Namna Wasafiri wanaweza kujilinda Mtandaoni wakati wa kusafiri

Namna Wasafiri wanaweza kujilinda Mtandaoni wakati wa kusafiri

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Wasafiri wengi hutumia mitandao ya kijamii zaidi wanapokuwa safarini mbali na nyumbani. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa kudumisha faragha na usalama wa akaunti zako za mitandao ya kijamii huwa changamoto zaidi unapokuwa safarini.

Namna Wasafiri wanaweza kujilinda Mtandaoni wakati wa kusafiri

a. Usipige picha za tiketi za kupanda usafiri wako na kuzisambaza

b. Iwapo ni lazima upige picha na kutuma, hakikisha umeficha taarifa nyeti zikiwemo Misimbo Pau (Barcode)

c. Chagua tiketi ya Kidijitali badala ya tiketi ya karatasi inapowezekana

d. Usiweke maelezo ya safari yako kwenye Mitandao ya Kijamii

Kwanini Ujilinde Mitandao ukiwa Safarini?
a. Wadukuzi wanaweza kupata taarifa zako na kuzitumia kukufanyia Ulaghai (Phishing).

b. Taarifa zako ni muhimu kwa wizi wa Utambulisho, zinaweza kuwezesha udanganyifu kama kufungua 'Credit Card' au kufanya manunuzi bila idhini.

c. Tukio hilo pia linaweza kuwa kichocheo cha Wezi kuvamia nyumbani kwako kwani umeweka taarifa kuwa haupo
 
Back
Top Bottom