Namna ya ku secure funds kwa local Ngo

Mufassa

Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
18
Reaction score
41
Kwema wakubwa,

Naomba niende moja kwa moja kwenye swali. Nina wazo naona ni potential ambalo litasaidia watu wa hali ya chini vijijini nataka nikasajili Ngo kwa level ya kitaifa then nitekeleze wazo langu lakini changamoto ya hili wazo linahitaji rasimali fedha ili litekeleze, je ni wapi naweza pata mfadhili ? Je kuna utaratibu wowote serikalini wa ku fund project zenye tija kwa jamii?

Je ni kwa jinsi gani naweza kupata donors kwenye international Ngo’s vipi makampuni binafsi ya kitanzania yanawezesha ku fund project binafsi zenye lengo la kusaidia jamii ? Taratibu ni zipi na vigezo ni vipi vya kupata donors ? Asante sana.
 
Ngoja kwanza ncheke......!!!
Hongera kwa kuwa na "wazo" la kusaidia jamii. Ila nikwambie tu ukweli, pesa za msaada kuja kuzipata siyo lelemama. Ni za kugombaniana na NGOs nyingine.
Na Wala wewe si wa kwanza kuwa nalo na pia hiyo Hali ya chini haipo hapo kwenu pekee. Hivyo basi, waambie wanakijiji wako waanze kujikomboa wenyewe kwa maana "Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe".
Yes serikali inaweza kuleta msaada, hata mfadhiri anaweza kuleta msaada, Ila, narudia, Ila wanakuja kuendeleza na kuboresha kilichopo tayari.
Ukiwa na ng'ombe mmoja wa maziwa, mfadhiri anaweza kukuona akakuongezea ng'ombe mwingine au akakupa mashine ya kukatia majani. Kama huna ng'ombe hata mmoja usitegemee kupata Chochote.
Halafu kijana, think for your children's children. Huwezi kuondoa "Hali ya chini" kwenye jamii hizi zenye watu hawahawa!

Nenda page ya www.usadf.gov tafuta Tanzania application Kisha ujipime pengine unaweza kuambulia namna ya kuwasaidia watu wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…