Nawatania
Senior Member
- Jul 13, 2021
- 148
- 549
Kwanza Mimi niseme Mimi sio mwizi wala sifanyi biashara haramu ya aina yeyote nitakayoyaandika hapa ni yale nimekutana nayo kwa kuona kwa macho au kwa kutumia mashahidi.
Niende moja kwa moja kwenye hoja mamba na Vitendo vya Wizi, Utapeli na Biashara haramu zinavyofanyika Tanzania.
1: Biashara haramu ya Bangi na Madawa ya kulevya.
Uvutaji wa bangi umekuwa sugu sana katika jiji la Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya na karibia mikoa yote ya Tanzania.
Bangi inapatikanaje mjini ni ngumu sana kutambua maeneo ya watu wanaouza bangi kama wewe sio mteja.
Mimi maeneo haya niliyafahamu kupitia kwenda kuinunua mfano Ukiwa mjini kwenye miji yetu mikubwa utaona maeneo ya mtu yupo kituo cha daladala anauza Pombe,Chenji au Pipi na Sigara hawa kazi yao kubwa ni kuuza bangi ukihitaji mzigo utaupata ila kama ni mgeni haupati mpaka uende kwa ishara kama ambavyo watu wa vitengo vya usalama utambuana! wateja wao wakubwa hapa ni Makonda, madereva na wapiga debe.
Pia bangi inauzwa kwenye baadhi ya maduka kwa ishara maduka hayo utakuta wanauza na pombe, ila pia kuna baadhi ya maduka ya nguo sehemu kama Kinondoni ndani yake unakuta biashara inaendelea hauwezi kuijua kirahisi mpaka uwe mzoefu wa hayo mambo ndio utafahamu.
Madawa ya kulevya maalufu kama Unga yanapatikana sana kwenye baadhi ya club za usiku na maduka makubwa pamoja na Supermarket baadhi sio zote ambazo wahindi wanapenda sana kununua bidhaa zao. Ingawa swala la madawa limekuwa likipungua kwa Tanzania ila biashara bado ipo sana na wanauziana kwa kujuana ukienda wewe unajifanya eti unataka hautapata chochote.
2: Wizi wa bodaboda
Wizi wa bodaboda umekuwa sugu sana na watu wengi wamepoteza maisha kwa sababu ya bodaboda.Mtu anakuja kama abilia ukimbeba anaenda kukunyang'anya pikipiki na kutoweka na kukuacha au amekuua kabisa.
Hii inakuwaje? ikishafika muda ya usiku epuka sana kufuatwa na watoto wa kike ambao wanataka uwapeleke sehemu ambayo upafahamu.
Wao uwa wanatazama bodaboda ambayo ni mpya kituoni kwa kukaa pembeni kidogo badae anakuja moja kwa moja kwako pia uwa wanaangalia body language yako, ule ulegevu, Upole
Hakikisha mtoto wa kike ambaye ni mzuri na mrembo anapokwambia ukifika pale sijui kuna kona then unaingia sijui hivi kuwa makimi wakati wa usiku nenda sehemu unazozijua ndio maana kila kituo kuna boda boda hivyo usiwe na tamaa ukiona ni mbali mbebe mpaka kituo kingine mwambie atafute sehemu hiyo kwa kuwatumia bodaboda wenyeji wanaopajua vizuri.
Hizi pikipiki zikiibiwa uwa zinarudishwa madukani hasa Kariakoo na kuuzwa tena kwa kufunguliwa na baadhi ya spare kuhamishiwa kwenye pikipiki zingine.
3: Wizi wa Magari
Wizi wa magari unafanyika sana maeneo yafuatayo Tanzania Dar, Moshi, Arusha na Tunduma.
Moshi magari uibiwa sana Kenya na kuletwa Tanzania 90% ya magari yanayoibiwa Nairobi yanaletwa Moshi na Arusha.
Na 90% ya Magari yanayoibiwa Arusha yanapelekwa Nairobi wanachokifanya wana gereji za kisasa wakifika kule wanabadilisha kila kitu ndani ya usiku mmoja na gari inakuwa mpya kabisa na kurudishwa kuuzwa tena.
