchi ikawa tulivu. CHADEMA kama ilivyo miaka mingine nayo iliandaa siku ya vijana na kuazimia kufanya maadhimisho hayo mkoani Mbeya kama walivyofanya Arusha, Taarifa zilizotolewa vizuri kwa Jeshi la polisi ili lijipange kuhakikisha usalama na jeshi la polisi lilitoa ushirikiano mpaka siku chache kabla ya tamasha kufanyika na sio maandamano wala mkutano wa chama.

Polisi akiwemo RPC anaokena kutoa ushirikiano kuhakikisha kuwa zoezi hilo linamalizika salama na watu kuendelea na shughuli zao kama walivyofanya ACT na CCM.
Kamishna wa mafunzo operesheni Bwana awadhi anaamua kukaa upande wa watawala na kusahau wajibu wake wa kutenda haki na anaamua kufanya uvamizi na kutoa amri ambayo inaondoa utulivu na amani saa chache kabla ya tamasha huku akisema kwamba ni Maagizo kutoka juu. Taarifa ya Polisi inashindwa kutofautisha kuwa kinachozuiwa na maandamano, mkutano, kusanyiko au kongamano. Ujinga unaongezeka pale watu wanapozuiliwa njiani pamoja na magari yao kuelekea Mbeya, ukiukwaji wa Katiba ya nchi wazi wazi kuwa kila mtu ana haki ya kwenda mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati huo huo hakuna boti au ndege iliyozuia watu kwenda Zanzibar.

Swali la msingi, Nani aliyesababisha uvunjifu wa amani kati ya polisi na CHADEMA? jibu sahihi ni polisi!
Kwa nchi inayoheshimu utawala wa sheria, baada ya kukamatwa viongozi na wanachama wa chadema ni dhahiri kwamba walikua wamefanya makosa au wamejaribu kufanya makosa (Tuseme kwa huo ujinga wako, kuamdamana bila kibali kutoka mamlaka husika) Afande Awadhi alipaswa kuwafungulia Mashtaka kwa mujibu wa sheria kwa muda usiozidi saa 24 na wapate adhabu yao inayostahili. Aibu ni Kwamba Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi anaagiza waachiwe mara moja. Swali kwako katibu mkuu wa ccm ana mamlaka gani juu ya vyombo vya usalama? Jibu linakuja sahihi kwamba ccm sio chama cha siasa ila ni kikundi dola kilichojificha nyuma ya siasa na watu wa dola ni wajumbe wake. Hii ni dhahiri kwamba wanaoleta vurugu au wanaotumiwa na mataifa ya nje kuiba rasimlimali za nchi ni watawala na wanapohojiwa husababisha taharuki na vurugu kwa wananchi.
Rejea maswala ya BANDARI yaliyompa Dr Slaa na Mwabukusi kesi ya UHAINI, rejea yanayoendelea Ngorongoro ambapo hata watu wamenyimwa haki ya kuishi, (Uwongo wa uhifadhi umetamalaki) huku Rais (Mwenyekiti wa chama akitangaza hadharani kwamba atatoa leseni za uchimbaji madini Serengeti mbugani kwa sababu tembo na simba hawali madini. (pima)
Kilichotokea Mbeya ni MAAGIZO ya chama cha mapinduzi (KAMATI KUU) Ambapo SPEAKER kutoka Mbeya ni mjumbe ambaye alizunguka karibu mkoa wote wa mbeya kuwaaminisha watu uhalali wa mkataba wa DP world ni sahihi mpaka Mahakama inakuja kusema tofauti kwamba una shida, Na mwenyekiti wa Chama ambaye ni mtia sahihi mkuu na mwenyekiti wa chama pia. Hofu kubwa ilitanda kwamba Yule Jamaa (Kajunjumele) atahutubia na kuwaeleza waendesha bajaji za mkopo wa Tulia Trust Mbeya nini cha kufanya alongside CHADEMA.
Ujinga wako mwingine unaowaabisha wamasai ambao tunaamini ni watu wenye akili ni huu: vyombo ya habari vinaaza kuandika sasa taarifa za uzushi juu ya uvunjifu wa demokrasia wa serikali, Swali kwako, Je vyombo vya habari kureport kwamba watu wamepigwa, wamekamatwa na wamezuiliwa njiani ni uzushi na uwongo? Kuwazuia watu kinyume cha sheria mlizotunga wenyewe sio kinyume cha sheria na demokrasia ya nchi? Kama walivunja sheria kazi ya mahakama ni nini?
 
pata muda usome hii hapa acha kuandika ujinga usiohimilika na watu waliolipa ada na sio wa elimu bure: https://www.nomos-elibrary.de/10.5771/0506-7286-1995-4-468.pdf?download_full_pdf=1
 
Nataka yakafanyikie Moshi siyo Mbeya. Mnatuharibia jiji letu. Kaharibuni kwenu huko uchagani
Kwa akili yako ulivyoona kuna maandamano yaliyofanyika na yaliyopelekea watu wasio kuwa na akili (iron) boys kufanya vurugu yalifanyia? Kuna taarifa yoyote ya kuwepo maandamano au tamasha la siku ya vijana? Je yangefanyika maandamano ya kumpongeza Tulia kwa kuwakopesha bajaji, badala kusimamia bunge lake liisimamie serikali ije na sera bora za ajira kwa wahitimu na wasiokua wahitimu badala ya kushupalia uuzaji wa bandari na mbuga zetu Polisi wangewazuia? acha ujinga taifa linakutegemea
 
Umeandika yote haya nikiamini hujazaliwa afrika na hujafika aftica.

Na naamini unaishi ktk nchi ya kidemokrasia lkn unataka afrika na tz iendeleze mfumo wa autocracy.

Wakati chadema inaamini ktk autonomous.

Kwa kuwa mfumo wa serikali kuu umeshindwa na kwasasa haupo ktk hizo nchi unaishi.

Amani na furaha kwa waAfrica na tz itapakana ukibadili mfumo wa utawala na kuwa wa federal zenye nguvu zaidi ya kujiamulia mambo yake wenyewe.

Amani na furaha kwa africa yapatikana iwapo uimla tutauondoa.

uimla unamfanya rais awe Mungu mtu.

Switzerland ni moja ya taifa lenye mgawanyiko wa makabila tofauti. Waliamua kila jimbo lijitegemee.

Africa na tz tunapaswa kucopy nakupaste mfumo huu wa utawala

 
Taifa linanitegemea ni kweli. Na nipo hapa natoa elimu ya bure kwa vijana wa Mbeya waache kufuata mkumbo kwenye maandamano.

Wanawatengenezea fedha tu akina Mbowe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…