Quartz360
Senior Member
- Mar 27, 2023
- 133
- 317
UTANGULIZI
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kunukuliwa akisema kwamba “Dhima kuu ya elimu ni kuleta uhuru wa kifikra miongoni mwa watu, uhuru wa kifikra ambao utawasaidia kujitoa katika wimbi kubwa la ujinga, utumwa na utegemezi, elimu ambayo itakuwa ni chachu ya kuwafanya watu waweze kuyaweka mawazo yao katika uhalisia”. Hayo yalikuwa ni maneno ya Mwalimu Julius Nyerere baba wa Taifa hili. Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa na malalamiko kutoka kwa wanajamii, mashirika, kampuni na asasi nyingi za kiraia juu ya uwezo mdogo wa wahitimu wanaotoka vyuoni, lawama hiizi zimekuwa zikitupwa moja kwa moja kwa wahitimu ya kuwa si wachapakazi, si wabunifu na hawana uwezo wa kujenga hoja katika mambo mbalimbali.
KIINI CHA MAADA
Kama taifa tunapaswa kulizingatia hili, kwa maana kwa kiasi kikubwa elimu ya juu ndiyo imebeba hatma ya taifa letu, kwa kuhakikisha tunazalisha wahitimu bora, wenye fikra chanya, wachapakazi na wenye ari ya kuleta mabadiliko katika jamii zao kwa kufanya yafuatayo.
1. Tubadilishe mitaala yote ambayo haiendani na ulimwengu wa sasa kuanzia kwenye ngazi za chini za elimu. Mtaala wa elimu ni kama dira na kitovu cha mabadiliko kwa watu katika taifa. Kile wanachofundishwa wanafunzi huakisi uwezo wao baada ya kuhitimu masomo yao. Hivyo, ni lazima serikali kwa kushirikiana na wadau wafanye maboresho ya mitaala yote ya elimu kuanzia kwenye ngazi za chini, mabadiliko hayo yaendane na kuondoa vitu vyote visivyokuwa na umuhimu kwa dunia ya leo, mabadiliko ya mitaala yaendae na kile kilichopo katika mazingira ya jamii zetu, vilevile mabadiliko hayo yalenge kuwajengea uwezo wanafunzi kuweza kuwa na fikra za kujitegemea, wajiamini na wawe tayari kupambana na hali zote za maisha baada ya kuhitimu masomo yao. Hivyo, wanapofika kwenye ngazi za juu za elimu wawe tayari wanaishi katika kusudi na karama zao za asili.
2. Kuandaliwe midahalo ya kitaifa itakayofanyika kila mwaka, midahalo hii ilenge kuwakutanisha wasomi walioko vyuoni na viongozi wa nchi, midahalo hii lienge kuibua mawazo yakinifu yenye kujenga ustawi wa taifa letu, viongozi wetu mfamo mawaziri, wakuu wa idara mbalimbali ha nata raisi, waweze kutembelea kwenye taasisi za elimu ya juu kwa lengo la kufanya midahalo na wasomi walioko vyuoni, kusikiliza hoja zao na kuzifanyia kazi, midahalo hiyo ikifanyika kila mwaka, itawajengea uwezo wa kujiamini wasomi walioko vyuoni, watakuwa na uwezo wa kujenga hoja kikamilifu, na watajua fika kuwa wanao wajibu wa kulijenga taifa lao kwa kuibua mawazo bora na yenye matokeo chanya. Hivyo hata baada ya kuhitimu watakuwa na uwezo madhubuti wa kuweza kujenga hoja,kutoa ushauri thabiti, kuwa mfano wa kuigwa na kuchochea ukuaji wa taifa letu.
3. Kuwepo na programu maalumu itakayofundishwa kwenye kila chuo. Programu hii isomwe na wanafunzi wote nchini walioko vyuoni bila kujali kozi zao, na ni bora zaidi programu hii ifundishwe mwaka wa mwisho wa masomo kabla ya kuhitimu, programu hii ijikite katika kuwajengea ujuzi vijana kuhusu masuala yanayohusu elimu ya kifedha, maendeleo binafsi, ujasiliamali, ubunifu na namna ya kutatua matatizo katika jamii zao. Ni dhahiri kuwa kupitia programu hii, vijana wataweza kuwa na uwezo binafsi wa kutatua changamoto zao na zile zinazoikumba jamii zao, itaamusha ushindani wa kimaendeleo, itawaongezea kujiamini, itatatua tatizo la ajira na italeta mwanga katika mapinduzi ya uchumi wa taifa letu.
4. Vyuo vyetu viboreshwe. Ili kupata wahitimu bora inabidi vyuo vyote vinavyotoa elimu ya juu viboreshwe kuanzia kwenye miundombinu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia, ubora wa walimu, vifaa na nyezo zote za ujifunzaji na ufundishaji. Ubora wa chuo pia huweza kuaksi ubora wa wanafunzi wake, na mazingira bora ya ujifunzaji huwa ni chachu ya mwanafuzi kuwa na uwezo mzuri zaidi katika taaluma yake, vile vile umahiri wa wahadhiri chuoni huweza kuzalisha wahitimu walio bora zaidi kwa maana “Chuma Hunoa Chuma” hivyo, wahadhiri wanapokuwa bora, hata wanafunzi watakuwa bora zaidi wakiwezeshwa na mazingira bora ya kujifunzia.
5. Vyuo vyote vikuu nchini vinapaswa kuwa na ushirikiano wa karibu na vyuo vya nje ya nchi. Siku zote ukitaka kuwa bora ni lazima uzungukwe na watu walio bora katika eneo unalotaka kuwa bora, vivyo hivyo kwa taasisi za elimu ya juu, zinapaswa kuwa na ushirikiano wa kuanzia hata vyuo vikuu vitano nje ya nchi kwa ajili ya kufanya mabadilishano ya wahitimu, kuboresha utafiti, kuongeza ujuzi na maarifa mapya miongoni mwa wahadhiri na wanafunzi wa taasisi washirika. Ushirika huu utakuwa ni chachu ya kuwafanya wanachuo wetu waweze kuwa na umahiri wa hali ya juu katika masomo wanayosomea na hii itawafanya wawe na mchango mkubwa katika jamii hata baada ya kuhitimu. Kufanikisha hili, kila chuo kiwe na kongamano na chuo kimoja wapo nje ya nchi kila mwaka kitakacho kuwa na wawakilishi kutoka kwenye kila idara kwa lengo la kubadilishana ujuzi, kufanya mashindano ya kiubunifu na kupeana mbinu za kuweza kufanya mapinduzi sathiki ya kielimu.
MWISHO
Hatupaswi kutoa lawama kwa wahitimu wanaotoka vyuoni kwa kusema ya kwamba hawana umahiri unaohitajika mtaani bila kujua sababu kuu inayosababisha changamoto hiyo, ni vyema tujikite katika kutafuta majibu ya changamoto hiyo, bila kumtupia lawama mtu yeyote yule. Hivyo, Serikali kupitia wizara ya elimu, kamisheni ya vyuo vikuu nchini, taasisi za umma, mashirika binafsi na asasi zingine za kiraia ziwe mstari wa mbele katika kuinua viwango vya elimu yetu na uwezo wa vijana wetu ili kutengeneza kizazi cha watu wenye maarifa, hekima, na wenye uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali katika jamii zao bila kutegemea nguvu yeyote kutoka nje. Kwani Nelson Mandela aliwahi kusema kuwa “Elimu ni moja ya silaha yenye nguvu, inayoweza kuubadili ulimwengu”
Asante kwa kusoma andiko hili.

Upvote
0