Ndio maana unaweza kukuta gari mpya kabisa ila ina Namba za ALN lakini ukiingia ndani unaona kama ni gari ya 2019 au 2020.
4: Makampuni hewa
Mwaka Fulani 2012 Rafiki yangu aliwahi kutapeliwa na chuo hewa.
Aliambiwa hivi chuo kipo Morogoro kinatoa fani za unesi na madawa na kinadhaminiwa na shirika moja lipo Canada hivyo ada yake itakuwa chini maana wanapewa udhamini hivyo achangamkie fursa.
Kile chuo hewa kilifanya hivi hakikutangaza matangazo yake yeyote Morogoro kilitangaza Mikoa mingine Tanzania na kikafanikiwa kuuzwa fomu zaidi ya 200 na fomu moja walikuwa wakiuza shilling elf 10.
Chuo hicho hewa kilifanikiwa kufungua account ya bank ambayo sitahitaja kwa sababu za kiusalama na kibiashara lengo langu nataka tujifunze kuwa makini.
Basi ile account ya benki ikapitishwa na ile banki maana wale jamaa walikuwa wamejipanga kweli rafiki yangu akaambiwa amepitishwa na wenzake 200 watasoma bure chuo kwa kulipiwa na ilo shirika la Canada basi akaambiwa anatakiwa kulipia laki 3 kipindi hicho kama pesa ya hosteli na chakula wawapo chuoni ila garama zingine ni chuo ndio kitahusika. Aliniambia na Mimi nishugulikie fursa ila sikuweza kulingana na hali niliyokuwa nayo kipindi hicho.
Wale jamaa wa chuo hewa kwa jinsi walivyokuwa wamejipanga ile account ya banki wazazi wakalipia na siku ya kuripoti wakaambiwa wafike Morogoro mapema siku hiyo watapokelewa na magari ya chuo na kupelekwa chuoni.
Kama senema vijana wakatoka mikoa mbali mbali wakakutana Morogoro wakasubiri kumbe ndio walikuwa wameshalizwa na pesa zao zimeshaenda. Tuwe makini sana katika kila kitu maishani tunachofanya.
Fikiria 200×300000=60,000,000
5: Minada ya kuuza Nyumba, Viwanja na vitu vya ndani kwa waliochukua mikopo.
Hapa kuna wizi mkubwa sana unakuta mtu nyumba yake thamani yake ni million 60 anachukua mkopo wa million 40 analipa biashara inakufa.
Ameshalipa nusu ya mkopo kwa mfano kashalipa million 30 anadaiwa million 20 pamoja na Riba. wanamsumbua anapaniki wanakuja na mtu wao wamemuandaa kwenye mnada wanaanza mnada nyumba inauzwa million 20 kweli inakuwaje nyumba ya million 60 inauzwa million 20?
Wakimaliza mnada waanza tena kutafuta mteja mingine wanamuuzia nyumba milioni 50 au 60 yaani mabenki yamekuwa yakifanya uhuni sana kwa wateja wake. Hii pia inaenda kwenye viwanja na mashamba wanafanya hivyo.
Ushauri wangu kwa ujumla huu ya haya
1: Kwenye bangi mitaa yetu mingi ifungiwe kamera ili kupunguza tatizo, Pia polisi wafanye kazi yao waache kupewa rushwa.
2: Madawa ya kulevya tupambane nayo kwenye mipaka hasa bandari zetu na viwanja vya ndege.
3: Pikipiki na magari zifungiwe vifaa maalumu vya kumonitor zilipo kama ilivyo kwenye simu.
4: Umakini uwepo kwa wazazi wawe makini katika kuchagua shule na vyuo vya watoto wao kwenda kusoma.
5: Ziletwe Bima za mikopo mtu akishindwa kulipa bima imlipie halafu yeye atailipa Bima Pole pole hata ikiwa ni miaka 20 ijayo.
Asante kwa kwa muda wenu naamni tumejifunza jambo kupitia mada hii

Upvote
22