Namna Ya Kuepuka Garama Na Usumbufu Wa Kuingiza Mzigo Kupitia Banda Ya Dae Es Salaam

Oppotunity

Member
Joined
Sep 9, 2013
Posts
38
Reaction score
12
Wana Jf Habari Zenu.
Mara nyingi nimekuwa nikiagiza bidhaa mbali mbali kutoka nje ya tanzania ila kero kubwa imekuwa ni makato makubwa yanayotozwa pale bandarini bila kuzingatia viwango halisi vya ushuru wa bidhaa yenyewe.
Licha ya hapo kuna usumbufu mkubwa sana tangu bidhaa inapowasili hadi pale unapoichukua baada ya kulipia kila kitu. ninataka niachane nao nitumie bandari ya mombasa kenya kwani wao naamini hawaendekezi ukiritimba kama huu wa hapa bongo. NAOMBA MWENYE UZOEFU AU KUJUA TARATIBU NA GHARAMA ZA HAWA JAMAA PAMOJA NA KUSAFIRSHA MZIGO HADI HAPA BONGO ANIJUZE TAFADHALI MAANA MIMI SIJAWAHI HATA KUFIKA HUKO.
Natanguliza Shukrani Za Dhati!!!
 
Kiukweli mombasa ni good idea kwa bidhaa kama magari kuna watu wanayaleta wakiyaendesha adi dar
Ila sina ufahamu wa kutosha juu ya hili
Ngoja wataalam wanakuja watakujuza
 
Mombasa kutoa mfano gari mpaka boda ya tanga ni usd 350 mpaka 450..mizigo ya container kama la 20ft ni usd 1500 mpaka 1800 to Border
 
Mombasa kutoa mfano gari mpaka boda ya tanga ni usd 350 mpaka 450..mizigo ya container kama la 20ft ni usd 1500 mpaka 1800 to Border

Real???? na Dar je gharama za container la 20ft ndani yake kuna nguo,viatu,handbags na accessories zingine gharama zake zikoje?
 
Kungekuwa na Transparency kwenye hizo rates sidhani kama kungekuwa na usumbufu huu wanayopata wafanyabiasha wa Tanzania... Hawa Jamaa wa bandarini na TRA wakati mwingine badala ya kukuza biashara ili wapate mapato zaidi wao wanaishia kuwakamua hadi wafe! Kuna ugumu gani wa wao ku-display rates wanazotoza pale bandarini kwa bidhaa na ujazo mbali mbali? ... nchi ya wasanii hii ...
 
Hizo garama ni za port..maswala ya ushuru unalipia TRA kama kawaida so mmi huwa naona bora dar..asvantage ya Mombasa ni momja tu..Cargo inawahi kitoka ila swala la kuwa cheap sio kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…