SoC04 Namna ya kufikia malengo ya melinia

SoC04 Namna ya kufikia malengo ya melinia

Tanzania Tuitakayo competition threads

Amos robert

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
3
Reaction score
2
NAMNA YA KUFIKIA MALENGO YA MAENDELEO YA MILENIA

Malengo ya maendeleo ya milenia ni seti ya malengo yanayolenga kuboresha maisha ya watu duniani kote.ingawa malengo yenyewe yamebadilishwa na malengo endelevu ya maendeleo (SDGs),bado tunaweza kujifunza na kuweka mikakati jengefu kufikia malengo hayo.

Tanzania ni moja kati ya mataifa 189 yanayo jikonkoja kuweza kufikia malengo nane ya maendeleo ya milenia (MDGs). Ila mpaka sasa bado misingi yake haijakaa sawa

Kuweza kufikia malengo ya maendeleo hasa katika muktadha wa Tanzania nchi yoyote, unahitaji mkakati thabiti na jitihada kubwa zinazoshirikisha serikali, mashirika ya kiraia, sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

Ninikifanyike kwasasa?

Hapa kunahatua kadhaa ambazo zinaweza kusaidia kufikia malengo haya ya maendeleo ya milenia nchini Tanzania

1. Ushirikiano; serikali inapaswa kushirikiana na mashirika ya kiraia, sekta binafsi na taasisi nyingine kutengeneza mikakati thabiti ya kufikia malengo hayo kwa asilimia kadhaa mpaka sasa Tanzania imefanikiwa kwa kiwango kikubwa juu ya hili maana mpaka sasa ajira nyingi za watanzania zinapatikana ndani ya mashirika binafsi na mashirika mengi ya kiraia

2. Elimu; kutoa elimu na uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa malengo hayo na jinsi wanavyoweza kuchangia katika kuyafikia. Kupitia ushirikiano na mashirika ya kiraia ambayo kwa asilimia kubwa yanatoa elimu elekezi kwa raia wake

3; kupunguza umasikini; ili kufikia lengo hili serikali inapaswa kuanzisha mipango ya kijamii na kiuchumi ambayo inaweza kuwasaidia masikini na kuwatolea fursa za kujiendeleza kama vile mafunzo ya ajira binafsi kwa raia wake hasa kwenye idara ya kilimo na ufugaji

4. afya na lishe bora; kutoa huduma bora za afya na kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora kwa watu wote na hasa familia za vijijini

Katika hizi MDGs chache nitajikita Zaidi kuelezea mdgs mbili kati ya hizo chache nilizo orodhesha , nikijikita Zaidi ni kwa namna gani nchi kama Tanzania itaweza kuyafikia maleongo hayo

Afya na lishe bora;

Lishe bora ndio msingi wa afya njema kwa jamii husika,na ndicho kiini ya maendeleo yeyote yale ya familia,jamii,kijiji,mkoa na hata taifa kwa ujumla, yote haya yatafikiwa endepo serikali itajikita kufanya mambo ya fuatayo

Kutoa elimu elekezi namna na umhimu wa lishe bora na jinsi gani jamii inaweza kuifikia na kuishi katika afya njema, kwani jamii kubwa Tanzania inaishi vijijini sehemu ambayo wengi wao hawajui ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa na afya njema maana hata huduma za kijamii tu kama vile shule,hosipitali na miundombinu yote ni mibovu, na ukizingatia ndani ya kata moja unakuta kuna zahanati moja nayo ina wahudumu wasiozidi watatu na pengine mmoja tu,jambo ambalo linapekea kuto kizi haja za wanajamii wanayo izunguka hiyo zahanati

