Namna ya kuepuka kuibiwa kwa njia ya wizi wa mfukon sehemu zenye misongamano

Namna ya kuepuka kuibiwa kwa njia ya wizi wa mfukon sehemu zenye misongamano

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Wizi wa mfukoni umeliza sana watu mjini kwenye msongamo, daladala n.k
Watu wameibiwa hela, simu n. K

Zingatia yafuatayo

1. Jiadhari na mtu anayekufatilia
Labda uko mjini unamuona mtu mpya anakufata bila sababu, umeingia dukani kaingia, umeenda kuchukua gazeti unashangaa yupo,
Huyo usione aibu mwambie ushamshutikia mtukane Kwa hasira, ni mwizi anakuibia

2. Jiepushe na taharuki za mjini zisizokuhusu
Unatembea mjini unakuta watu wanapigana au vinginevyo we hali safari yako ukisogea utaibiwa

3 Jiepushe kukaribiana na mtu kwenye msongamo, atakunyemelea akuchomolee malii zako

4. Kwenye daladala
Hakikisha pesa na simu vipo kwenye mfuko na umevishika kabisa, epuka kushika Bomba ya daladala ukasahau mali zako mfukoni

5. Usivae viwalo mjini
Kama kariakoo n. K
Vaa kawaida, Toka na pensi na nguo za kawaida
Ukivaa viwalo wahuni watakusoma wewe ni mgeni na hakika utaibiwa

6. Epuka kuongea na mtu usiyemjua.
Huwa wanakuja wawili au watatu wanakuzubaisha na story na mwingine anakuchomolea mfukoni na kuchukua vitu vyako

7 Usiokote pesa mjini
Ukifika mjini Kuna msongamano Usiokote pesa kabisa
Huwa wanatega na ukiokota wanakuzushia umewaibia, hivyo kila ulicho nacho mfukoni kitakuwa halali yao

8. Usitembee na pesa nyingi mjini bila sababu
wezi wa Sasa wanatumia ushirikina, unaweza uchukue tahadhari zote ila upigwe finger kimazingaombwe
 
Back
Top Bottom