Nini kifanyike ili kulitatua hili; serikali inapaswa iweke nia na udhubutu wa kuajiri wataalamu wengi wa idara ya afya katika mitaa, yaani kila mtaa ndani ya kata kuwe na mtaalamu wa idara ya afya ambaye atapangiwa majukumu yake kuyafanya ndani ya familia kadhaa na atakuwa na uwezo wakutembelea familia moja hadi nyingine kwa kuhakikisha mtaa wake uko salama na una afya njema, na kwa dharura yeyote katika moja ya familia hiyo ataweza kupigiwa simu na kufika ili kutoa huduma katika familia husika, kwani mpaka sasa kuna namba kubwa ya wataalamu wa idara hii nabado wapo mtaani bila ajira, hivyo serikali yetu ikilizingatia hili,jamii yetu itakuwa salama na yenye afya njema hivyo kuimarisha maendeleo ya nchi kwa ujumla,kwani palipo na afya kuna maendeleo

Hoja ya pili ni jinsi gani serikali inaweza kupunguza umasikini kwa wananchi;

Serikali yetu inapaswa iliangalie kwa namana ya kipekee swala la kuboresha idara ya mifugo, kwani ni idara pekee inayoweza kujenga taifa katika nyanda za kiuchumi na kupunguza umasikini, kwasababu nchi yetu mpaka sasa ina idadi kubwa sana ya wataalamu wa mifugo, lakini nchi kwa ujumla ina mifugo zaifu isiyo kidhi viwango vya kimataifa vya uzarishaji, na hata hivyo bado haturuhusiwi kuuza nyama katika matifa yaliyo endelea yote ni kwasababu tu ya uwepo wa magonjwa erndelevu yenye mazara kwa binadamu (zoonotic diseases).

Nchi zilizoendelea kama vile USA,DENMARK,GERMAN, zimeweza kutokomeza haya magonjwa ingawa hazina wataalamu wengi wa idara hiyo kama ilivyo kwetu, badara yake zimeanzisha mfumo wa kuajiri wataalamu hao kutoka mataifa ya nje ikiwemo Tanzania, mpaka sasa kuna Zaidi ya wataalamu wa mifugo 400 kutoka Tanzania walio patiwa ajira katika nchi hizo, na bado zinazidi kutoa ajira hizo,

Serikali isipo kuwa makini na hili tutajikuta wataalamu wetu wote wanaishia kuleta maendeleo katika nchi zilizo kwishwa kuendelea,maana wanapo baki hapa wanakosa ajira ingawa utaalamu mmewapatia wenyewe, mfano muajiriwa mmoja kwenyue shamba la mifugo anaweza kuzalisha nguruwe 300 kwa siku, kukamua maziwa Zaidi ya lita500 kwa siku .kulisha na kuokotota mayai Zaidi ya trayi 300, jambo ambalo kama Tanzania ingeweza kuwekeza kwa namna hii hawa wataalamu wetu wanao kimbilia kwenda kuajiriwa huko na kuhudumia mashamba ya huko na kujenga nchi za watu ingawa utaalamu huo wameupata hapahapa nchini itaweza kufikia lengo la nchi, kwani niaibu kubwa kwa nchi kama Tanzania kuwa na uwezo wa kuzalisha wataalamu wa kariba hii lakini inashindwa kuwa tumia kadiri ingali inawagalamikia kuwapataia elimu hiyo kwanini inashindwa kuboresha mazingira ili iweze kuwaajairi na kuwatumia kama ngazi ya kuleta maendeleo katika jamii?

Kwa kutoa ushirikiano na mashirika ya kiraia,watu binafsi serikali iruhusu watu hawa kuwekeza na kuwapatia fedha za ufadhili na kuboresha uzalishaji na usimamizi wa mifugo ndani ya nchi hii, ukiwa na mashamba bora yaliyojikita kibiashara Zaidi hata magonjwa ambukizi kwa binadamu (zoonotic disease) yanaweza kutoweka na hivyo kuruhusu mazao yatokanayo na mifugo kuuzwa katika dola, kwa mantiki hiyo nchi itapata fedha za kigeni kwa wingi ita boresha uchumi wa raia na kupunguza gepu la umasikini ndani ya nchi

Juhudi inazo tumia serikali iweke juhudi hizohizo kudumisha ushirikiano wa kiraia na mashirika binafsi,kutokomeza ujinga na kupunguza umasikini na kuimarisha afya bora kwa kila raia,nchi yetu itaweza kufikia lengo kuu la kiuchumi la maendeleo ya milenia.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom